Wakuu,
Mambo magumu huko😂🤣🤣, hesabu naona kama zile ya Yanga, hata na kalkuleta bado ngoma mbichiiiii!
Hivi kesi ya Lissu inaenda mpaka tarehe ngapi tena?🌚 Jamaa bado anagoma kuingia kwenye Maridhiano ya mchongo?
Maana za ndaaaaaaaaani zinasema Lissu ameshafuatwa gerezani zaidi ya mara moja akubali maridhiano, wakina Heche na viongozi wengine wa CHADEMA wapewe vyeo vya uwaziri nk, lakini mwamba kagoma, wakina Boni wakatumwa wakafikishe ujumbe, wakaambiwa hii haiwezekani, nendeni wenyewe gerezani, wakaenda mwamba kagoma!
Na angekubali Watnganyika tungemla nyama🌚🌚, yaani wauwe ndugu zetu kwa maelfu halafu tusahau tu kama vile hakuna kilichotokea? Tukubali kuongozwa na wale wale, wanaotuua kila siku, wanaotuteka kila siku, wanaofanya kila juhudi kututaabisha na kuongeza ugumu wetu wa maisha? Hapana.
Kwa namna mambo yanavyoenda naona moja kati ya haya yanaenda kutokea;
- Kesi ya Lissu iishe, Samia ajiuzulu tuanze mchakato mwingine
- Samia apeleke lawama zote kwa jeshi la polisi, kwamba walifanya yale kwa maamuzi yao, yapatikane maridhiano (sijui yatakuwa ya namna gani)
- Lissu akutwe na hatia, afungwe, "Kinuke" tena
- ICC wafanye yao, CCM walazimishe Samia kujiuzulu, ufanyike mchakato mwingine wa uchaguzi!
Unadhani nini kinaenda kutokea?
Pia soma Ni miezi mitatu toka Rais Samia ateue Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, nini matarajio yako? Je, tunaelekea pazuri?
======
Tume ya Oktoba 29 imeongezewa siku 42, wanatakiwa kukamilisha majukumu yao April 3, 2026. Awali ilikuwa wakamilishe kabla au siku ya Februari 20, 2026, ila kutokana na sababu 5 walizotoa, ikiwemo wingi wa taarifa, pamoja na ulazima wa kutumia Wataalam, wameongezewa siku hizo ili kukamilisha kazi yao
===
TAARIFA YA KAWAIDA NA. 3352
TAARIFA YA KUONGEZA MUDA WA KUKAMILISHA KAZI YA TUME YA KUCHUNGUZA MATUKIO YA UVUNJIFU WA AMANI WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA ОКТОВА 2025
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 20 Novemba, 2025 mara baada ya kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais na ilitarajiwa kukamilisha kazi na kuwasilisha taarifa ndani ya kipindi cha siku 90. Kwa mujibu wa Mpango Kazi, Tume ilipaswa kuwasilisha Taarifa kabla au ifikapo tarehe 20 Februari 2026. Hata hivyo, kutokana na sababu zilizoainishwa hapa chini Tume haijakamilisha kazi yake.
HIVYO UMMA UNATANGAZIWA KUWA, Mamlaka ya Uteuzi imeongeza muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025 na kuitaka ikamilishe kazi na kuwasilisha Taarifa yake kabla au ifikapo tarehe 3 Aprili, 2026.
MADHUMUNI YA KUONGEZA MUDA ni kutoa fursa na muda wa kutosha kwa kila mwenye taarifa, ushahidi au maoni, aliyepo nchini au nje ya nchi, kuwasiliana na Tume ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote, au taasisi yoyote, itakayokosa nafasi ya kusikilizwa. Sababu nyingine za kuongeza muda ni pamoja na zifuatazo:
(a) Wingi na mchanganyiko wa taarifa zilizokusanywa, na zinazoendelea kukusanywa, na Tume ambazo zinahitaji muda zaidi wa kufanyiwa uchambuzi wa kina;
(b) Tume kulazimika kutumia Wataalamu (experts) kutoka ndani na nje ya nchi wenye uwezo wa kufanya uchunguzi wa kisayansi, na uchambuzi wa kidijitali wa baadhi ya taarifa na vielelezo kutokana na aina ya matukio na ushahidi uliokusanywa hadi sasa, na unaoendelea kuwasilishwa;
(c) Tume kubaini mapengo kadhaa katika taarifa na vielelezo vilivyokusanywa hadi sasa hivyo kuhitaji kutafuta au kupata taarifa zaidi ili kukamilisha ushahidi kwa kila hoja inayohusika;
(d) Kutoa fursa kwa wadau wachache muhimu ambao kwa sababu mbalimbali bado hawajafika mbele ya Tume, licha ya kupelekewa mialiko zaidi ya mara moja. Wadau hao ni pamoja na baadhi ya viongozi wa dini; viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi; na
(e) Wingi wa wananchi wengine wanaoendelea kufika mbele ya Tume kuwasilisha taarifa, ushahidi na ushauri wao.
KUTOKANA NA FURSA HII YA TUME KUONGEZEWA MUDA, TUME INATOA WITO UFUATAO:
1. Wananchi wote kuendelea kuwasilisha ushahidi kwenye Tume kwa kutumia njia zote zilizokuwa zimeainishwa awali ambazo ni majadiliano ya ana kwa ana, mawasilisho ya maandishi (written submissions) kwa njia ya posta au tovuti maalumu ya Tume; barua pepe; ujumbe mfupi wa simu (SMS); kujaza dodoso maalumu kwenye mtandao (
www.tume.uchunguzi.go.tz), au kwa kupitia mitandao mingine ya kijamii.
2. Wito maalumu unatolewa kwa baadhi ya viongozi wa dini; viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa, taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi ambao wamepewa mialiko na Tume lakini bado hawajafika mbele ya Tume kutumia fursa hii kufika au kuwasiliana na Tume kutoa mchango wao katika uchunguzi unaoendelea kwa manufaa ya Wananchi, Wadau na Nchi kwa ujumla.
UMMA UNAENDELEA KUKUMBUSHWA umuhimu wa kuendelea kuipa Tume ushirikiano ili kuiwezesha kukamilisha kazi yake ya uchunguzi. Kama ilivyokuwa mwanzo, Tume itaendelea kufanya vikao vya wazi (public hearing) isipokuwa pale ambapo mashahidi kwa faida ya usalama wao hawapendi majina yao, sura na taarifa zao zitolewe kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii.
KWA MAWASILIANO NA TUME, TAFADHALI TUMIA NJIA ZIFUATAZO:
Sanduku la Barua:
Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya
Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya
Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025,
Jengo la Benki Kuu ya Tanzania, Ukumbi wa Manyara.
S.L.P 471,
DAR ES SALAAM.
Tovuti:
www.tume.uchunguzi.go.tz
Baruapepe:
[email protected],
[email protected]
Ujumbe mfupi wa Simu-0737 305449, 0743 040890
WhatsApp-0737 305449
Mitandao ya kijamii (Instagram, x, Facebook) - tume_uchunguzi
Imetolewa na
MWENYEKITI WA TUME
18 Februari, 2026
View attachment 3547142View attachment 3547143View attachment 3547144
-