Tume Huru ya Uchaguzi imemebaki Tume ya Uchaguzi ya Tanzania

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Huwa siamini hata kidogo kama upo uwezekano wa kupata tume huru ya uchaguzi kwa namna kama Kenya walivyofanya; au hata Zanzibar walivyowahi kufanya. Kwa kilichotokea Kenya kupitia baadhi ya wajumbe kuyakana matokeo ya kazi yao natangaza kuwa Tanzania tuna tume bora na huru ya uchaguzi

 
Naunga mkono hoja
Nami nakubaliana na wewe Tanzania tuna Tume Bora kabisa ya uchaguzi tatizo letu watanzania tunaendeshwa na matamko ya wanasiasa yasiyo na nia njema.

Tunapaswa kuamini kuwa hakuna Viongozi wanaopenda nchi zao ziwe na machafuko ndio maana kila jambo Lina msemaji wake tukiacha kila mtu ajisemee lolote analotaka kama walivyofanya Kenya kwenye uchaguzi kwamba kila mtu anakua na matokeo yake si salama kwa Taifa.

Sipingi kuwa tunahitaji uwazi kwenye uchaguzi au Kenya wamefanya vibaya lakini Kuna mambo mengine ni ya kuyaangalia mapema nini matokeo yake kabla ya kuruhusu kufanyika tatizo linalotokea Sasa hivi.

Kenya ni matokeo ya kuruhusu kila mtu kuwa na msemaji na kuwa na matokeo yake kila mtu ameenda kwenye ukumbi wa Bomas na matokeo yake mfukoni.
 
Una muabisha baba ako we mtoto.
 
Tume ya kutangaza kushinda bila kupingwa ndio tume yako bora! Sawa kila mja ana mtazamo wake
 
Uko serious au unatania[emoji850]?
 
Chadema waliokuwa wanasema Kenya kuna tume huru ya uchaguzi sijui watasema nini tena kuhusu yale yaliyotokea ukumbini
 
Sijaelewa....mada yenu mnaendesha baada ya kutoka kwenye mataputapu au mnaandika ili kujifurahisha. Tume yetu Ni remote control ya aliyeiweka. Akisema Mkurugenzi asikuyangaze hata vipi fomu inaweza chanwa mbele yako na hufanyi kitu. Kwa Kenya matatizo yanakuja kwenye matokeo tu.....kwingine kote saaaafiiii Ila usiguse matokeo tu. Sasa hapa Nini Bora.....tubaki Ni kuwa siku ukipata rungu jitangazie tu jimbo
 
Chadema waliokuwa wanasema Kenya kuna tume huru ya uchaguzi sijui watasema nini tena kuhusu yale yaliyotokea ukumbini
Aisee ,NCHI ya watu wa ajabu Sana..[emoji1787]ETI huyu nae akirudi nyumban anaitwa BABA[emoji1787]
 
Acheni kuwaonea wivu Wakenya na demokrasia yao. Sisi tujilaumu wenyewe kwa kukubali kuburuzwa na chama kimoja miaka 60.
 
Acheni kuwaonea wivu Wakenya na demokrasia yao. Sisi tujilaumu wenyewe kwa kukubali kuburuzwa na chama kimoja miaka 60.
Chadema bhana, vyama vingi c vimeanza 1995 sasa hy miaka 60 imefikaje.? Bogus ww
 
Mbuluma wako wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…