Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Enzi hizo naanza maisha nilikopa Kikoba Cha bimkubwa kama kilo 3 nilipanga nilipige sopu sopu geto langu.

Ebhana we Ile Hela nilit.o.mbea na mitikasi mingine isiyo na akili nilipanga na kibunda.

Niliteseka miezi 3 napaswa nilipe ulie mkopo hatimae niliumaliza

Ulinufundisha sana ule mkopo.

Leo nakopa kwa akili na mipango

Kopa wekeza mradi wenye tija.

Robaert Toru Kiyosaki anasema use other people's money to create your own wealth

Katu situmie my hard earned money kuwekeza natumia Hela za watu[emoji1]
Kuna mzee aliniambia niwe nakopa kipindi nikiwa sina shida ya hela. Zangu nizihifadhi
 
Nafkri na Mimi nifanye hivyo. For real nateseka sana. Yaani kesho niende kuongea nao mkopo usimame wenyewe bila riba. Waki goma hata mahakamn wanifunge tu[emoji24].
Lipa 500k yao halafu waite mkubaliane kuhusu hizo faini na riba. Kwa sababu ulishalipa riba kadhaa basi wafute, wapunguze au wasiendelee kuongeza na wakupe muda wa kuzilipa. Ongea nao kikakamavu baada ya kulipa 500k yao kwanza.
 
Acha kabisa mkuu,
Mimi nishapunguzahata Kasi ya kuagiza mzigo,

Usipoenda kwa timing
Unajikuta una mzigo mkubwa dukan na wateja hamna na hapo hapo unadaiwa rejesho.

Mwisho wa siku unajikuta unajumlisha mzigo kwa Bei ya hasara ili upate rejesho
Kweli mzee. Utakuta una mzigo wa 20m ndani lakini laki 5 tu chash inaleta wenge.
 
On the otherside of the story: Kwa wakopeshaji, Kuna shost anaishi huko uswahilini kazi yake kukopesha wamama. Sasa kuna muda anaumwa sana ukimuuliza anasema wakopaji wanamloga asahau madeni [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Akaanza kwenda kwa mganga na yeye kujiweka fit, Mwisho ameolewa na mganga siku hizi na biashara yake ya kukopesha anaendelea nayo.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Lipa 500k yao halafu waite mkubaliane kuhusu hizo faini na riba. Kwa sababu ulishalipa riba kadhaa basi wafute, wapunguze au wasiendelee kuongeza na wakupe muda wa kuzilipa. Ongea nao kikakamavu baada ya kulipa 500k yao kwanza.
Ahsante ndugu. Hapa umenipa pa kuanzia [emoji120]
 
Hatari sana maisha ni majaribu tumepitia mengi jamani tupeni pole
 
Mwaka huu pale kongowe amezikwa mfanya biashara wa siku nyingi sana kisa madeni ya benk. Nkitulia ntaleta huu mkasa
Haya sasa nawapa kisa
Huyu mzee wa makamo (around 49 au 50 hivi) alikuwa moja ya wenye maduka makubwa sana ya vitu vya ndani jumla na reja reja. Aliwekeza kwenye majengo akawa na nyumba za wapangaji na yake ya kuishi. Kifupi milioni 20 hadi 40 hivi za mzunguko wa biashara tu zilikuwa hakosi bado mishe zingine za kumuingizia hela.
Huku na huku sijui alipata pepo gani lilomtuma aende benk kukopa tumilion kadhaa dhamana zikiwa mali zake iliwemo duka, na nyuma zake zote (hazipungui 3 au 4 hivi).
Baada ya mkopo mambo yakaenda ndivyo sivyo watu wa benk wanataka Chao.
Akawa anakopa watu ili akimbizane na kasi ya bank....
Harakati zote hizi zikagonga mwamba mali zake zikapigwa mnada.
Kukwepa aibu akakimbilia shinyanga akaanza biashara ya kuuza mchele wa reja reja kwa kupewa kamtaji kadogo na mama yake mzazi baada ya kuuza shamba lake huko killage (kijijini).
Muda wote akawa mtu wa mawazo hadi akili zikachanganya akafariki..lakini hadi anafariki anaongelea mali zake na utajiri wake ulioteketea...

Kwa hiyo wandugu mikopo ni mizuri lakini ikikugeuka utaomba poo
 
Inaumiza Sana[emoji22]
 
Back
Top Bottom