Tuliowahi kuvamiwa, kuibiwa au kutekwa na majambazi tujikumbushe

Tuliowahi kuvamiwa, kuibiwa au kutekwa na majambazi tujikumbushe

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
2,035
Reaction score
2,715
Nakumbuka ilikuwa 2013, bana wee sitaka nisahau maishani mwangu.

Nakumbuka nilipiga kazi kwenye biashara yangu, nikajikusanyia pesa nzuri tu sio chini ya million 2, ghetto nilipapendezesha vizuri sana.

Chumba changu kilikuwa pembezoni na mto Arusha eneo nililopewa na wazazi wangu pamezungukwa na miti na migomba mingi sana, kuna msitu mmoja mzuri sana kama ulaya vile.

Sasa kipindi hicho nilikuwa nimenunua bonge la speaker, daily nilikuwa nakula reggae na nyimbo za hiphop za chuga, nilikuwa na computer ya dell desktop, kipindi hicho ukiwa na computer mtaa mzima unakuheshimu.

Ilikuwa majira ya saa 9 usiku, nikiwa nimelala gheto, ghafla nikasikia mlango umepigwa jiwe fatuma kwa watu wanaojua jiwe fatuma ni nini watakuambia, walikuwa kama 7 hivi wameshika marungu na mapanga wengine wananimulika na torch machoni yani kama movie vile..

Jamaa wakaniambia toa ulichonacho, nikawaambia sina chochote zaidi ya hivi vitu vya gheto, hakuna!! toa pesa ulizonazo mara mabapa ya mgongo kwa sana, nikawaambia sina pesa, kuna jamaa akawaambia huyu mpaka akatwe ndo atoe pesa, daah jamaa akanikata na panga mgongoni, nikaona niwape hela zao waondoke.

Jamaa wakanipa kichapo cha maana, wakabeba computer, nguo, viatu vyote, speaker na pesa zote nilizosave wakaondoka zao.

Nilichojifunza, simuonei mwizi huruma nikishajua ameiba kweli, yani atakula vitofali mpaka ajute kwanini kaiba..

Hayo ni yangu yalionikuta enzi hizo je nyie kiliwakuta kipi, nakaribisha mchango wenu kwenye huu uzi.

ONE TIME,
ONE FOR THE ROAD..
APPROXIMATELY ONCE AGAIN..
,
 
Back
Top Bottom