Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Mikopo,mhhhh.
Nilikopa Saccos moja nikanunua shamba,nikijua mshahara utanisaidia kurejesha chap,duuuu.
Mshahara ukaanza kusuasua,marejesho yakaanza kusumbua.
Mhh,muda wa kulipa ukaisha,daaaaa.saccos wakaanza kunifatilia,acheni wazeee!!
Mungu akanisaidia nikafanya juu chini nikamaliza Deni ,yaani furaha niliyoipata kwa kumaliza deni Ni kubwa Sana.
 
Na sisi tunaodhamini wakopaji tukutane wapi??????
Hili nalo balaa linginee.
Nilimdhamini mfanyakazi mwenzangu kuchukua mkopo kidogo tuu,Mara jamaa akashindwa kurejesha kwa mwezi km ilivyotakiwa

Gafla nikaambiwa inabidi nianze kumlipia ,yaani nikalipa marejesho mwezi mmoja,ikabidi nifanye maarifa boss amkate juu kwa juu Deni likalipwa Ila Mimi nikiwa mhanga,acha tuuu.
Sitakuwa mwepesi kumdhamini mtu tena
 
Hahaahah
Mimi nilikua afisa wa mikopo kwenye microfinance moja ivi nikaacha nikaingia mtaani kwenye biashara nilichofanyiwa na mikopo sina hamu, alikuja afisa mikopo juzi kunishauri nikakope kwao nimeishia kumtolea panga
Kausha damu
Usiombe uchukue mkopo wa KAUSHA DAMU...wanakupa leo kesho unaanza marejesho mfululizo mpaka utapomaliza kina mama wamekauka huko mitaani sio poa
 
Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi,hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
Huo ujinga sifanyi
 
kama sio letshgo sijui
walifanya upuuzi huu kwa mke wangu nikawapandia hewani siku hiyo wakatuma statement ya bank ya marejesho ikaonekana deni limeisha walikuwa wanafanya uhuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…