Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Watu wengi hatujuwi kama kutafuta hela siyo kazi, kazi inayo tugarimu tulio wengi ni kutunza hela, hatujuwi kabisa na ndiyo maana hata upate ml200 bado utafilisika tu kwakuwa hatuna nidhamu ya pesa hivyo tujifunze kutunza pesa.
 
Nikiwa nimemaliza chuo sina hili wala lile, niko kitaa nikijipanga, nikachangiwa na ndugu zangu mtaji wa milion 4 point something huko, niende nikafanye biashara ya mchele toka Moro vijijini kuleta mijini na kusambaza kwa bei ya jumla.

Biashara mwanzo ilienda vizuri, mwisho wateja wangu wa siku zote wakawa wakopaji wangu wakubwa, malipo yakawa ya kuzungushana, nikawa mkali kidogo ila kwa bahati mbaya pesa ikawa ndogo kwenye mzunguko wangu, sinunui tena zile kilo nilizoanza nazo kwa wakati, mambo yakawa tofauti kidogo, nikaenda weee.

Mwisho wa siku nikachanganyiwa mchele kipuuzi kabisa na mtu ambae nilikua namuamini, nikajikuta nipo na mchele wa vitumbua na jamaa yule kakimbia, hapo ndio ukawa mwisho wangu, nilifilisika kama kuku, ndugu zangu hawakunielewa tena, nilipata stress kama tani 7 hivi.

Wakati tena nikapataga milion 3 kwa enzi zile haikua haba aisee, nikawa naishi vizuri tu, hizo elf 10 kwangu zilikua buku, sina cha kujibania kwa kweli, kuja kustuka nimenunua friji na tv tu vya geto tena ka friji kale kadogoo kabisaa, hela yotee imeisha katika njia zisizoeleweka, nilichanganyikiwa tena, sina nidhamu ya fedha.

Mwisho nikarudi zangu kusoma tena chuo ndio nikaja kutoboa kwa njia zingine kabisa kwa kutumia kazi niliyosomea.

Je, wewe unakumbuka vipi? Nini kilikupata?
Kuna watu natamani mungu awafunulie wasome hii thread. Watu wengine wakifulia kidogo tu wanataka mpaka kujiua, wakati kuna malegend humu ni kama walishakufa wakafufuka. Mpaka stori zinatisha. Ukisoma hii thread utajua kumbe kukata tamaa ni mwiko. Imenijenga sana mimi kifikra, mambo ninayopitia ya kukatisha tamaa sana. Jana tu kuna mtu kataka kujiua kisa PhD anayosoma inazingua na kazini washasimamisha mshahara. Ana masters lakini anaona akikosa PhD bora afe. Angesoma hii ingemsaidia sana.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kuna mwanangu mmoja hivi tulimaliza naye adavance,bahati nzuri tukakutana tena chuo udsm,ni chalii ya manyara babati huko,yule jamaa ana balaa,kwanza picha linaanza viatu vyake anavyovaa chuo ni vya advance,mwana mnapata boom wote ila nyie zenu zinakata zoote yeye bado anazo kama asilimia 95 hv ya hela zote..yule jamaa saluti sana anajua sana kumanage hela asee..

Hajawahi kuwa na demu,hali cafetaria ye zake ni wali maharage nje huko,maji anadownload kama kawa[emoji23][emoji23][emoji23]dah yule jamaa alikuwa ananiacha hoi sana..akati kuna mwanangu mwingine yeye ni jangwani sea breeze na yeye kila ijumaa,juis ya parachichi nzito na misosi ya cafetaria 1,mbona mwana alidisco[emoji23][emoji23]ni dereva bajaji leo town hapa

All in all UBAHIRI NDIO SIRI YA UTAJIRI.
Ana mradi gani Hadi hivi sasa tangu mmalize?
 
Ahaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kujitesa kote huko halafu kawa dereva bajaj? Nilijua utasema sasa hivi ana majumba na biashara na ndinga kibao bila kusahau cash money.
 
Kuna mwana tulupangiwa wote mabibo hosteli miaka hiyo ya late 2000's. Mchizi likuwa ametoka mwanza/shy town dah jamaa daily yeye ni kutembea kwa miguu kutoka mabibo mpk campus hana habari na shuttle,Misosi ni RB tu mwanzo mwisho
 
Mwezi wa tatu mwaka jana nikapewa mil 8 za mirathi. Nikawaza nifanyie nini? Wazo langu la kwanza, ninunue shamba porini, nifuge mbuzi na kondooo. Nikaenda minada ya mbuzi na kondooo, nikakuta hali siyo nzuri. Yaani vitoto vinauzwa kwa bei ya mbuzi na kondoo waliokomaa.

Jamaa yangu akanishauri tuchonge mitumbwi na kununua nyavu. Mwanzoni nikapewa tu hela, nikaongeza mtaji.

Nashtuka naambiwa nyavu za 2mil zimeibiwa. Hadi sasa nimebaki na mitumbwi yenye rangi ya tanganyika tu
Daah ungekomaa na plan yako ya mwanzo ya kununua shamba na ufugaji.
 
Bora wewe 70 mimi kuna mtu nimemfungulia salon na niko mwenyewe kwanza na check upepo week nzima imeingia tsh 2500 hahahah saloon ina week 2. Na hlo eneo salon ni mimi tu
Hapo ndipo panafaa sasa,na hiyo biashara itakunyookea siku za usoni mpaka hutaamini. Siku zote ukiona mwanzo mgumu ujue mbeleni ndio kuzuri,ila ukiona umeanza na kitonga tu yani mambo mserereko basi jiandae kuingia shimoni.
 
Ahaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kujitesa kote huko halafu kawa dereva bajaj? Nilijua utasema sasa hivi ana majumba na biashara na ndinga kibao bila kusahau cash money.
Nadhani amemaanisha kuwa yule aliyekuwa akienda Jangwani Sea Breeze ndio amekuwa dereva wa Bajaj
 
Ahaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kujitesa kote huko halafu kawa dereva bajaj? Nilijua utasema sasa hivi ana majumba na biashara na ndinga kibao bila kusahau cash money.
Ama kweli kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti....hapo wamezungumziwa watu wawili tofauti angalia vizuri
 
Nilikuwa Baba mwenye nyumba!;
nikamuuzia mpangaji nyumba na kuanza kuwa mpangaji kwenye ileile nyumba!
Hivi ninavyo andika nimepewa notice NIHAME!
IMG_20211226_190249.jpg
 
Back
Top Bottom