Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Japo kuwa humu zingine zina chumvi ila nimejifunza

2019 nikiwa sina lile wala hili kuna jamaa yangu akaniambia twende tukazamie migodi wapi hiyo Msumbiji basi tumefika kule tukapata kisehem tukapiga kama Zari hivi tukapata mzigo kwenda kupiga bei
Umetema kama m630 ukija kupiga pasu mtu mbili kama m300

Tokea hapo tukakataana urafiki kila mtu aliingia njia zake mana jamaa yangu akadai tukawekeze mim nikaona kuzeeshana mapema huku mi nikaenda zangu dar bila kupitia hom

Fika dar mkwanja si upo kwa bank nikakodi gest nzima nikatafuta mabamnsa kwaajili ya ulinzi tafuta pisi kali kama 10 hivi wakiwemo na mastaa wakike watatu nilikaanao pale gest kwa siku 10 na kubakiwa na laki mbili ya nauli ya kurudi hom mbeya fika hom nikala msoto wa ajabu haijawahi tokea toka nije duniani toka anga za mbali mwaka ukapita nakutana na jamaa yangu ana kampuni yake songea ya usafirishaji mizigo scania kama 23 kumbe mwenzangu aliwekeza kule kele kwenye migodi

Sio siri maumivu yalizidi kusikia hivyo nikamwomba anipe nafasi ya udereva kwenye kampuni yake mana nilikuwa nimepitia huko kabla
Kwakuwa tulikuwa kama ndugu

Akaniambia hapana siwezi kukupa nafasi tena asee kusikia hvy maumivu yalizidi nikajiona sifai nimetengwa na dunia baada ya hisia kunishinda nikatafuta sumu ya panya nikaenda mbali kdg na hom nikanywa
Imepita dakika mbili mwili ukaanza kunyong'onyea macho yanaanza poteza nuru machozi yakinilenga nikikumbuka yote niliyoyafanya ,
Nikasema Mungu naomba unisamehe kwa yote niliyokufanyia ambayo hayakukupendeza

Punde si punde nikiwa kwenye hali hiyo akatokea jamaa yupo na kipkpk akawa anasikia kama kilio hivi cha kugurumia sikujua kilichoendelea ila nilijikuta hospitali nimewekewa ma dripu tazama pembeni jamaa yangu yule wa migodi nimekaa hospitali siku sita

Nilivyokuwa fresh jamaa akaniambia sasa nazani umepata funzo kwenye maisha yako akaacha hom m2 kwaajili ya matumizi akanichukua tukaenda migodi akanipa eneo na kuniambia pambana

Nikatafuta nyoka yaani wafanyakazi lugha za migodi hizo, tukapiga kazi Mungu si asumani nikapata jiwe la pesa ndefu nakumbuka waliungana kama wanunuzi wa madini watatu kuuchukua ule mzigo nikawapa wale nyoka m200 kila mmoja, walikuwa nne nikaenda kwa jamaa akanipa somo jinsi ya kukaa na hela isipukutike hovyo bila kukusudia nakumbuka pesa yote aliniachia ninapo sema pesa ni pesa kweli

Akaniagizia kama Volvo za mizigo 14 hivi za kichina akawa anazisimamia yeye si unajua watu wa nchi hiyi wakijua unapesa ukikoswa na majambazi basi yatakukuta yale ya jamaa wa mtwara na polisi alijinyonga kwa taulo nchi hiyi ni mwiko kuwa na pesa za ghafla basi nikajenga ka nyumba kakisasa kwajili ya wazazi, fungua pub ya nguvu mbinga na dar anzisha kiwanda kidogo cha unga songea hayo yote nimefanya kwa mgongo wa jamaa sikutaka nijulikane kama nina pesa alafu nikamwambia nipe kazi kwenye hiyo kampuni yako nikawa kama dereva mtiifu baada ya wiki tunakutana kwa siri kujadili hali ya uchumi wetu na mpaka sasa hakuna anayejua mm nina shera kwenye kampuni ya jamaa zaidi ya family yangu maisha yangu ya kawaida sana na hata kwenda kwa miguu kazini kawaida kukaa kijiweni kucheza bao draft kawaida yote haya nimejifunza niliyopitia jamaa wanajua mm ni mwajiriwa wa rafiki yake na kuongea ooh alipata hela kachezea mpaka akanywa sumu ila hawajui kinachoendelea sina cha kupoteza ila nimejifunza sio hayo tu kuna mengi ndani yake ambayo ukifuatilia nyuz zangu utawapata japo nilididimia hapa katikati ila nimekaa sawa

