PreGE2025 Tume Huru ya Uchaguzi yatangaza majimbo mapya nane, Dar es Salaam yapata Kivule na Chamazi

PreGE2025 Tume Huru ya Uchaguzi yatangaza majimbo mapya nane, Dar es Salaam yapata Kivule na Chamazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele leo Mei 12,2025 ametangaza kuwa Tume hiyo imekubali kuanzisha Majimbo mapya ya uchaguzi nane katika Mikoa mbalimbali nchini ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanzishwa Majimbo mapya mawili ambayo ni Jimbo la Kivule na Jimbo la Chamazi.

1747041154250.png

====

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kukubali kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi nane katika mikoa mbalimbali nchini huku majimbo 12 yakibadilishwa majina.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema;

1. Katika mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jipya la Uyole

2. Katika mkoa wa Dodoma, limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba.

3. Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya la Bariadi Mjini ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa.

4. Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili ambayo ni Katoro na Chato Kusini yakigawanywa majimbo ya Busanda na Chato.

5. Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jipya la Itwangi.

6. Katika Mkoa wa Dar es salaam Majimbo mawili yamegawanywa na kuanzishwa majimbo mapya mawili ambapo Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jipya la Kivule, na jimbo la Mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.

Soma, Pia
 
Attachments

Tume Huru ya Uchaguzi imetangaza
mabadiliko makubwa ya kiutawala katika mipaka ya majimboya uchaguzi chini, ikiwemo mabadiliko ya majina ya majimbo 12 na kuanzishwa kwa majimbo mapya 8.

View: https://www.youtube.com/live/VeEefbyioOE?si=pfdJQLer_JOcZGwg
Kwa mujibu wa tarifa ya tume, majimbo hayo mapya yameanzishwa kutokana na kugawanywa kwa baadhi ya
majimbo yaliyokuwa na ukubwa mkubwa au ongezeko la watu, hatua inayolenga kuboresha uwakilishi wa wananchi.

Majimbo mapya yaliyoanzishwa ni kama ifuatavyo:Majimbo Mapya ya Uchaguzi: Kivule lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Ukonga, Mkoa wa Dar es Salaam na Chamazi - lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Mbagala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Mengine ni Mtumba lililoanzishwa baada ya kugawanywakwa Jimbo la Dodoma Mjini, Mkoa wa Dodoma, Uyole lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbeya na Bariadi Mjini lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

Pia lipo Katoro lillloanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Busanda, Mkoa wa Geita, Chato Kusini lilioanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Chato, Mkoa wa Geita na Utwangi lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Solwa, Mkoa wa Shinyanga.

Tume imesema mabadiliko haya ni sehemu ya maboresho ya mipaka ya kiutawala ili kuhakikisha uwiano wa idadi ya watu kwenye majimbo ya uchaguzi na ufanisi wa uwakilishi wa wananchi bungeni.

Source: Global tv
 
Kwa dsm yanatakiwa yaongezwe. Hii ni kwa mujibu ya kanuni ya uwakilishi.
 
Ahsante jimbo langu halikuganwanywa. Jimbo lina idadi ndogo sana ya wananchi lakini mbunge wa zamani baada ya kuona hataweza kushinda uchaguzi ujao, akahamasisha jimbo ligawanywe ili wagawane na mbunge aliepo sasa.

Nashukuru tume imepiga chini hayo maombi ya kipumbavu. Niligombana na mbunge wa zamani kwa kupinga hoja yake ya kugawa jimbo ili yeye agombee. Sasa ngoja niendelee kukorofishana nae kwenye WhatsApp.
 
Yaani mkoa wa mwanza hasa wilaya ya misungwi na ilemela wameshindwa kuanzisha jimbo kweli?
 
Ungejiuliza faida za kugawanya haya majimbo kwa nchi masikini kama yetu loh? sijui nani ameturoga hao wenyewe waliopo ni mzigo kwa nchi masikini kama yetu, leo mnakuja kuongeza tena majitu kisa watoto wenu wachaguliwe , hilo la chattle najua mnataka mumuhonge yule kilaza wa jiwe aliyepata foo ila ana digirii na mastazi, kimsingi hiyo ni nchi ya kugawana mbao tu na si kupambana kutatua shida za wananchi.
 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele leo Mei 12,2025 ametangaza kuwa Tume hiyo imekubali kuanzisha Majimbo mapya ya uchaguzi nane katika Mikoa mbalimbali nchini ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanzishwa Majimbo mapya mawili ambayo ni Jimbo la Kivule na Jimbo la Chamazi.

====

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kukubali kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi nane katika mikoa mbalimbali nchini huku majimbo 12 yakibadilishwa majina.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema Katika mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jipya la Uyole

Katika mkoa wa Dodoma, limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba.

Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya la Bariadi mjini ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa.

Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili ambayo ni Katoro na Chato Kusini yakigawanywa majimbo ya Busanda na Chato.

Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jipya la Itwangi.

Katika Mkoa wa Dar es salaam Majimbo mawili yamegawanywa na kuanzishwa majimbo mapya mawili ambapo Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jipya la kivule, na jimbo la mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.

Soma, Pia
Tume huru ipi, ile ya ccm? Kule kuna watu wana mashati ya kijani
 
nikijua mchango wa wabunge waliopo bungeni, nitaelewa kugawanya majimbo ya uchaguzi vinginevyo ni akili ndogo za mtu mweusi.
wananchi hawana shida na idadi ya majimbo yaliyopo. wana shida na mchango toka kwa wabunge waliopo
 
Back
Top Bottom