Tuliowahi kutembea kwa sababu ya kukosa nauli tukutane hapa

Ilikuwa mara mojatu.
Wakati wakwenda, nili panda DCM kariakoo sokoni nikafanikiwa kumkwepa konda sikulipa nauli.
Hapo naelekea mikocheni maeneo ya ITV kusaka ajira, nikakaa hadi sa6 mchana bila mafanikio njaa iliniumasana nikaamua 150 yangu niile mihogo na kachimbari.

Kurudi nilitembea kutoka mikocheni ITV mbaka uhasibu cota za bandari.

Daaah, thanks GOD for what you did in my life.
Umefanya njia pasipo kuwa na njia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tushatembea toka Manyara mjini hadi Dodoma mjini (kwa hapa bongo tu)na hatusemi neno,
achilia mbali zile route tulizopiga katika harakati za kuvuka border kwenda SA.....wewe hapa na ubungo tu unaona umetembeea!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo manzi alikupiga hela, shukuru alikuachia ya nauli
 
Mimi nakumbuka nikiwa form four au three nilikuwa nasoma boarding sasa siku naondoka nyumbani hali ilikuwa ngumu sana nikapewa sh. 2000 wakati huo nauli ya kutoka hapo nyumbani hadi mji ninaosoma (sio mpaka shule) nauli ni hiyohiyo 2000. Nilimuomba konda nikasafiri kwa 1500, nilipofika mjini pale nikanunua vipande viwili vya sabuni nikaanza kuchanja mbuga kwenda shuleni na begi langu kichwani. Daladala ilikuwa 100 kipindi hicho kwa wanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha usinikumbushe kuna siku ilipigwa game ya SIMBA NA YANGA... basi natoka taifa ile sina hata buku nkaanza upiga wa mguu hadi mbagala...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee sitosahau siku nilikua na dada mmoja mzuri nampenda lakini alikua hanipendi yaani ukiomba mechi mpaka upewe mwezi. Basi siku moja nikasema nataka nije Kwa Azizi Ali tuongee akasema usije, nikaenda bana nikafika nikamtext sijui alisema nini nilikua kama nina 12000 kwenye tigo pesa nikamtumia nikasema basi tumia hiyo kutatua shida yako, kumbuka hapo hakuja sababu alisema nisije nikajitia kiherehere so mimi nikapiga mguu from Azizi Ali mpaka Magomeni Morocco Hotel. Aiseee sitosahau. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mwaka 2008
 
Ndo hivyo, mnazi mmoja chocho kwa chocho Hadi buguruni, unazuga zuga kidogo, unaingia chocho Kama unaenda vingunguti reli kwa reli Hadi spenco (maji machafu) hadi tabata bima unaingia chocho Hadi magorofa ya ladwa unashusha bonde ukipandisha upo tabata mawenzi, unateleza tu, chocho ndogo hadi kimanga destination.
 
Hujatulia mkuu
 
kuna siku nipo na mshikahi wangu sana, tumetoka chuo posta tunaenda malapa, sasa mimi nauli ninayo yeye hana so ikabidi wote tutembe ilikua sa 8 iv mchana af miezi kama hii jua/joto balaa sitakuja kusau siku iyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole mkuu ila natumaini baada ya dhiki hii imekuja faraja
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshapiga sana route za:

1. Mikocheni - Tandika - Kurasini - Buguruni.

2. Posta - Gongolamboto.

3. Kigamboni Daraja jipya - Karume.

Yaani sometimes mpaka miguu ilikuwa inavimba.

Note.

Binafsi nimezaliwa kijijini na kutembea umbali mrefu vijiji kwa vijiji ni kawaida ILA tatizo hapa DAR ni KUPOTEA njia, then uulizie URUDI utembee tena. INACHOSHA sana
 
Hadi sasa usafiri wangu ni miguu ujingaujinga sitaki labda kama naenda mbali
Fullstop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…