PostGE2025 Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 yaongezewa muda mpaka Aprili 3, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wazee wa people's power wanajitekenya na kucheka.
Hakuna mpinzani wa kweli anataka hisani ya rais muuaji. Vile vyama vyenu shikizi ndio vinahitaji hisani. Wapinzani wa kweli wanaweza kupata vyeo kihalali kwa ridhaa ya wananchi na sio kwa kujikomba.

Hiyo tume ya muuaji inafanya kwa utashi wa aliyeiteua, na lengo ni kuficha uovu wake. Ameisogezea muda ili pressure ishuke, lakini tunaojitambua toka mwanzo tulijua ni usanii wa wazi. Huyo muuaji aliunda tume kuchunguza utekaji wa Ali Kibao na wote waliotekwa, ripoti iliwahi kutoka? Ogopa porojo za muuaji.
 
Msingefanya vurugu za kipuuzi hata isingeundwa hiyo tume.

Tumieni akili siku nyingine kabla hamjaanzisha vurugu mkitaka kupigana na dola, mtawatia hasara kubwa wengi wasio na hatia.
 
Katiba hairuhusu kuteua waziri toka chama kingine
Mkitunga uwongo jitahidini uwe na nukta za ukweli
Ni kweli katiba hairuhusu "serikali shirikishi au mseto" lakini kama kweli wana mawazo haya maana yake kinachoweza kufanyika ni moja kati ya haya;

1. Wale CHADEMA akiwemo Tundu Lissu wanaokubaliana na wazo hili la Samuya wataingizwa serikalini kama walivyowahi kuingia CHADEMA wengine kama vile Dr Slaa, Patrobas Katambi, LijuaLikali nk. Hii sio kitu kingine isipokuwa ni hongo/rushwa

ATHARI ZA HILI NI:

👉🏻Hebu fikiri kama Tundu Lissu, John Heche, John Mnyika na wengine watakubaliana na ushenzi huu maana yake ni nini hasa? Ni kuwa, CHADEMA inakuwa imekufa kifo cha mende..!

IS IT POSSIBLE?

👉🏻JIBU: Hili ni wazo la kijinga, HALIWEZEKANI IWAPO TU CHADEMA ITAENDELEA KUWA CHINI YA UONGOZI WA TUNDU LISSU. Tunaelewa kuwa huu ndio mpango wenu CCM, ndio matamanio yenu. Lakini bahati mbaya ni kuwa hamuwezi kuyapata matamanio haya..!!!

2. Wanataka CHADEMA wakubali maridhiano pamoja na ofa hiyo kwa ahadi kuwa tutakaa mezani na kukubaliana kufanya minimal constitutional reforms ili ku - accommodate serikali mseto/shirikishi...

IS IT POSSIBLE?

No way. Samia, CCM na serikali yao they can't do this willingly until they get a vicious push...!!

Hii ni hadaa ya Samia na wahuni wenzake tu. CHADEMA sees things far more than these stupid CCM hooligans and their illegitimate government...!

WHAT IS THE BEST OPTION TO SOLVE THIS COMPLEX PUZZLE?​

👉🏻Ni Samia Suluhu Hassan na Serikali hii haramu yote kuachia ngazi ili kuruhusu uchaguzi mpya chini ya taratibu na sheria na katiba mpya...

👉🏻Wahalifu wa ubinadamu wote waliohusika na kuharibu uchaguzi wa 2025 (Tume ya uchaguzi yote), na wote waliohusika kwa kushiriki mauaji kuanzia waliotoa amri au maelekezo ya SHOOT and KILL, walioshika bunduki na kuua wote wawajibike kisheria na kisiasa..!!

👉🏻Ni maamuzi yanayoonekana kuwa ni magumu lakini ndio suluhu au jibu la mkwamo uliopo. Hakuna shortcut. There's no other clear and safe altenative. NI LAZIMA HIKI KIFANYIKE. Kuzunguka zunguka ili kutafuta watu wa kutwisha makosa ya watu wengine haitasaidia chochote na MUNGU WA MBINGUNI AMESHAKATAA..!!
 
"Tume kulazimika kutumia Wataalamu (experts) kutoka ndani na nje ya nchi wenye uwezo wa kufanya uchunguzi wa kisayansi, na uchambuzi wa kidijitali wa baadhi ya taarifa na vielelezo kutokana na aina ya matukio na ushahidi uliokusanywa hadi sasa, na unaoendelea kuwasilishwa". Lugha iliyotumika hapa ni Ile inayotumika dhidi ya mtu unayemuona mjinga.
 
Msingefanya vurugu za kipuuzi hata isingeundwa hiyo tume.

Tumieni akili siku nyingine kabla hamjaanzisha vurugu mkitaka kupigana na dola, mtawatia hasara kubwa wengi wasio na hatia.
Kwa taarifa yako bila machafuko hatutapata mabadiliko yoyote. Na machafuko yanatakiwa yawe makubwa sana hadi tupate Tanzania ya kweli. Kama mlitegemea mtapora chaguzi siku zote na tukae kimya kama makhanisi basi mmeukalia.
 
Maskini KODI ZETU!
ZINATUMBULIWA BILA HURUMA!
 
'' Tume inalazimika kutumia Wataalam kutoka ndani na nje ya Nchi wenye uwezo...'' Bw. Steven Joel Ntamusano si ulisema watu kutoka nje hawahitajiki!

''... Taarifa imewataja baadhi ya wadau kuwa viongozi wa Dini, Vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserkali na watu binafsi kufika mbele ya Tume licha ya kupewa mialiko zaidi ya mara moja'' Bw. Steven Joel Ntamusano tulikueleza Tume ya Jaji Chande inategemea hisani, haina nguvu za kumwita mtu. Kilichopaswa kuwepo kama alivyoshauri Prof Tibaijuka ni Tume ya Kijaji. