Tuliowahi kutembea kwa sababu ya kukosa nauli tukutane hapa

Tuliowahi kutembea kwa sababu ya kukosa nauli tukutane hapa

Ilikuwa mara mojatu.
Wakati wakwenda, nili panda DCM kariakoo sokoni nikafanikiwa kumkwepa konda sikulipa nauli.
Hapo naelekea mikocheni maeneo ya ITV kusaka ajira, nikakaa hadi sa6 mchana bila mafanikio njaa iliniumasana nikaamua 150 yangu niile mihogo na kachimbari.

Kurudi nilitembea kutoka mikocheni ITV mbaka uhasibu cota za bandari.

Daaah, thanks GOD for what you did in my life.
Umefanya njia pasipo kuwa na njia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tushatembea toka Manyara mjini hadi Dodoma mjini (kwa hapa bongo tu)na hatusemi neno,
achilia mbali zile route tulizopiga katika harakati za kuvuka border kwenda SA.....wewe hapa na ubungo tu unaona umetembeea!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miaka hiyo nilimsindikiza girlfriend wangu shuleni kwao alikua akisoma boarding huko sanya juu basi nilispend hela nyingi kweli njiani, nilimfikisha shule tukaagana vizuri na hug za kujifichaficha as shule ilikua ni ya masista, basi wakati naondoka alirudi akanipa elfu tano nikamuuliza yanini hakunijibu akaondoka, basi nilirudi nikapanda hiace mpaka boma halafu niende Arusha cha ajabu ni kwamba baada ya kujisearch sikuwa na hela nyingine yeoyote zaidi ya ile 5000 aliyonipa...........
Huyo manzi alikupiga hela, shukuru alikuachia ya nauli
 
Mimi nakumbuka nikiwa form four au three nilikuwa nasoma boarding sasa siku naondoka nyumbani hali ilikuwa ngumu sana nikapewa sh. 2000 wakati huo nauli ya kutoka hapo nyumbani hadi mji ninaosoma (sio mpaka shule) nauli ni hiyohiyo 2000. Nilimuomba konda nikasafiri kwa 1500, nilipofika mjini pale nikanunua vipande viwili vya sabuni nikaanza kuchanja mbuga kwenda shuleni na begi langu kichwani. Daladala ilikuwa 100 kipindi hicho kwa wanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha usinikumbushe kuna siku ilipigwa game ya SIMBA NA YANGA... basi natoka taifa ile sina hata buku nkaanza upiga wa mguu hadi mbagala...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee sitosahau siku nilikua na dada mmoja mzuri nampenda lakini alikua hanipendi yaani ukiomba mechi mpaka upewe mwezi. Basi siku moja nikasema nataka nije Kwa Azizi Ali tuongee akasema usije, nikaenda bana nikafika nikamtext sijui alisema nini nilikua kama nina 12000 kwenye tigo pesa nikamtumia nikasema basi tumia hiyo kutatua shida yako, kumbuka hapo hakuja sababu alisema nisije nikajitia kiherehere so mimi nikapiga mguu from Azizi Ali mpaka Magomeni Morocco Hotel. Aiseee sitosahau. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mwaka 2008
 
Ndo hivyo, mnazi mmoja chocho kwa chocho Hadi buguruni, unazuga zuga kidogo, unaingia chocho Kama unaenda vingunguti reli kwa reli Hadi spenco (maji machafu) hadi tabata bima unaingia chocho Hadi magorofa ya ladwa unashusha bonde ukipandisha upo tabata mawenzi, unateleza tu, chocho ndogo hadi kimanga destination.
 
We umetembea hapo tu unaanzisha thread wakati mi nishatembea toka Dar hadi Bagamoyo hadi nikaanza kuhisi harufu ya mishkaki inanukia kumbe ma.pumbu yangu mwenyewe[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

"ᴬ ᵍᵒᵒᵈ ᵖˡᵃⁿ ᵛⁱᵒˡᵉⁿᵗˡʸ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵒʷ ⁱˢ ᵇᵉᵗᵗᵉʳ ᵗʰᵃⁿ ᵃ ᵖᵉʳᶠᵉᶜᵗ ᵖˡᵃⁿ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵉˣᵗ ʷᵉᵉᵏ"
Hujatulia mkuu
 
kuna siku nipo na mshikahi wangu sana, tumetoka chuo posta tunaenda malapa, sasa mimi nauli ninayo yeye hana so ikabidi wote tutembe ilikua sa 8 iv mchana af miezi kama hii jua/joto balaa sitakuja kusau siku iyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole mkuu ila natumaini baada ya dhiki hii imekuja faraja
Ndo hivyo, mnazi mmoja chocho kwa chocho Hadi buguruni, unazuga zuga kidogo, unaingia chocho Kama unaenda vingunguti reli kwa reli Hadi spenco (maji machafu) hadi tabata bima unaingia chocho Hadi magorofa ya ladwa unashusha bonde ukipandisha upo tabata mawenzi, unateleza tu, chocho ndogo hadi kimanga destination.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu Mimi rekodi zangu nimevunja hapa hapa dar inatokea nishakula nauli kwa hiyo option ya mwisho ikawa Ni kuprint by ngoko.nishatoka kariakoo mpaka segerea kwa mguu,pia route ya ubungo mpaka buguruni Mara kibao tu.ni nyakati tu zinatokea katika maisha.hapa yenyewe Sina hela mfukoni wakuu naona Bora hata nisimwombe mtu nitembee tu Niko mubashara barabarani napiga Hamza kanuni mdogo mdogo kutoka posta mpaka buguruni.tutadata tutanyoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeshapiga sana route za:

1. Mikocheni - Tandika - Kurasini - Buguruni.

2. Posta - Gongolamboto.

3. Kigamboni Daraja jipya - Karume.

Yaani sometimes mpaka miguu ilikuwa inavimba.

Note.

Binafsi nimezaliwa kijijini na kutembea umbali mrefu vijiji kwa vijiji ni kawaida ILA tatizo hapa DAR ni KUPOTEA njia, then uulizie URUDI utembee tena. INACHOSHA sana
 
Hadi sasa usafiri wangu ni miguu ujingaujinga sitaki labda kama naenda mbali
Fullstop
 
Back
Top Bottom