Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Nlifilisika kabisa kipind cha korona biashara ilikuwa ngumu had nikauza frame kkoo, mke akaniacha , wana na baadhi ya ndugu walinicheka asa ivi nimerudi kwenye form hao hao wanaomba msaada nawazoom tu, uyo mwanamke anajifanya mwema asa ivi kunishaur sina kinyongo na mtu ila nimewajua vizur yupi wangu yupi si wangu.
Nimetoa mchozi! MKE kabisa alikuacha?
 
Mwaka 2011 soko kuu mwanza nikiwa ninauza nafaka zikiwemo karanga, njugu, choroko,dengu,ufuta,ulezi,uwele,mtama,maharage na kunde.

Kamtaji kalivyokuwa nikawa naendea karanga tabora tani kadhaa nauza jumla. Nilipata pesa kwa njia hiyo. Basi kufkia December karanga zikawa chache Sokoni hivyo mwenye nazo alipiga pesa balaa.

January 2012 nikaingia poli kusaka karanga mpya ili niwahi bei sokoni. Basi nikapata kama gunia 30 (tani 3). Kufkisha Sokoni ziligombaniwa kama nyama. Nikaona pesa si hii apa. Nikazoa msingi wote around kama 22.8m. ili nikapige mkupuo mmoja nije nitulie.

Kuleta mzigo nafika Sokoni nakutana na fuso 6 zinashusha mzigo. Sasa kila mmoja ashajua ni dil acha bei ishuke. Nilijikuta karanga nimezinunua 2300 natakiwa niziuze 1600. Sasa nilipoharibu nikapiga mzigo stoo kwamba bei ikikaa sawa nitauza duh! Kumbe mzigo si haujakauka vizuri, nilikaa kama wiki nafungua stoo nakuta mzigo wote umevunda... Duh!
Daah..pole sana biashara za nafaka zinahitaji mahesabu makali sana ya kuliwahi soko.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo akili inarudi pale receipt inaposoma salio lako ni laki mbili [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] ndio unajiuliza hii niiiinunuliee halafu jibu linakujia pale pale haitoshi baada ya siku mbili unaenda toa laki na nusu halafu hukanyagi tena bank na ukipita karibu ni upande wa pili wa Barabara [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binasfi cjawahi filisika lakin nakili wazi kabsa kma asingekuwa mke wangu kuniongoza vema kwenye mambo ya kheri mhhh bac mpaka sasa ningekuwa nishafilisika zamaaaaan!! Mwanamke wangu shujaa wangu hela natafuta mimi lakin matumiz napangiwa hela inayobaki tunafanyia jambo la maana kabsa ningekuwa mimi mwenyewe nicngeweza
Hongera jamaa..wengine wake zetu ndio wametuletea umasikini..acha tu ukipata mwanamke mwenye akili ya utafutaji na awe na tako utaenjoy sana..

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mimi wakati tunakaribia kufunga ndoa tu na mume wangu akafukuzwa kazi ,kazi iliyokuwa ikimlipa vizuri sanaaaa weee nikakaa nikajiuliza niendelee na hii ndoa au lah maana nilikuwa nawaza mimi nafanya kazi kwa wahindi mshahara wangu hauwezi kulipa kodi ya nyumba na sisi tukala nikamuomba Mungu nikasonga mbele na ndoa aisee si mchezo yani ukipokea mshahara ushaisha unaanza upya yani kila ikifika mwisho wa mwezi ndo machungu yanaanza.
Nikapata mimba hapo mume haingizi hata senti tano ila akawa tu ni mtu mzuri hana makwazo kwahiyo tukawa tunaongea lugha moja.Wakati kwa kujifungua ukafika ile nimemaliza mwezi mimi ni HR boss wangu kanipigia simu tukaongee kwenda ananiambia inabidi tufunge ofisi hataweza kuendelea kulipa wafanyakazi hivyo ni bora alipe watu akiwa bado ana pesa aiseee tulikuwa sehemu nilikuwa sielewi nini naongea mana nilikuwa nawaza mtoto nyumbani mwenzangu bado hajapata kazi [emoji1544] nilijikaza nikamjibu boss wangu sawa mana mimi ndo natakiwa kwenda kubreak the news.