Nb kufilisika sio mwisho changa upya karata zako yote yanawezekana mwanaume pambana kisawasawa acha kulia lia sijui ndio basi kazaaaa kubali kufa ukipambana acha kuwaza waza pambana mpaka uache alama kwenye dunia ameen

Na huu ndio ukumbusho wa picha kati ya pesa ambazo tulikuwa tukigawana hukoo machimbo enzi hizoo nikiwa kwa digar na jamaa zangu[emoji116][emoji116]2020View attachment 2098320
Wewe ni katika waliopangiwa kua na maisha bora kuna uliowakuta wakipambana umewapita hongera
 
Mimi ndio ngedere kabisa nilifanya kazi kwenye kampuni ya gas ndani ya miaka mi3 nilipata kama milion 10 nikanunua pikipiki ya kutembelea nikawa kazi yangu kuwafata mademu na kwenda kula bata beach demu nikimpata mtandaon hata awe anakaa Kibaha namfata na pikipiki kiukwel sikuamini kama ile hela ingekuja kuisha nilikuwa naiona nyingi sana kumbuka mii nmetokea familia ya kimasikin hivi nnavyoandika hapa nmerudi naishi home kwa baba na mama sina hata mia mfukoni

Unaendeleaje mkuu[emoji23][emoji23]
 
Ha ha ha,nilikua na kikazi kimoja kila siku hela ya maji ya kunywa 100,000 na kuendelea,
nakumbuka nimekula ulabu toka 2000-2010 non stop daily,

kweli pombe sio chai jameni,acheni nilime haya majaruba tu

[emoji23][emoji23]
 
Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.
Leo tar 1 nina laki moja tu..wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa..niliowasaidia wamenitupa.
Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.
Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira

I hope umetusua tena my brother
 
Hongera kwa waliotoa uzoefu wao kwa madhira waliyoyapitia, ni funzo kubw na zuri sna kwao na wengine. Na hivyo kuna watu watapata kujifunza na kuepuka kufanya makosa kwenye utafutaji.

NOTE.
Nikiwa nakamilish kuleta story yangu hapa, Krb asilimia 90+ wameeleza wanawake kuwa chanzo cha anguko Lao. Nilivyokwish chunguza na kuona khs wanawake, Ni kwamba unaweza kuw hata na M200, lkn ukijiingiza kweny uchakaji wa mbususu, hata kama utapig wawil watatu, na ukawa unawahonga elf 20@,

Lkn mwisho wa siku wawez jikuta pesa zimepukutika na michongo haieleweki, Kinachofanyik hapo ni kwamba Tendo la ngono ni mkosi/ laana, dhambi,/ umasikin ambao unapukutish sn,
Zaid kama hujui kuyaon mambo , ktk ukimwengu wa kiroho , ni ngumu kuelewa.

Pili, Luna wadau wanasema pesa ya mkopo haifai ktk biashara, tunaomba wataalamu walete UFAFANUZI hapa,
 
Kuna vitu haviko sawa
Alipata mil300 2019, adi unakutana nae tena alikuwa na scania 23, apo ni kama mwaka nyuma ina maana 2020 hivi au 21 mwanzon, yani baada ya mwaka moja akawa na scania 23, kuna uongo apa, maana kichwa kimoja cha scania ni mil70 mpaka 300 kutegemea na aina na upya na scania na treller ni kama milion100, sasa huo uongo sijui unautetea vipi

Umu kuna uongo mwing unanukia
Kasema za mchina
 
Nikiwa nimemaliza chuo sina hili wala lile, niko kitaa nikijipanga, nikachangiwa na ndugu zangu mtaji wa milion 4 point something huko, niende nikafanye biashara ya mchele toka Moro vijijini kuleta mijini na kusambaza kwa bei ya jumla.

