Tumbo la mwezi kwa vigoli (Dysmenorrhoea) iwe sababu maalum ya kukosa mahudhurio ya darasani siku mbili kwa mwezi

Ni kweli kuna idadi ya wanaopata maumivu haya lakini si mabinti wote. Hata hivyo kuna sehemu ambazo bado ni taboo kuongelea tumbo la heshima. Kuwe na njia rahisi itakayoweka mawasiliani rahisi na ya kueleweka binti anapohitaji muda huu kujiuguza.
 
Naunga mkono hoja,

Ifanyiwe kampeni haraka, watoto wanateseka sana.
 
Kwa mujibu wa Madocter wanasema haupaswi kuona ni kawaida pale unapopata maumivu kila unapoingia kwenye hizo siku zenu, Unashauliwa kumuona dactatari ili upate matibabu, kwani kawida haupaswi kupata maumivu ya kukufanya ushindwe kazi ya aina yoyote ukioana hivyo uje kuna vitu haviko sawa kiafya ila wengi wenu mna puuzia na kuona ni kawaida kupata hayo maumivu. so simple kama unapata maumivu nenda hospital katibiwe kazi iendeleee!
 
Ni kweli kuna idadi ya wanaopata maumivu haya lakini si mabinti wote. Hata hivyo kuna sehemu ambazo bado ni taboo kuongelea tumbo la heshima. Kuwe na njia rahisi itakayoweka mawasiliani rahisi na ya kueleweka binti anapohitaji muda huu kujiuguza.
Natumaini tumekubaliana hapo juu, sawa tukija kwenye ishu ambalo umeigusia la Taboo kwenye jamii kuengelea swala la hedhi kwa watoto wa kike na wanawake kiujumla, kwa my simple mind ni swala la elimu tu linahitajika sababu swala la hedhi ni ishu ya kibaolojia nothing special kutokana na mmong'onyoko (kumradhi ashakum si matusi kama nimekosea lugha hapo) wa damu zilizoambata na tishu kutoka nje ya mwili wa binadamu kupitia njia ya uzazi (Menstrual flow) pindi yai lisiporutubishwa na mbegu za kiume! So mechanism hiyo ya kibailojia sio tatizo kuiongelea maana ni sawa sawa na mechanism zingine za kibailojia zinafanyika ndan ya mwili kama kumeng'enywa chakula ili mwili upate nguvu na virutubisho uweze kufanya kazi ipasavyo.
So Elimu tu inahitajika but naamini tunaenda at the right direction, so dont worry the society will understand you if not today, tomorrow!

Over and Out!
 
Nilipokuwa JKT kwa mujibu wa sheria baada ya kumaliza Kidato cha 6, wasichana walikuwa wakitamka kwenye gwaride 'Nina ugonjwa wa Matron' na wanapewa off baada ya matron kwenda faragha na mhusika kuthibitisha kwamba msichana huyo kweli yuko mwezini.
kwani mada inazungumzia jeshini?
 
Hii mada muhimu sana,inatakiwa wahusika,walichukulie kwa uzito wa Hali ya juu.Wanafunzi wengi wa kike,wanapata tabu sana,wakati wa masomo na wakati wa mitihani,nakumbuka wakati tunasoma,yupo mwanafunzi wa kike hii hali ilimkuta darasani,akashindwa kuinuka kwenye dawati,baada ya nguo zake kuchafuka,bahati mwalimu akatumia busara,ya kututoa nje,wanafunzi wa kiume.
 
Poleni sana,sasa nyie kama wanawake mpaze sauti zenu kwa serikali tukufu iweze kuwasaidia jamii ya akina mama na wasichana hapa nchini na duniani kwa ujumla.
 
Mtu ambae hajawahi/haumwi hili tumbo ni rahisi kusema hivi na vile...linauma sana jamani huku miguu na kutapika juu, wahanga ni wengi ila kulisema wazi ndo inashindikana..!
Ni mateso makali..
Ila ikiwekwa wazi hata km ingekua mimi na utu uzima huu ama ht zamani nisingesema..

Ningeugua kimya kimya tu...

Iwe tu binti anaomba ruhusa akiona hajiwezi..
 
Mhhh sio kweli...
Kuna vitu havina tiba ya kudumu na menstrual cramps ni mojawapo

Unaweza tu kupata ahueni kwa dawa,massage,yoga.,kulala nk
 
Umeongelea maumivu haya yanapotokea wakati wa mitihani , hili hata mimi sikuwahi kukiwaza. Sifahamu kama kuna muda unatolewa ili mhitimu amalize mitihani yake yote au inampasa binti kupoteza mwaka mzima wa masomo. Changamoto ni nyingi sana.
 
Mashuleni huwa wanapewa ruhusa mkuu.

Kwa huu ushauri wako utaongeza zaidi watoro mashuleni kwasababu ni ngumu kuthibitisha hayo maumivu kwa mtu.

Lakini pia siku huwa zinatofautiana, si ndio?? Kama ni hivyo itawawia vigumu mno walimu kufundisha kwasababu kila leo kutakua na wanafunzi kadhaa hawapo darasani, na bahati mbaya zaidi wengine wengi watatumia njia hiyo kwa utoro na uvivu tu.

Ila kwa hili huwa nawapa kongole wanawake, wengi wenu mnajua kujiswafi mpaka msijulikane ni wakati gani mnaingia huko mwezini.
 
Feminists bwana! Wakati mwingine kama nyaya zinakatikaga vichwani mwao.
 
na je likimkuta kwenye mtihani muhimu kama necta inakuaje? asipokuja hizo siku mbili baraza la mtihani lipewe taarifa alikua hedhi kwahiyo wamuongezee muda? nikweli hedhi ina maumivu makali lakini kuna dawa za kupoza kidogo waelimishwe wazitumie kuliko kujikaza kuvumilia maumivu.
 
Itabidi na kwenye mitihani mtengenezewe Marking scheme ya kike ili kufidia hizo siku mbili...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…