Tulishawaonyeni sana hapa JamiiForums kuwa hawa 'QNET' ni 'Matapeli' hamkusikia sasa ngojeni 'Wawanyoosheni' ili mkome

Tulishawaonyeni sana hapa JamiiForums kuwa hawa 'QNET' ni 'Matapeli' hamkusikia sasa ngojeni 'Wawanyoosheni' ili mkome

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
WAATHIRIKA WA AJIRA ZA QNET WAANZA KUREJESHWA MAKWAO: Waathirika wa utapeli unaofanywa kupitia Kampuni ya Biashara ya Mtandao Q Net katika eneo la Mbezi Dar es Salaam wameanza kurejeshwa makwao kupitia operesheni maalumu inayofanywa na ofisi za wenyeviti a serikali za mitaa ikihusisha kuondolewa katika nyumba wanamoishi zoezi linalosimamiwa na Polisi Kata.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi Louis amesema vijana hao wengi wao wakitoka nje ya mkoa wa Dar es salaam watafikishwa katika kituo kikuu cha Mabasi Magufuli ili kusubiria utaratibu wa kupata nauli za kurejea makwao na wale watakaokaidi watafikishwa mahakamani.

Chanzo: Azam TV

Wewe umeona wapi Kauli Mbiu ya Kampuni ni Salamu ya ''Good Morning' 'na hata mkikutana Mchana Saa 7 au Usiku Saa 1 bado mnatakiwa Kusalimiana hivyo hivyo 'Good Morning' tu?

Kama katika Salamu tu Wameshatudanganya (Kututapeli) katika Salamu hivi huko Kwingineko katika Masuala mazima ya Fedha na Mafanikio watakuwa Wakweli? Eti 'Good Morning' hovyo kabisa.

Na kinachoniuma zaidi ni kwamba Kampuni hii ya Kitapeli ya QNET imedekezwa mno na Serikali na imeumiza pia Watanzania wengi mpaka hata kuharibu Ndoa za Watu.
 
IMG_20220624_060519.jpg
IMG_20220624_060500.jpg

Kwani Kigwangala anasemaje ?
 
Kuna rafiki wa miaka mingi alikuwa huko. Akanishawishi sana kujiunga nikawa namkwepa. Siku nikaamua kwenda kuonana nao ofisin kwao.
Nikagundua n utapeli mtu, pesa kupata mpaka umshawishi nawe mtu wa kujiunga. Kiingilio n 5M.

Nikamwambia jamaa huo n utapeli. Sitaki kuingia huko. Kaninunia mpaka leo
 
Biashara ya Neteork Marketing ha work kwa nchi masikini lazima ionekane ni utapeli, Qnet kama Qnet wapo sana shida Model yao kwa nchi masikini haofanyo kazi, ni the same na Folever living, GNLD na wengineo, Mfano ilianza GNLD wakashindwa wakaondoka lakini kampuni bado ipo na wana product kibao zinauzwa hata Tanzania na tunazitumia sana kama ile mbolea yao
 
Folever living ndio nn? Sasa mpaka leo matumizi ya R na L hujui ndio ushindwe kupigwa!!! Fanya kazi
 
Biashara ya Neteork Marketing ha work kwa nchi masikini lazima ionekane ni utapeli, Qnet kama Qnet wapo sana shida Model yao kwa nchi masikini haofanyo kazi, ni the same na Folever living, GNLD na wengineo, Mfano ilianza GNLD wakashindwa wakaondoka lakini kampuni bado ipo na wana product kibao zinauzwa hata Tanzania na tunazitumia sana kama ile mbolea yao
Rudi nyumbani ukalime.
 
Niliiona hyo Habari azam TV, ilinifikirisha sana, maana ilikuwa haija "balance"..

Kiongozi wa mtaa amewashutumu wazi wazi kuwa Q net ni matapeli, na Hao sio vijana WA kwanza kufanyiwa utapeli huo, ni operation ya Tatu ya kuwarudisha makwao vijana waliotapeliwa na mtandao huo wa Qnet...

Kinachonishangaza ofisi zao (Qnet) zinajulikana zilipo, kwa nn Hao viongozi pamoja na polisi hawakwenda kupeleka malalamiko juu ya wale vijana?

Azam walirusha hiyo taarifa kwa nn hawakwenda ofisi za Qnet kuwahoji kama wao wanahusika na huo utapeli?

Kama ni taasisi ya kitapeli kwa nn bado ipo nchini?

Je, Kigwangala Ana maoni gani juu ya hili maana alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa hyo taasisi.
 
Kuna nyngine wanijiita idea debator watu wamepgwa saNa sku mbili hiz[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16]
[emoji16][emoji16][emoji16] idea debator, bhana sijui nisemaje ila jamaa wamekomba ma boom ya wanafunzi mbaya mbovu aisee..

Mimi mwenyew wamenila kichwa japo niliweka Tsh 10000=/ kam mtaji..

Sent from my BAC-L21 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu
Roho wa Mungu alikuepusha na hawa matapeli?
Almanusura 😀😀😀 sema waliponipiga ule msasa wa Kwanza , wakanambia nije kesho yake kufinalize daaah njiani niliona watu wote hawajui kutafta hela mi ndo nimelifuma chaka 😊😊😀😀... !! Baada ya kuingia jamii forum nikakuta huu uozo nilipiga bonge moja la U-turn si ya nchi hii
 
Biashara ya Neteork Marketing ha work kwa nchi masikini lazima ionekane ni utapeli, Qnet kama Qnet wapo sana shida Model yao kwa nchi masikini haofanyo kazi, ni the same na Folever living, GNLD na wengineo, Mfano ilianza GNLD wakashindwa wakaondoka lakini kampuni bado ipo na wana product kibao zinauzwa hata Tanzania na tunazitumia sana kama ile mbolea yao
Mkuu mbona unaandika kama wewe ni mkurugenzi mwenyewe kabisa wa Q.net?
Andika vizuri basi usikimbie kama unafukuzwa na jini!
Unakimbilia wapi sasa?
 
Back
Top Bottom