Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli kuna idadi ya wanaopata maumivu haya lakini si mabinti wote. Hata hivyo kuna sehemu ambazo bado ni taboo kuongelea tumbo la heshima. Kuwe na njia rahisi itakayoweka mawasiliani rahisi na ya kueleweka binti anapohitaji muda huu kujiuguza.Ni wazi zuri ambalo umelitoa ingawa sikubaliani nalo, Tukienda kitaalamu zaid dysmenorrhoea (maumivu ya hedhi) sio wote wanaopata maumivu haya ni asilimia kadhaa ya wasichana wa kike, so kufanya generalization ya maumivu ya hedhi wanayopata asilimia kadhaa ya wasichana, kwamba wapate exemption ya kutohudhuria darasani au kwenye shughuli zingine za kimasomo au zingine zozote sidhani ni sahihi!
Ofcoz nakubaliana kwa namna moja au nyingine kwa baadhi wa wanayopata maumivu hayo kwa kiwango kikubwa (ivuke threshold level) sababu wengi wao wanapata maumivu hayo kwa kiwango kidogo in such a way it doesn't affect them intellectually or even psychologically, sawa kuna namna ambayo inawaathiri physiologically and psychologically, lakini Intellectually unapima kati ya benefits and drawbacks ratio, haileti mantiki ya wao kutohudhuria masomo yao kwa kundi la wachache ifanyiwe generalization kwa kundi la wengi, wakati data zinaongea ndivyo sivyo! So research zaid ifanyike kuona namna gan mambo yalivyo na yafanyiwe evaluation especially kwenye kupima benefits and drawbacks ratio!
Na kwa haraka haraka nnavyofahamu kwa watoto wa kike wanaosumbuliwa na tumbo au ugonjwa wengine wowote huwa wanaomba ruhusa na kupewa ya kujiuguza, sijawahi experience kwa kuona au kusikia, mwanafunzi wa kike anaomba ruhusa na kukatiliwa kisa kwa sababu haipo kwenye miongozo ya kupewa ruhusa pindi apatapo maumivu ya hedhi!
Nawasilisha!
Natumaini tumekubaliana hapo juu, sawa tukija kwenye ishu ambalo umeigusia la Taboo kwenye jamii kuengelea swala la hedhi kwa watoto wa kike na wanawake kiujumla, kwa my simple mind ni swala la elimu tu linahitajika sababu swala la hedhi ni ishu ya kibaolojia nothing special kutokana na mmong'onyoko (kumradhi ashakum si matusi kama nimekosea lugha hapo) wa damu zilizoambata na tishu kutoka nje ya mwili wa binadamu kupitia njia ya uzazi (Menstrual flow) pindi yai lisiporutubishwa na mbegu za kiume! So mechanism hiyo ya kibailojia sio tatizo kuiongelea maana ni sawa sawa na mechanism zingine za kibailojia zinafanyika ndan ya mwili kama kumeng'enywa chakula ili mwili upate nguvu na virutubisho uweze kufanya kazi ipasavyo.Ni kweli kuna idadi ya wanaopata maumivu haya lakini si mabinti wote. Hata hivyo kuna sehemu ambazo bado ni taboo kuongelea tumbo la heshima. Kuwe na njia rahisi itakayoweka mawasiliani rahisi na ya kueleweka binti anapohitaji muda huu kujiuguza.
kwani mada inazungumzia jeshini?Nilipokuwa JKT kwa mujibu wa sheria baada ya kumaliza Kidato cha 6, wasichana walikuwa wakitamka kwenye gwaride 'Nina ugonjwa wa Matron' na wanapewa off baada ya matron kwenda faragha na mhusika kuthibitisha kwamba msichana huyo kweli yuko mwezini.
