Nami nakubaliana na wewe Tanzania tuna Tume Bora kabisa ya uchaguzi tatizo letu watanzania tunaendeshwa na matamko ya wanasiasa yasiyo na nia njema tunapaswa kuamini kuwa hakuna Viongozi wanaopenda nchi zao ziwe na machafuko ndio maana kila jambo Lina msemaji wake tukiacha kila mtu ajisemee lolote analotaka kama walivyofanya Kenya kwenye uchaguzi kwamba kila mtu anakua na matokeo yake si salama kwa Taifa. Sipingi kuwa tunahitaji uwazi kwenye uchaguzi au Kenya wamefanya vibaya lakini Kuna mambo mengine ni ya kuyaangalia mapema nini matokeo yake kabla ya kuruhusu kufanyika tatizo linalotokea Sasa hivi Kenya ni matokeo ya kuruhusu kila mtu kuwa na msemaji na kuwa na matokeo yake kila mtu ameenda kwenye ukumbi wa Bomas na matokeo yake mfukoni.