PostGE2025 Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 yaongezewa muda mpaka Aprili 3, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wazo la katiba mpya Lina uwawa hivyo!
 
DAR ES SALAAM:* MAMLAKA ya Uteuzi imeongeza muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025 na kuitaka ikamilishe kazi na kuwasilisha Taarifa yake kabla au ifikapo tarehe 3 Aprili, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa katika gazeti la serikali Tume imeongezewa muda huo ili kutoa fursa na muda wa kutosha kwa kila mwenye taarifa, ushahidi au maoni, aliyepo nchini au nje ya nchi, kuwasiliana na Tume ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote, au taasisi yoyote, itakayokosa nafasi ya kusikilizwa.

Sababu nyingine za kuongeza muda ni pamoja na zifuatazo Wingi na mchanganyiko wa taarifa zilizokusanywa, na zinazoendelea kukusanywa, na Tume ambazo zinahitaji muda zaidi wa kufanyiwa uchambuzi wa kina, Tume kulazimika kutumia Wataalamu (experts) kutoka ndani na nje ya nchi wenye uwezo wa kufanya uchunguzi wa kisayansi, na uchambuzi wa kidijitali wa baadhi ya taarifa na vielelezo kutokana na aina ya matukio na ushahidi uliokusanywa hadi sasa, na unaoendelea kuwasilishwa.

Sababu nyingine ni Tume kubaini mapengo kadhaa katika taarifa na vielelezo vilivyokusanywa hadi sasa hivyo kuhitaji kutafuta au kupata taarifa zaidi ili kukamilisha ushahidi kwa kila hoja inayohusika, Kutoa fursa kwa wadau wachache muhimu ambao kwa sababu mbalimbali bado hawajafika mbele ya Tume, licha ya kupelekewa mialiko zaidi ya mara moja.

Taarika hiyo imewataja wadau hao kuwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa dini, viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi na Wingi wa wananchi wengine wanaoendelea kufika mbele ya Tume kuwasilisha taarifa, ushahidi na ushauri wao.

Kutokana na fursa hiyo ya Tume kuongezewa muda Tume kupitia Mwenyekiti wake Jaji Othuman Chande inatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuwasilisha ushahidi kwenye Tume kwa kutumia njia zote zilizokuwa zimeainishwa awali ambazo ni majadiliano ya ana kwa ana, mawasilisho ya maandishi (written submissions) kwa njia ya posta au tovuti maalumu ya Tume; barua pepe; ujumbe mfupi wa simu (SMS); kujaza dodoso maalumu kwenye mtandao (www.tume.uchunguzi.go.tz), au kwa kupitia mitandao mingine ya kijamii.

Pia tume hiyo imetoa wito maalumu kwa baadhi ya viongozi wa dini, viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi ambao wamepewa mialiko na Tume lakini bado hawajafika mbele ya Tume kutumia fursa hii kufika au kuwasiliana na Tume kutoa mchango wao katika uchunguzi unaoendelea kwa manufaa ya wananchi, wadau na nchi kwa ujumla.

Taarifa hiyo pia kupitia Gazeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaeleza Umma umuhimu wa kuendelea kuipa Tume ushirikiano ili kuiwezesha kukamilisha kazi yake ya uchunguzi. Kama ilivyokuwa mwanzo, Tume itaendelea kufanya vikao vya wazi (public hearing) isipokuwa pale ambapo mashahidi kwa faida ya usalama wao hawapendi majina yao, sura na taarifa zao zitolewe kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Mpango Kazi, Tume ilipaswa kuwasilisha Taarifa kabla au ifikapo tarehe 20 Februari 2026 ikiwa ndani ya siku 90, ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 20 Novemba, 2025 mara baada ya kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais.
 
Hakuna namna lazima bibi wa Kizimkazi ajibu kuhusu mauaji aliyoamrisha!
 
Halaf Kidudu mtu chenyewe kimejificha zake kwao Zanzibar kinatumbua tu hela za Tanganyika. Shenzy kabisa🚮🚮
 
Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na viongoz wa juu wanaenda tolewa kafara baada ya tume kutoa report...

Siasa ni mbaya sana,haswa mahali ambapo katiba na sheria za nchi ziko chini ya watu flani flani!

Wanaenda kutoka kwa aibu na doa ambalo halitafutika katika historia ya hili Taifa na maisha yao na vizzazi vyao!
 
Katiba hairuhusu kuteua waziri toka chama kingine
Mkitunga uwongo jitahidini uwe na nukta za ukweli
Kwenye maridhiano hamnaga Cha katiba maana wenye katiba ni wao wenyewe CCM sio wananchi, wanauwezo wa kupindisha kivyovyote kama ilivyo kawaida Yao, ili waendelee kukaa MADARAKANI.

Maana yake CHADEMA wakikubali maridhiano CCM itaendelea kuongoza na samiah ataendelea kuwa madarakani
 
Hapa Pana tatizo. Kuendelea kuruhusu kupokea taarifa bila huko wa muda.l, ni njia inayoweza kuhalalisha kuendesha kuongezea muda Tume Hata ikifika huo mwezi wa nne. Itangazwe Rasmi tarehe ya ukomo wa kupokea taarifa, ili taarifa zitakazokuwa zimekusanywa zifsnyiwe kazi. Kisha ripotinya Tume iandaliwe na kutolewa.
 
Hii ni tume ya CCM, hamna Cha tume hapo msitarajie la maana lolote hapo
 
Utakuja ulombwe kwa huo uchawa mtoto wa kiume jishikilie ushikishwe ukuta maana unatuaibisha sana wanaume kutetea mambo ya kike!
 
Hakuna chaguo zaidi ya Samia na kundi lake lote kufikishwa mbele ya sheria na kwa waTanzania kuwachagua viongozi wanaowataka wao kuongoza taifa hili kwa UHURU na HAKI.

Hayo mengine yoooote ni porojo zisizokuwa na faida yoyote. Siku za kuwalaghai waTanzania zimekwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…