Tumbo la mwezi kwa vigoli (Dysmenorrhoea) iwe sababu maalum ya kukosa mahudhurio ya darasani siku mbili kwa mwezi

Tumbo la mwezi kwa vigoli (Dysmenorrhoea) iwe sababu maalum ya kukosa mahudhurio ya darasani siku mbili kwa mwezi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wanawake na mabinti wengi walipitia ama wanapitia maumivu ya tumbo la mwezi Dysmenorrhoea kila mwezi. Maumivu haya yana athiri uwezo wa mwili kisaikolojia, fizikia hata kujichanganya na wenzako inakuwa shida. Wengi hasa hupata maumivu haya siku moja au mbili ambazo wengine hutapika na tumbo kuuma pamoja na miguu kushindwa kutembea.

Wengi hutumia panadol na dawa nyingine za kutuliza maumivu ili kutuliza makali ya tumbo hil, wengine hushinda na chupa za maji ya moto na wengine wanahitaji matubabu zaidi ya kitaalamu hata kufanyiwa upasuaji. Hii ni asili ya binadamu huwezi kuidharau na hii ni mfumo wa jamii kuzalisha na kuongezeka duniani.

. Katika dunia ya mfumo dume hili tatizo halijawahi yakinishwa. Binti hupoteza siku mbili ambazo hawezi kuhudhuria masomo. Bahati iwe nzuri tumbo hili lianze kuuma Jumamosi, unaweza kutumia weekend kujitibu. Likianza Jumatatu ni shida mno.

Tukiwa tunapambana na kumpatia mtoto wa kike taulo za kujikinga. Kwa wale wahanga ni muhimu kufikiriwa muda huu wa siku mbili kwa mwezi wawe exempted kujiuguza.
 
Hata kama ni utandawazi hatuendi hivyo. Tumbo la mwezi lisiwe kisingizio cha kukacha masomo na pia bora waseme alikua anaumwa sio mpaka kila mmoja ajue fulani huwa anaingia period muda huu na ule
 
Mtu ambae hajawahi/haumwi hili tumbo ni rahisi kusema hivi na vile...linauma sana jamani huku miguu na kutapika juu, wahanga ni wengi ila kulisema wazi ndo inashindikana..!
 
Miaka yote hakuna kitu kama hicho,kwa nini leo, au bleed zimebadilika?
Nilipokuwa JKT kwa mujibu wa sheria baada ya kumaliza Kidato cha 6, wasichana walikuwa wakitamka kwenye gwaride 'Nina ugonjwa wa Matron' na wanapewa off baada ya matron kwenda faragha na mhusika kuthibitisha kwamba msichana huyo kweli yuko mwezini.
 
Ni wazi zuri ambalo umelitoa ingawa sikubaliani nalo, Tukienda kitaalamu zaid dysmenorrhoea (maumivu ya hedhi) sio wote wanaopata maumivu haya ni asilimia kadhaa ya wasichana wa kike, so kufanya generalization ya maumivu ya hedhi wanayopata asilimia kadhaa ya wasichana, kwamba wapate exemption ya kutohudhuria darasani au kwenye shughuli zingine za kimasomo au zingine zozote sidhani ni sahihi!
Ofcoz nakubaliana kwa namna moja au nyingine kwa baadhi wa wanayopata maumivu hayo kwa kiwango kikubwa (ivuke threshold level) sababu wengi wao wanapata maumivu hayo kwa kiwango kidogo in such a way it doesn't affect them intellectually or even psychologically, sawa kuna namna ambayo inawaathiri physiologically and psychologically, lakini Intellectually unapima kati ya benefits and drawbacks ratio, haileti mantiki ya wao kutohudhuria masomo yao kwa kundi la wachache ifanyiwe generalization kwa kundi la wengi, wakati data zinaongea ndivyo sivyo! So research zaid ifanyike kuona namna gan mambo yalivyo na yafanyiwe evaluation especially kwenye kupima benefits and drawbacks ratio!
Na kwa haraka haraka nnavyofahamu kwa watoto wa kike wanaosumbuliwa na tumbo au ugonjwa wengine wowote huwa wanaomba ruhusa na kupewa ya kujiuguza, sijawahi experience kwa kuona au kusikia, mwanafunzi wa kike anaomba ruhusa na kukatiliwa kisa kwa sababu haipo kwenye miongozo ya kupewa ruhusa pindi apatapo maumivu ya hedhi!

Nawasilisha!
 
Mimi sijaelewa hoja hapa. Hii exemption haipo kwa sasa? Yaani kama msichana anaumwa kwa tatizo ulilotaja au jingine lolote kiasi hawezi hudhuria darasani, je kwa utaratibu wa sasa analazimika kwenda darasani? Suala la muhimu nafikiri ni report ya daktari. Daktari (anayekubalika na shule husika) akiandika mwanafunzi X apumzike (akimpa "bed rest"), ni nani anaweza kuzuia?

Au unakusudia blanket and automatic exemption? Kwamba msichana aamue mwenyewe kama ana tatizo ulilotaja na hivyo asiende darasani kwa siku 2 bila kuhitaji uthibitisho wa kitabibu? Kindly elaborate (Sky Eclat
 
Mimi sijaelewa hoja hapa. Hii exemption haipo kwa sasa? Yaani kama msichana anaumwa kwa tatizo ulilotaja au jingine lolote kiasi hawezi hudhuria darasani, je kwa utaratibu wa sasa analazimika kwenda darasani? Suala la muhimu nafikiri ni report ya daktari. Daktari (anayekubalika na shule husika) akiandika mwanafunzi X apumzike (akimpa "bed rest"), ni nani anaweza kuzuia?

Au unakusudia blanket and automatic exemption? Kwamba msichana aamue mwenyewe kama ana tatizo ulilotaja na hivyo asiende darasani kwa siku 2 bila kuhitaji uthibitisho wa kitabibu? Kindly elaborate (Sky Eclat
Hii ni hali inayojirudia na kwa wale wanaopata maumivu makali hupelekwa kwa daktari mpaka wanapopata njia muafaka ya kutuliza maumivu kila mwezi.

Wengine wanajua njia wanazotumia kutuliza maumivu, kwa hawa wanaweza tu kuutaarifu uongozi wa shule kuwa hawataweza kuhudhuria darasa kwa siku hiyo. Register itaonyesha kama kuna wanao chukua muda huu zaidi ya mara moja kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom