PreGE2025 Tume Huru ya Uchaguzi yatangaza majimbo mapya nane, Dar es Salaam yapata Kivule na Chamazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
nawapongeza Tume kwa jambo zuri walilofanya, Ndoto yangu ya kuwa Mbunge mahala hapo baadae ipo pale pale, ngoja nijipange kikamilifu. japo majimbo yote yana vigogo, lakini nitatia NIA tu.
 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele leo Mei 12,2025 ametangaza kuwa Tume hiyo imekubali kuanzisha Majimbo mapya ya uchaguzi nane katika Mikoa mbalimbali nchini ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanzishwa Majimbo mapya mawili ambayo ni Jimbo la Kivule na Jimbo la Chamazi.

====

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kukubali kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi nane katika mikoa mbalimbali nchini huku majimbo 12 yakibadilishwa majina.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema Katika mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jipya la Uyole

Katika mkoa wa Dodoma, limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba.

Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya la Bariadi mjini ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa.

Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili ambayo ni Katoro na Chato Kusini yakigawanywa majimbo ya Busanda na Chato.

Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jipya la Itwangi.

Katika Mkoa wa Dar es salaam Majimbo mawili yamegawanywa na kuanzishwa majimbo mapya mawili ambapo Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jipya la kivule, na jimbo la mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.

Soma, Pia
Naona jelly anataka kuikimbia kivule
 
Halafu mtu anasema uchaguzi uhairishwe! kama TrueVoter
..andika vzr wewe, "uhairishwe" ndio neno gani?
Acha kukariri mambo km kasuku, eleza maana ya kuahirisha uchaguzi ni nini..hakuna sababu ya kuingia gharama ya maisha ya watu, pesa, muda na utu kwa jambo ambalo linafanyika km ushahidi tu kwamba na Tanzania huwa inafanya uchaguzi mkuu..ni bora kutofanya uchaguzi tukakubaliana watawala waendelee hadi pale Mungu ataamua vinginevyo!
 
Yaani Tanzania tunafanya uchaguzi ili kutakatisha Madaraka tu
 
lengo la kuongeza majimbo ni kupanua wigo wa uwakilishi wa wananchi katika vyombo vya maamuzi kitaifa, lakini pia kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi, full stop.

kinyume na hapo ni upotoshaji gentleman :putinWalk:
Zidumu fikra za Mwenyekiti
 
Ndo maana nakwambia we ni chawa mbobevu kila kitu ndiyoo kula mkojo ndiyo
narudia tena,
INEC inawajibika kuskiza na kuzingatia maoni na mapendekezo ya wananchi,
na kwahivyo inawajibu wa kugawanya majimbo ya uchaguzi yaliyokidhi vigezo na sifa za kisheria,
na hatimae kuongeza wigo wa uwakilishi wa wananchi kwenye vyombo vya maamuzi kitaifa na kusogeza huduma muhimu za kijamii karibu zaidi na wananchi.

ni muhimu san kufahamu haya bila mihemko gentleman :pulpTRAVOLTA:
 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele leo Mei 12,2025 ametangaza kuwa Tume hiyo imekubali kuanzisha Majimbo mapya ya uchaguzi nane katika Mikoa mbalimbali nchini ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanzishwa Majimbo mapya mawili ambayo ni Jimbo la Kivule na Jimbo la Chamazi.

====

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kukubali kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi nane katika mikoa mbalimbali nchini huku majimbo 12 yakibadilishwa majina.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema Katika mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jipya la Uyole

Katika mkoa wa Dodoma, limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba.

Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya la Bariadi mjini ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa.

Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili ambayo ni Katoro na Chato Kusini yakigawanywa majimbo ya Busanda na Chato.

Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jipya la Itwangi.

Katika Mkoa wa Dar es salaam Majimbo mawili yamegawanywa na kuanzishwa majimbo mapya mawili ambapo Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jipya la kivule, na jimbo la mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.

Soma, Pia
Eti Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 😕😡
 
Back
Top Bottom