Turudi nyuma kidogo mwenzangu kuna pesa aliipataga zamani basi akanisaidia kiasi kikubwa kuanzisha biashara yangu (na hii ndo sababu niendelee mbele na ndoa mana nilishajua ni mtu wa namna gani). So wakati haya yote yakiendelea tuliyokuwa tukiiendesha kwa hasara lakini sababu nilikuwa na kazi nikawa naendesha hvyo hivyo najipiga tafu kupitia kazi yangu ya kuajiriwa basi nilivyoona familia imeongezeka nikaona sitaweza kuihudumia biashara nikataka kuifunga kumbe Mungu ananichelewesha kuifunga kwani anajua nitakosa kazi,kazi ilivyoisha bahati nzuri nilikuwa nimepata maternity yangu karibuni nikachukua kiasi nikatemgeneza ofisi kidogo na tulipofunga ofisi sababu nilikuwa maternity nilipata mishahara kama mitano hvyo plus kiiunua mgongo basi tukakaa na mwenzangu tukaenda buguruni tukanunua kila kitu cha ndani at least kitakachotupeleka kwa miezi mitatu tukiwa tunajitafuta.

Mungu ni mwema hatuna maisha kama ya zamani lakini nimewekeza akili na kila kitu kwenye ile biashara yangu na sababu nipo mwenyewe naifanya mwenyewe na pesa sasa inaendesha maisha + na mume wangu anafanya kazi zake hakosi pesa za chakula.

Tusikate tamaa na kumuomba Mungu mana kila anapokupa jaribu anakupa na mlango wa kutokea mlango ni akili zinazokuongoza kutafuta namna ya kuzitatua na tujitume na kutokata tamaa.
Na zaidi kwenye maisha kukosa ni kawaida kama sio leo ni kesho.
 
Mkuu nimefukuzwa kazini kwa madai ya utoro maana nilipata issue moja,emergency nikaomba ruhusa nikanyimwa ikabidi nisepe hivo hivo,hasa kupata barua ya termination hawataki kunipa.
Hivyo na nssf yangu ngumu kupata
Habari, umechukua hatua gani baada ya tukio hilo? Kama siku 30 tangu wakutimue hazijafika, nicheki PM naweza kukushauri kitu.
 
Mimi wakati tunakaribia kufunga ndoa tu na mume wangu akafukuzwa kazi ,kazi iliyokuwa ikimlipa vizuri sanaaaa weee nikakaa nikajiuliza niendelee na hii ndoa au lah maana nilikuwa nawaza mimi nafanya kazi kwa wahindi mshahara wangu hauwezi kulipa kodi ya nyumba na sisi tukala nikamuomba Mungu nikasonga mbele na ndoa aisee si mchezo yani ukipokea mshahara ushaisha unaanza upya yani kila ikifika mwisho wa mwezi ndo machungu yanaanza.
Nikapata mimba hapo mume haingizi hata senti tano ila akawa tu ni mtu mzuri hana makwazo kwahiyo tukawa tunaongea lugha moja.Wakati kwa kujifungua ukafika ile nimemaliza mwezi mimi ni HR boss wangu kanipigia simu tukaongee kwenda ananiambia inabidi tufunge ofisi hataweza kuendelea kulipa wafanyakazi hivyo ni bora alipe watu akiwa bado ana pesa aiseee tulikuwa sehemu nilikuwa sielewi nini naongea mana nilikuwa nawaza mtoto nyumbani mwenzangu bado hajapata kazi [emoji1544] nilijikaza nikamjibu boss wangu sawa mana mimi ndo natakiwa kwenda kubreak the news.

Turudi nyuma kidogo mwenzangu kuna pesa aliipataga zamani basi akanisaidia kiasi kikubwa kuanzisha biashara yangu (na hii ndo sababu niendelee mbele na ndoa mana nilishajua ni mtu wa namna gani). So wakati haya yote yakiendelea tuliyokuwa tukiiendesha kwa hasara lakini sababu nilikuwa na kazi nikawa naendesha hvyo hivyo najipiga tafu kupitia kazi yangu ya kuajiriwa basi nilivyoona familia imeongezeka nikaona sitaweza kuihudumia biashara nikataka kuifunga kumbe Mungu ananichelewesha kuifunga kwani anajua nitakosa kazi,kazi ilivyoisha bahati nzuri nilikuwa nimepata maternity yangu karibuni nikachukua kiasi nikatemgeneza ofisi kidogo na tulipofunga ofisi sababu nilikuwa maternity nilipata mishahara kama mitano hvyo plus kiiunua mgongo basi tukakaa na mwenzangu tukaenda buguruni tukanunua kila kitu cha ndani at least kitakachotupeleka kwa miezi mitatu tukiwa tunajitafuta.

