Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

On the otherside of the story: Kwa wakopeshaji, Kuna shost anaishi huko uswahilini kazi yake kukopesha wamama. Sasa kuna muda anaumwa sana ukimuuliza anasema wakopaji wanamloga asahau madeni [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Akaanza kwenda kwa mganga na yeye kujiweka fit, Mwisho ameolewa na mganga siku hizi na biashara yake ya kukopesha anaendelea nayo.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Bhana eee nilikopa 15m, nikanunua Bati na kulipa fundi hela ikaisha, nikasota miaka 4 kurudisha, nikivyomjinga si nikakopa tana baada ya miaka 4 kuisha huku nikihaidiwa kusaidia kulipa mkopo, mbona na henya mwenyewe!

Cha ajabu Sasa nikakopa tena 3m kutoka kwa ndugu yangu niliyemwambia ntarejesha mwaka ujao kabla ya March ha ha ha ha ..Sina hela na nyumba haijaisha!

nyie haya maisha daah nakonda peke yangu
Usijengee hela ya mkopo
 
Na mimi nataka kukopa lakini sina biashara bali nina nyumba yenye HATI safi Dodoma,sasa kama kuna Mfanyabiashara anayekopesheka anahitaji kukopa Bank lakini hana dhamana mimi ninayo aje inbox tuyajenge,Nyumba ipo Dodoma Mjini,thamani ya Nyumba ni zaidi ya Milioni 50 na ni Nyumba mpya,karibuni
Una hamu ya kulia?maana huo mkopo utalipa wewe na hutakuwa na uwezo wa kulipa, nyumba itauzwa hiyo
 
Hili nalo balaa linginee.
Nilimdhamini mfanyakazi mwenzangu kuchukua mkopo kidogo tuu,Mara jamaa akashindwa kurejesha kwa mwezi km ilivyotakiwa

Gafla nikaambiwa inabidi nianze kumlipia ,yaani nikalipa marejesho mwezi mmoja,ikabidi nifanye maarifa boss amkate juu kwa juu Deni likalipwa Ila Mimi nikiwa mhanga,acha tuuu.
Sitakuwa mwepesi kumdhamini mtu tena
Ulifanya jambo la kijinga

Usimwekee mtu dhamana.
 
Mkuu mimi Mzazi wangu kakopa pesa Banki lakini kwa marejesho ya banki kukata kwenye pensheni yake sasa pensheni yake Azina hawaja muingizia benki miezi 4 imefika sasa Afisa mikopo wa Banki ana tusumbua sisi watoto tumpeleke mzee wetu Azina akahakikiwe, Mimi nimekataa simpeleke kwasababu pesa alivyokopa haja tugaiya kaitumia peke yake, sasa hatujui afisa mikopo wa benki atazipataje pesa zaidi ya Milioni 10

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Nyumba itauzwa
 
On the otherside of the story: Kwa wakopeshaji, Kuna shost anaishi huko uswahilini kazi yake kukopesha wamama. Sasa kuna muda anaumwa sana ukimuuliza anasema wakopaji wanamloga asahau madeni 😅😅😅😅😅

Akaanza kwenda kwa mganga na yeye kujiweka fit, Mwisho am seeeolewa na mganga siku hizi na biashara yake ya kukopesha anaendelea nayo.
Eeh kwa hiyo mganga kamloga ili amoende na kafanikiwa🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nilikopa mkopo wa manispaa nikafanya matumizi nje ya malengo na nyingine nikanywea bia. Nikawa nategemea kulipa kwa mshahara, mara tukasimamishwa kwa ajili ya corona. Nikaanza kubeti mara ligi zikasimamishwa.
Ingawa ni hela ndogo lakini ilisimamisha kichwa.
Ndio wewe nn ulisimamishwa na majaliwa juz 😃
 
Back
Top Bottom