Tulipofikia ni kama aibu. Tunaweza kununua V8 ila inakuwaje mpaka mnapewa vifaa vya tehema tena laptop?

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,749
Reaction score
37,420
Hii nchi sijui tunaelekea wapi.Vifaa vya tehama mpaka mnasaidiwa au maigizo.

1784448433750.png

----------------

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea vifaa vya kisasa vya Chumba cha Kanzi Data, vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na miundombinu iliyoboreshwa ya mtandao kutoka Mamlaka ya Taifa ya Nyaraka na Kumbukumbu ya Sultanate ya Oman.

Mchango huu kuwa unalenga kuimarisha usimamizi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali katika mfumo wa kidijitali, kuongeza usalama wa taarifa za Serikali, kuboresha upatikanaji wa nyaraka kwa wakati, kuimarisha uhifadhi wa muda mrefu wa kumbukumbu muhimu za taifa na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za umma na kwa upande mwengine ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano wa kihistoria na ushirikiano imara uliopo kati ya Tanzania na Oman.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali za Tanzania na Oman, akiwemo Balozi wa Sultanate ya Oman nchini Tanzania Mhe. Said Hilal Al-Shidhani, Balozi Abdallah Kilima kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka.

Chanzo: Azam Tv
 
Mm pamoja na ukapuku wangu, Siwezi tumia simu, laptop au kifaa chochote cha Tehama cha kupewa.

Carne hii, ya modern warfare (Cyber warfare ). Unawezaje kupewa Vifaa vya electronic na Mifumo kutoka nchi nyingine ukakubali?

Bora waka wape wanafunzi huko tana wa secondary au Msingi, Havifai kukaa hata ofisi ya Mwalimu mkuu.
 
Mm pamoja na ukapuku wangu, Siwezi tumia simu, laptop au kifaa chochote cha Tehama.

Carne hii, ya modern warfare (Cyber warfare ). Unawezaje kupewa Vifaa vya electronic na Mifumo kutoka nchi nyingine ukakubali?

Bora waka wape wanafunzi huko tana wa secondary au Msingi, Havifai kukaa hata ofisi ya Mwalimu mkuu.
Imagine in short hata Kwa hao wanafunzi pia havifai kama wame vitrack ni changamoto nzito Tena sana
 
Kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam,Mbeya,Arusha,Mwanza kulipaswa kuwepo na ongezeko kubwa sana la Vyuo vya kati na vyuo vya ujuzi lakini ongezeko ni la machinga wa mitumba,bidhaa hafifu za chini,wachoma mahindi,wauza machunga badala ya vijana hao kuwepo kwenye site,viwanda,mikoani wakitumia ujuzi.Jibu ni kuwa hatuna viongozi wanaioitazama kesho ya miji na Tanzania na wanchotazama ni namna ya kupata cheo au kupiga mipenyo ya fedha.
 
Nchi imeweka kodi kwenye vitu vya kusomea baadae mnakuja kupewa laptop na kujitangaza ni aibu kama Nchi kupewa hivyo vifaa aisee toeni kodi huko ni madaftari tu hayo mnatia aibu kama Nchi aisee..
 
Hii nchi sijui tunaelekea wapi.Vifaa vya tehama mpaka mnasaidiwa au maigizo.

View attachment 3632459​

----------------

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea vifaa vya kisasa vya Chumba cha Kanzi Data, vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na miundombinu iliyoboreshwa ya mtandao kutoka Mamlaka ya Taifa ya Nyaraka na Kumbukumbu ya Sultanate ya Oman.

Mchango huu kuwa unalenga kuimarisha usimamizi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali katika mfumo wa kidijitali, kuongeza usalama wa taarifa za Serikali, kuboresha upatikanaji wa nyaraka kwa wakati, kuimarisha uhifadhi wa muda mrefu wa kumbukumbu muhimu za taifa na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za umma na kwa upande mwengine ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano wa kihistoria na ushirikiano imara uliopo kati ya Tanzania na Oman.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali za Tanzania na Oman, akiwemo Balozi wa Sultanate ya Oman nchini Tanzania Mhe. Said Hilal Al-Shidhani, Balozi Abdallah Kilima kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka.

Chanzo: Azam Tv
Nchi inaongozwa na CHAMA CHA watu wenye matatizo
 
Sa100 kaiharibu sana Tanganyika yetu.Zamani tulikuwa middle income hadi tukawa tunatoa misaada kwa nchi kama malawi n.k.Leo hii sa100 katurudisha kwenye umasikini wa kutupwa hadi tunapewa misaada ya laptop za laki tatu hadi laki mbili kweli?Hiiiiii bhaghoshaaa
 
ishu sio wakat wa nan , ccmu wote vilaza , wameshindwa kuendesha nchi
Hawajashindwa Bali hawataki cause wanahisi ili waendelee kutawala wanapaswa kuzalisha masikini wengi ili wasiweze kupata challenge

So ni mission maalum kabisa
 
Hivyo vifaa wawape watu wachezee magemu na kuingiza nyimbo...Hizi aibu ndogo ndogo ni za kujitakia kabisa.
 
Back
Top Bottom