Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Wanasema mkopo sio zawadi, nimejitoa kwenye mfumo wa kukopa kabisa, nakumbuka nilikuwa na project ndogo ya serikali, nikakopa nikijua payment ingefanya ndani ya wakati ningelipa.. Ohoooo.. ilipigwa delay ya maana sana, nikajikuta nauza gari mbili kwa mpigo na sikuwa nimekaa nazo hata zaidi ya miezi mitatu.. Kuanzia hapo naogopa mikopo kama ukoma na ninashukuru nimetoka kwenye mikopo yenyewe labda mbeleni huko
Miradi ya serikali noma sana. Watu ambao walifanya kazi enzi za JK halafu malipo yao yakakutana na uongozi wa JPM walilizwa mno. Kuna jamaa yangu Kigoma alikuwa kashapiga hatua aliishia kufilisika mazima. Ukiwa unafanya project.ya serikali inahitaji umakini.
 
Miradi ya serikali noma sana. Watu ambao walifanya kazi enzi za JK halafu malipo yao yakakutana na uongozi wa JPM walilizwa mno. Kuna jamaa yangu Kigoma alikuwa kashapiga hatua aliishia kufilisika mazima. Ukiwa unafanya project.ya serikali inahitaji umakini.
Project za Serikali ni pasua kichwa sana, shift ya kutoka kwa JK to JPM imefanya makandarasi wengi kuwa maskini. Kukopea hela mradi wa Serikali pasua kichwa, labda uingie ubia na bank katika mradi husika inaweza pona pona yako.
 
Miradi ya serikali noma sana. Watu ambao walifanya kazi enzi za JK halafu malipo yao yakakutana na uongozi wa JPM walilizwa mno. Kuna jamaa yangu Kigoma alikuwa kashapiga hatua aliishia kufilisika mazima. Ukiwa unafanya project.ya serikali inahitaji umakini.
Yeah hata Mimi sikulipwa..... Nilianza na JK, JPM hakulipa
 
Na mimi nataka kukopa lakini sina biashara bali nina nyumba yenye HATI safi Dodoma, sasa kama kuna Mfanyabiashara anayekopesheka anahitaji kukopa Bank lakini hana dhamana mimi ninayo aje inbox tuyajenge, Nyumba ipo Dodoma Mjini, thamani ya Nyumba ni zaidi ya Milioni 50 na ni Nyumba mpya, karibuni.
 
Aisee hii mikopo iko nzuri na mibaya, nilishawai kuchukuwa M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani. Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya. Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
Je tukichukua kuendeleza biashara na si kuanzisha kama uliyosema hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom