Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?

Sri Lanka walipowapa Wachina banadari ya Hambantota walitajiana kiasi kabisa cha uwekezaji wa dola bilioni 1.
Nasubiri uweke hiyo IGA ya Italy. Mbona umehamisha magoli tena?
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo

8.) Kwa nini zabuni ya uwezekezaji haikutangazwa? Kwa nini Mbarawa alidanganya kuwa Zabuni ilitangazwa?

9.) KWA nini walikaa na mkataba kwa miezi tisa kisha wakaupeleka bungeni kwa hati ya dharula?

10.) Kwa nini Zanzibar wameingia ubia na kampuni ya Global Logistics (AGL) kuendesha bandari zao na sio DPW na tena kwa miaka mitano tu?
 
Anzisha uzi wako uongelee hayo. Hapa limeulizwa swali linahitaji majibu. Ulichoweka hapa ni longolongo tu
 
China-Pakistan Economic Corridor (CPEC) walikubaliana ni uwekezaji wa zaidi ya dollar bilioni 46, thamani za mradi mmoja mmoja na pesa za miradi zitatoka katika vyanzo vipi.
 
China-Pakistan Economic Corridor (CPEC) walikubaliana ni uwekezaji wa zaidi ya dollar bilioni 46, thamani za mradi mmoja mmoja na pesa za miradi zitatoka katika vyanzo vipi.
Bwashee acha longolongo. Weka ushahidi kujibu swali kama lilivyoulizwa
 
Bwashee acha longolongo. Weka ushahidi kujibu swali kama lilivyoulizwa
Watu hawana muda wa kupoteza kukutafutia hivi vitu vidogo vidogo ambavyo vimezagaa kila kona mtandaoni.
 
Watu hawana muda wa kupoteza kukutafutia hivi vitu vidogo vidogo ambavyo vimezagaa kila kona mtandaoni.
Kwa nini nisiseme kuwa umeingia kwenye huu uzi kupiga longolongo sasa?
 
🤣🤣🤣🤣 Naona upo hoi umechoka sana kwa kumtetea mama Samia. Kama kweli unampenda mshauri achutame mambo yameshaharibika
Kwa hiyo umekuwa msemaji wangu?

Mama Samia yupo vizuri na hadi sasa sioni shida yeyote kwake.

Kwenye suala la Bandari namwambia asonge mbele maana tumechelewa sana. asisikilize kelele za wajinga na wapotoshaji kama wewe na wenzako
 
Haya. Namtakia safari njema
 
Porojo ndeeeefu za kijinga, umeshindwa kujibu swali jepesi tu.

Ndiyo tuseme una macho lakini hayaoni au ndivyo mlivyozowea kuishi namna hiyo, mpaka mnafikia kujidanganya wenyewe? "Swali ni very simple", Tazama hata heading tu ya huu uzi, ndili swali lenyewe.

Naliruduai hapa, hapa hili bandiko lako refu wapi limejibu?

Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?​

Huna tofauti na wale mawakili wabovu na kina mruma waliokwenda kutuabisha ICSID.

cc: Anna Tibaijuka
 
1. Mtu anayesema anaielewa na kuikubali IGA ya DPW hawezi kuniambia kuwa na akili timamu nikakubali.

2. FaizaFoxy anasema kuwa anaielewa na kuikubali IGA ya DPW

3. Hivyo, FaizaFoxy hawezi kuniambia kuwa ana akili timamu nikakubali.
 
China-Pakistan Economic Corridor (CPEC) walikubaliana ni ushirikiano wa uwekezaji wa zaidi ya dollar bilioni 46, pia thamani za mradi mmoja mmoja midogo midogo na pesa za miradi zitatoka katika vyanzo vipi walionyesha.
 
1. Mtu anayesema anaielewa na kuikubali IGA ya DPW hawezi kuniambia kuwa na akili timamu nikakubali.

2. FaizaFoxy anasema kuwa anaielewa na kuikubali IGA ya DPW

3. Hivyo, FaizaFoxy hawezi kuniambia kuwa ana akili timamu nikakubali.
Wewe achana na ujinga wa "character assassination", jibu swali:

Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?​

Character ya Anna Tibaijuka ilishakufa alipoiba na kina Ruge wakishirikiana na benki ya kanisa. Yangu huwezi kuiuwa ipo JF peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…