Biashara mwanzo ilienda vizuri, mwisho wateja wangu wa siku zote wakawa wakopaji wangu wakubwa, malipo yakawa ya kuzungushana, nikawa mkali kidogo ila kwa bahati mbaya pesa ikawa ndogo kwenye mzunguko wangu, sinunui tena zile kilo nilizoanza nazo kwa wakati, mambo yakawa tofauti kidogo, nikaenda weee.

Mwisho wa siku nikachanganyiwa mchele kipuuzi kabisa na mtu ambae nilikua namuamini, nikajikuta nipo na mchele wa vitumbua na jamaa yule kakimbia, hapo ndio ukawa mwisho wangu, nilifilisika kama kuku, ndugu zangu hawakunielewa tena, nilipata stress kama tani 7 hivi.

Wakati tena nikapataga milion 3 kwa enzi zile haikua haba aisee, nikawa naishi vizuri tu, hizo elf 10 kwangu zilikua buku, sina cha kujibania kwa kweli, kuja kustuka nimenunua friji na tv tu vya geto tena ka friji kale kadogoo kabisaa, hela yotee imeisha katika njia zisizoeleweka, nilichanganyikiwa tena, sina nidhamu ya fedha.

Mwisho nikarudi zangu kusoma tena chuo ndio nikaja kutoboa kwa njia zingine kabisa kwa kutumia kazi niliyosomea.

Je, wewe unakumbuka vipi? Nini kilikupata?
Maisha yana ups and down za kutosha
 
Sasa unadhani ukipata dollar million moja utafanya starehe hapa bongo..sii utaanza kusafirisha wanawake dubai ukagegede....starehe hazina mwisho ata hiyo million dollar unafilisika tuu ukiendekeza starehe
Idris Sultan alipata Tsh 500m ambazo ni zaidi ya U$D 200,000. Zilienda wapi? Na kama mtu anaweza kuchezea USD 200,000 watu wanashangaa nini mtu kuchezea USD 1m? Umesema vizuri kabisa starehe hazina mwisho. Ukiwa na USD 1m, demu akikuambia umlipe 50m utaona mbona hela ndogo sana hiyo..?
 
Mlio rudi kwenye gem tustuwane wakuu

Sioa lazima iwe kama ulivokua walau utoke kwenye msoto tu tupeane mbinu
 
Nina mjomba wangu mmoja hivi alikuwa anaimba imba kwenye hizi bendi za muziki kipindi hicho. Unawataja ma papaa, watu wazito alaf wanakutunza pesa ndefu. Sasa sijui alipigaje hela, ila alikuja kumiliki pesa ndefu. Mjini akawa yeye ndio Don, kila kona ana demu. Muda wote kachomekea, starehe mwanzo mwisho. Baada ya miezi kadhaa akafulia mbaya, hadi soo.

Akapotelea migodini. Huko alikaa kama miaka miwili au mitatu. Akapiga mshindo wa maana. Kurudi town ana hela chafu. Akiingia bar anatoa watu wote, anaikodi bar alaf anabaki na wapambe wake tu. Kuna siku mlevi mmoja wakati anatolewa nje kwavile bar imekodiwa na anko, yule mlevi alitukana. Anko akaomba aitiwe huyo aliyetukana. Kabla hata hajamwangalia usoni, akamuagiza mhudumu ampe yule mlevi kreti za bia sawa na urefu wake. Siku nyingine anaweza akatoa order kuwa wahudumu wote wa bar wabaki na pichu tu na sidiria. Haikupita miaka miwili akafulia mbaya.