Hii mada muhimu sana,inatakiwa wahusika,walichukulie kwa uzito wa Hali ya juu.Wanafunzi wengi wa kike,wanapata tabu sana,wakati wa masomo na wakati wa mitihani,nakumbuka wakati tunasoma,yupo mwanafunzi wa kike hii hali ilimkuta darasani,akashindwa kuinuka kwenye dawati,baada ya nguo zake kuchafuka,bahati mwalimu akatumia busara,ya kututoa nje,wanafunzi wa kiume.Wanawake na mabinti wengi walipitia ama wanapitia maumivu ya tumbo la mwezi Dysmenorrhoea kila mwezi. Maumivu haya yana athiri uwezo wa mwili kisaikolojia, fizikia hata kujichanganya na wenzako inakuwa shida. Wengi hasa hupata maumivu haya siku moja au mbili ambazo wengine hutapika na tumbo kuuma pamoja na miguu kushindwa kutembea.
Wengi hutumia panadol na dawa nyingine za kutuliza maumivu ili kutuliza makali ya tumbo hil, wengine hushinda na chupa za maji ya moto na wengine wanahitaji matubabu zaidi ya kitaalamu hata kufanyiwa upasuaji. Hii ni asili ya binadamu huwezi kuidharau na hii ni mfumo wa jamii kuzalisha na kuongezeka duniani.
. Katika dunia ya mfumo dume hili tatizo halijawahi yakinishwa. Binti hupoteza siku mbili ambazo hawezi kuhudhuria masomo. Bahati iwe nzuri tumbo hili lianze kuuma Jumamosi, unaweza kutumia weekend kujitibu. Likianza Jumatatu ni shida mno.
Tukiwa tunapambana na kumpatia mtoto wa kike taulo za kujikinga. Kwa wale wahanga ni muhimu kufikiriwa muda huu wa siku mbili kwa mwezi wawe exempted kujiuguza.
Umeleta mada muhimu sana,hii ndio mada ya kuchangiwa na wengi.Ni rahisi kusema uliumwa malaria ueleweke kuliko kusema tumbo la mwezi. Jamii zetu nyingi zinachukulia mambo ya mfumo wa uzazi ni kitu cha faragha.
Ni mateso makali..Mtu ambae hajawahi/haumwi hili tumbo ni rahisi kusema hivi na vile...linauma sana jamani huku miguu na kutapika juu, wahanga ni wengi ila kulisema wazi ndo inashindikana..!
Mhhh sio kweli...Kwa mujibu wa Madocter wanasema haupaswi kuona ni kawaida pale unapopata maumivu kila unapoingia kwenye hizo siku zenu, Unashauliwa kumuona dactatari ili upate matibabu, kwani kawida haupaswi kupata maumivu ya kukufanya ushindwe kazi ya aina yoyote ukioana hivyo uje kuna vitu haviko sawa kiafya ila wengi wenu mna puuzia na kuona ni kawaida kupata hayo maumivu. so simple kama unapata maumivu nenda hospital katibiwe kazi iendeleee!
Umeongelea maumivu haya yanapotokea wakati wa mitihani , hili hata mimi sikuwahi kukiwaza. Sifahamu kama kuna muda unatolewa ili mhitimu amalize mitihani yake yote au inampasa binti kupoteza mwaka mzima wa masomo. Changamoto ni nyingi sana.Hii mada muhimu sana,inatakiwa wahusika,walichukulie kwa uzito wa Hali ya juu.Wanafunzi wengi wa kike,wanapata tabu sana,wakati wa masomo na wakati wa mitihani,nakumbuka wakati tunasoma,yupo mwanafunzi wa kike hii hali ilimkuta darasani,akashindwa kuinuka kwenye dawati,baada ya nguo zake kuchafuka,bahati mwalimu akatumia busara,ya kututoa nje,wanafunzi wa kiume.
Asante kumuelimisha muulizaji.Ni sehemu mojawapo ambapo baadhi ya vijana wa kike hutumia muda katika maisha yao.
Anakopi notes kutoka kwa wenzake. Lakini siyo wote wanaumwa mpaka hawendi shule au chuo.Halafu masomo aliyopoteza kwa hizo siku mbili za "mapumziko" anayafidiaje?