Tuliowahi kusomesha Wachumba na hatujawaoa. Tukutane hapa

Kuna Dada ninayemjua wa kitengo cha kemikali, alisomeshwa na jamaa huko milimani yuko hapa town na jamaa ingine
 
P[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana, kwhy badae ulikuja kujua nini khs wale watoto.
Ni wake au walikuwa wa jirani kweli?
Sikuchunguza zaidi, but kulikuwa na uwezekano huyo Baba mwenye hao watoto ndiye aliyemuuzia hiyo nyumba aliyonunua
 
Hapa watajifanya wagumu hawasomeshi ila ukweli ni kuwa wanasomesha sana tu.

Mtusomeshe tu jamani, mengine ni matokeo tu.

Matokeo?

Kila nikitaka kufanya chochote kwa mwanamke akili huwa ina-click je hiki hakitaniumiza huko mbele?

Kiukweli sipendi kuwekeza kwa mwanamke kwa namna yeyote ile

Iwe ni kiasi kidogo cha kati au kikubwa

Sitaki maumivu mara mbili niwaze kimapenzi na mali NO

Wapo waliosomeshwa na waume zao wa ndoa wakahudumiwa kila kitu lakini baada ya chuo ndani ya miezi 6 unaskia flani anafunga ndoa tena

Principle ni moja tu ukitaka kuoa

Muone kama alivyo kama alikuwa hana shule abaki hivyo hivyo mpaka milele,

Kwanini umsomeshe mwanamke?

Mwanamke alikazana na shetani pale edeni

Hawa watu wana mioyo migumu sana

Mimi nikikuoa usitegemee ntakupeleka shule hata iweje

Na hata biashara nikikufungulia nitai-monitor 24/7 mwenyewe na ikiwezekana access ya pesa niwe nayo mimi

Kama tutanunua nyumba na assets zingine kama tuna watoto zitasajiliwa kwa majina yao

Mwanamke unaweza kukaa nae miaka 20 halafu ukashangaa kakijana kanyoa kiduku kanalegeza suruali ndo kanamkaza kadata mpaka basi

Kuna Dada ninayemjua wa kitengo cha kemikali, alisomeshwa na jamaa huko milimani yuko hapa town na jamaa ingine


Aiseeee.
 
Tatizo twajipendekeza. Hawa watu hatutakiwi kuwaamini
 
We jamaa nimecheka sana! We ni nyoko aisee
 
Andishi lako umetiririka kwa mwandiko unaosomeka vyema, hongera sana kwa uandishi murua.

Kuna neno umelirudia mara nyingi katika bandiko lako hili,....'nilikasirika sana'....
Sasa kila nikipima cha kukukasirisha nashindwa kukibaini hapo.

Maana yake ni kwamba, sehemu ya majadiliano ama kubembelezana, wewe ulitembeza umfumo dume kwa kufosi!

Mlikuwa wachumba, ni kipindi mujarabu cha kuchunguzana na kutegana.

Ulivyokuwa unafanya wewe kumchunguza ndivyo alivyofanya na yeye. Na kwa kuwa watoto wa kike wamejaaliwa akili za kutulia, saazingine aligundua mapema kwamba ni wa hovyo na haufai, ndiyo maana kakupokonya mtoto kisayansi.

Ulishikilia bakuli la ugali, yeye akashikilia la mboga na ulipoumwaga, yeye naye akamwaga mboga na kutupa bakuli, yaani hapo ni bilabila.

Tunachosihi sana, vijana muda wenu wa kuoa ukifika, oeni hima bila ya kukaa na kuanza kuchunguzana tabia, matokeo yake huwaga na mwisho mbaya, maana binadamu hatujakamilika, tuna mapungufu mengi ya kila aina na kila mtu na yake.

Hivyo, mnapokaa muda mrefu mkichunguzana huku mkiitana wachumba, matokeo yake huwa ni kumwagana hata kwa vijisababu vidogo kama hivyo ulivyo visimulia katika andiko lako.

Je sababu ulizozitaja, kama ungelikuwa umeshafunga naye ndoa kwa kutumia rasilimali za jasho lako na gharama kubwa ya harusi tangia 'day one', ungelithubutu kuivunja ndoa hiyo kirahisi rahisi, kadri ulivyojisikia wewe bila hata ya mwenzako kuitwa na kusikilizwa, tena stand ya mabasi?

Huyo mchumba asibebeshwe lawama za kusomeshwa na kisha kuingia mitini, hapana.

Hakuna popote uliposema kwamba mchumba wako huyo alikukataa, bali ni wewe mwenyewe uliuvunja uchumba huo kwa ghadhabu na kwenda kuoa kwingine.

Ni nani alaumiwe sasa?
 
Demu/Hawara/Kimada/Girlfriend naye anaitwa MCHUMBA!!! Ninavyofahamu kuna tofauti kati ya mchumba na kimada/hawara/girlfriend/demu, yaani girl/boy friend, mchumba ni fiancèe. Yaani maana yake kuna taratibu fulani za kimila au kiutamaduni zimefanyika barua ya posa imepelekwa au hata mahari imetolewa au na pete amevishwa ktk sherehe/ceremony ya familia mbili zikiwepo, siyo pete za vichochoroni kinachosubiriwa ni ndoa tu ya kanisani au msikitini au ya kimila, si sahihi mwanamke au mwanamme ambaye kwao hawakutambui rasmi kama mume au mke mtarajiwa na hakuna taratibu zozote zilizofanyika, kuitwa MCHUMBA/FIANCÈE, uchumba una taratibu zake otherwise ni hawara, kimada, rafiki, girlfriend au demu tu
 
Mkuu kunywa mkubwa wao bill kwangu
 
Ninakumbuka tukiwa O level kuna bint mmoja mzuri sana alikuwa anasomeshwa na boyfriend wake.

Yule kaka kila Jumamosi alikuwa analeta makulaji, mkate wa Arusha, juice, matunda na kuku wa kukaanga.

Sijui walioana.

Kwahiyo ile mikate ya njano ya mayai tena mitamu na juice za kenya mmepiga sana msivo na huruma
 
Kwa kiasi kikubwa bora hata wewe mtoa mada umepata hata mtoto na pia mwanamke ndiyo anayetaka muoane.

Ila kuna hawa wakuda wengine ndiyo tatizo. Tunajadili hivi, wao wanafanya hivi!

Wakuda wanalazimisha waoe wakati hayo mambo hayalazimishwi
 
Kumbe tunaumizan wenyewe kwa wenyewe halafu tunalaumu wanawake
 

Kwa akili kama zako mkuu subiri kulia tu hamna namna

Hii comment yako inaonyesha kabisa wewe ni mtu wa aina gani

Mkuu kunywa mkubwa wao bill kwangu

Kbla sijaagiza wewe ni KE/ME
 
Mkuu hapa sijamlaumu mtu.
Na kilichosumbua wakati ule ni yeye kuja kukataa kabisa kuwa tulimtelekeza na kwa uzuri, aliona aibu sana nilivyompostia risit zake za ada
 
Mimba, miaka 5 ya mtoto eti bado kuoana?? Kwanza ulipomjaza tu mimba ulipaswa uanze taratibu za utambulisho then ndoa....Kama hujui mwanaume akimpa mwanamke mimba halafu baada ya hapo kile kimya kisaikolojia mwanamke anaona kabisa hapo hakuna ndoa hivyo analea Huku anajipanga na mambo mengineyo ya future yake hata bila wewe. Na isingekuwa rahisi yeye kuishi bila mwanae wakati yuko hai na shule alishamaliza.
 
Basi aliusoma mchezo vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…