Alivyofulia akapotea bila kujua kaenda wapi. Akaja kuibuka baada ya miaka kadhaa. Siku anakuja home kanawiri kichizi, akampa bi mkubwa (mama angu mimi) busness kadi yake ambayo inaonesha yeye ni engeneer na anamiliki kampuni ya ujenzi wa barabara (anko aliishia la saba) [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sasa hivi ameshaoa na ana life zuri tu. Ukimpigia simu story zake ni either yupo njiani anaenda makao makuu Dodoma au yupo njiani anatoka kule. Ukimpigia simu asipopokea, badae akikuchek utaskia alikuwa kwenye kikao na Mama ndio maana hakupokea (hapo anamaanisha mama Salma Kikwete)

Mara ya mwisho kumpigia simu aliniambia "Ngoja naingia Usalama, ntakuchek badae, siunajua ofisi za watu hizi" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mungu akupe maisha marefu anko.
Huyo legend hahahah
 
Nimesoma comments zote kiukweli zinafurahisha,kuhuzunisha na kukejelisha pia[emoji28].

Ebu mie niwape yangu japo Mungu alijua kurudisha Upinde kwangu baada ya kuuvunja wa mwanzo.

2000's (censored) nipo mwaka wa Mwisho chuo,napokea simu ya mzee "maliza uje kuna kazi nimekutafutia uje uanzie maisha".

Mwana tii!! Nadondoka job kwa cheo kikuubwa (ambacho wewe kama unge apply wangetaka 5 yrs experience,4.5+ GPA na makolokolo kibao)[emoji28],mie hiyo nimezama sijapata hata gamba chuoni litakuja mbele ya safari chezeea!!

Salary per month around 2M+ na mashehena kibaoo hapo toa madili na vishoka somewhere!!

Mchawi/wa kumlaumu ni "dereva wa bajaji" dogo junk flani hivi ..mwanzoni mwanzoni hapo natafuta pipi tu sijavuta hata kigoda cha mzungu aka Ndinga...huyo dogo ndio alikuwa ananitoa home mpaka job na kunirudisha kwa malipo ya mwezi kipande cha MIKOCHENI hapo...

Kipindi naanza job full kupiga kazi hasa mpaka mida ya saa mbili usiku hukoo ndio naachia ofisi...dogo wa bajaji hyo ratiba alikuwa anaijua...pia alijua mausha yangu yote kama nipo single...siku ya siku akanichoreshea kiramani flani "braza kwaninj uteseke kurudu home night wakat kuna pande flani unaweza kupozi na ukala matunda ya peponi"[emoji28].

Kwa kuanzia nikapelekwa "Massage Parlor" moja matata mnooo yani yani yani yani acheni tu.!!!

Kuingia watoto wa kila rangi afu wamesimama kama mwibaa hasaaa....(wazuri)..dogo akamuita matroni[emoji28][emoji28] "braza haya mambo ni mpya,mpe Menu atakayo shindwa kuisahau milele" ...matroni[emoji860]"yupo njema?!!"...dogo[emoji860]"weee mama wewee mie sitembeagi na wauza matunda[emoji28]"

Matroni[emoji860]"kama vipi na mie naingia mzigoni na vijana wangu kama 2 3 hv tusimamie show ya mgeni muheshimiwa mpya"

Dogo[emoji860]"fanya hivyo utakuja kunishukuru badae mchizi ana jiwe hasaa"

FUPISHA STORY:

Wanangu ee wa JF
Watoto wa hiyo parlor walichukua namba yangu wakaanza kuwa wananitafuta privately kila mmoja anataka kutumia opportunity kibinafsi.....

Dogo akanipeleka saloon hiyo wananyoa Mastaa tu full vidada vya instagram na bongo movie kibaoo hapo

Picha linaanza naingia tu kutupa jicho mwanangu Byser huyo hapoo mbele!! Sijacheki pembeni Nyandu tozy yule paleee naanza kuambaa ambaa Naona kiti cha kupumzikia ka chill Young dee paka rapper!!!

Nilivyotoka kunyoa pale naanza kupokea meseji kibao "braza mie msanii,najua kuimba nisimamie"
Mwingine "kaka mie ni model nahitaji support ya mavazi,location na cameraman wa maaana"!!

ITAENDELEA
But now Mungu kanipa second chance although najua laana zote za hapa bongo kupitia huyo "dogo wa bajaji"....
2000's bajaji zilikuwepo? Nyandu tozi?? Hii chai ina tangawizi nyingi
 
Back
Top Bottom