Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Wanawake na mabinti wengi walipitia ama wanapitia maumivu ya tumbo la mwezi Dysmenorrhoea kila mwezi. Maumivu haya yana athiri uwezo wa mwili kisaikolojia, fizikia hata kujichanganya na wenzako inakuwa shida. Wengi hasa hupata maumivu haya siku moja au mbili ambazo wengine hutapika na tumbo kuuma pamoja na miguu kushindwa kutembea.
Wengi hutumia panadol na dawa nyingine za kutuliza maumivu ili kutuliza makali ya tumbo hil, wengine hushinda na chupa za maji ya moto na wengine wanahitaji matubabu zaidi ya kitaalamu hata kufanyiwa upasuaji. Hii ni asili ya binadamu huwezi kuidharau na hii ni mfumo wa jamii kuzalisha na kuongezeka duniani.
. Katika dunia ya mfumo dume hili tatizo halijawahi yakinishwa. Binti hupoteza siku mbili ambazo hawezi kuhudhuria masomo. Bahati iwe nzuri tumbo hili lianze kuuma Jumamosi, unaweza kutumia weekend kujitibu. Likianza Jumatatu ni shida mno.
Tukiwa tunapambana na kumpatia mtoto wa kike taulo za kujikinga. Kwa wale wahanga ni muhimu kufikiriwa muda huu wa siku mbili kwa mwezi wawe exempted kujiuguza.