Tume iko wapi kukibana CCM na mgombea wake ili kutengua uteuzi wake? Tume itende haki

Tume iko wapi kukibana CCM na mgombea wake ili kutengua uteuzi wake? Tume itende haki

mkulimamiwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
2,591
Reaction score
5,315
Moja ya mambo ambayo yakija kutokea huko mbeleni pengine kutokea machafuko nchini kwa kisababishi cha upendeleo wa kunyamazia mambo yanayotokea CCM na mambo hayo hayo hayanyamaziwi yanapotokea vyama pinzani

Tunapozungumza leo, Chadema imesimamishwa mikutano, luzuku na hata kiongozi yoyote kufanya press yoyote na waandashi wa habari kwa sababu eti, haikufuata sheria za uchaguzi kupata viongozi wao ndani ya chama

Lakini, mambo hayo hayo ambayo yanasadikika kufanyika Chadema, yamefanyika wazi wazi kwa chama kilichopo madarakani CCM

Hivi, Haki iko wapi?

Ni nani ataitwa muuwaji yakitokea machafuko ambayo sababu yake ni huu upendeleo?

Hatuombei yatokee, lakini kwa Nini Tume na mwenyekiti wake wananyamazia kuvunjwa kwa kanuni na sheria za uchaguzi ndani ya chama cha CCM?

Ninaimani, mambo haya iwapo yangetokea ACT na ama chama kingine, wangekiangazia kwa kutokukubaliana na uchaguzi huo

Tunaiomba Tume Itende haki

Ikizuwie CCM kuendelea na kampeni zake ili warudi kwenye uteuzi na uchaguzi huru unaoendana na sheria zake
 
Viongozi wa Tume ni wateule wa Rais, wakiambiwa hii katiba haifai ndio Kwanza "wanajichetua"
 
Tanzania haikuwa tayari kupokea mfumo wa vyama vingi

Mambo yanayofanywa na watawala pamoja na tume ni mambo ya hovyo sana
 
Back
Top Bottom