Mungu ni mwema hatuna maisha kama ya zamani lakini nimewekeza akili na kila kitu kwenye ile biashara yangu na sababu nipo mwenyewe naifanya mwenyewe na pesa sasa inaendesha maisha + na mume wangu anafanya kazi zake hakosi pesa za chakula.

Tusikate tamaa na kumuomba Mungu mana kila anapokupa jaribu anakupa na mlango wa kutokea mlango ni akili zinazokuongoza kutafuta namna ya kuzitatua na tujitume na kutokata tamaa.
Na zaidi kwenye maisha kukosa ni kawaida kama sio leo ni kesho.
Mmeo alifukuzwa kazi kwa kosa gani…?
Mliendelea na ndoa lakini ndoa hamkufunga…?
 
Mwaka 2012/2013 tulipiga 50M, mimi na msela wangu kwenye company moja ya vinjwaji huko Kanda ya Ziwa! Tukagawana 25M!

Ilikua Ijumaa,nikakata fast jet,faster Dsm,saa kumi na moja tukasepa Mwanza,bondeni hotel pale magomeni ndiyo nikawa nalala pale! Baada ya kufika dsm saa moja hivi za jioni,mwanangu mmoja alikua Sinza Mgabe pale,fanya Mpango Shangazi Ezekiel alichezea koki kwa siku hiyo,hadi asubuhi kwa laki tano,hapo toa gharama ya vinjwaji na chakula plus ticket ya ndege,chumba cha kulala,maana yake 2M inakata hiyo, Basi bwana,kesho yake nikashinda nimelala tu, kozi ya uchovu na Pombe na gegedo! Usiku tukazama Casino pale Palm Beach,tukapigwa laki 5,tukaenda the Grande tukapigwa laki 5,basi hapo Mimi nasema haina shida pesa ipo! Tukaenda The Princess pale IT Plaza,aiseee tukapiga 5M! Jamaa akasema tusepe,hapo nishalewa,kulikua na demu flan hivi Mfilipino,alikua anauza nikasema twende,bei USD 500! Nika change pale pesa,nikawa na USD kama 100 hivi! Jamaa yangu akasepa zake,kaniacha,nikachukua yule demu,nikaenda kula!

Kesho yake nikarudi pekee yangu Casino,si wakanila 3M! Nikaondoka kurudi Hotel,hapo kwenye 25M bado kama 20M hivi!

Nikarudi Mwanza,fanya fujo sana,nikaja shituka nina 10M! Nikanunua kiwanja na furniture za ndani pesa yote kwisha! Nikasema sasa hapa tupige deal tena nianze kujenga,deal likawa dirisha,kikaota,nikasepa zangu shytown! Hangaika sana ramani hazisomi! Ikabidi niende tu kwenye company za wavaa overall! Maisha na pesa ni kama shetani hivi hua anakuja!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ushamba na ulimbukeni wako tu, hata usimsingizie shetani
 
Hichi ndo kilichosababisha mpaka leo ile 1,300,000 nikaipeleka kununua hisa mwezi wa saba.. Ungekuta ile hela imeshapotea mpaka sasa hivi.. Ni kitu pia nimejifunza.. Usikae na cash kabisa..

Ila na mimi nliwahi kupoteza kama 4,000,000 miaka 2 iliyopita.. Sitaki kukumbuka maana niliishiwa mpaka kula ilinishinda. Ilikuwa kuna wakati nashindia 1000 kwa siku. Asubuhi maandazi ya 500 mchana napitisha nakula mihogo ya 500 usiku imetoka.

Ndani ya miezi miwili nilichuja ilikuwa nikitembea barabarani gari kubwa ikipita napepesuka kabisa na kupulizwa na upepo tu. Acha kabisaaaa..

Huku kodi ya nyumba nadaiwa miezi mitatu sijalipa mwenyenyumba kila siku anakuja kunigongea asubuhi.. Acha kabisaa wandugu niliteseka mno na maisha karibu mwaka mzima.

Honestly ni kipindi ambacho kimebadilisha mwenendo wa maisha yangu. Nowadays najiona nimekuwa mtu mwenye roho mbaya sana na najiamini sana.. Mtu hata anililie shida wala sishituki maana shida nliyopitia si mchezo yani
Vipi now si ume make money na una enjoy mkuu? Vipi totoz hupendelei?
 
Back
Top Bottom