Alipita fresh tu, mpaka sasa ni contractor, wafanyakazi wake wanakuita injinia, nadhan hawajui kama aliishia la saba [emoji28][emoji28][emoji28].
Mwaka juzi tulienda kijijini kwenye msiba. Mida ya jioni palitokea ugomvi, siunajua misiba ya kiafrika,pombe zinakuwa nyingi. Sasa kwenye ule ugomvi, kwa hasira Anko akawa anashika kiunoni kama anataka kutoa bastola, baadhi ya wanakijiji wakatawanyika (wanakijiji wanajua Anko ni usalama wa Taifa). Mkewe akawa anacheka sana kwa kile kitendo, anatwambia "Huyo bastola anaiona kwenye movie tu, hata kuiona kwa macho yake hajawahi, sembuse kuwa nayo?" [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]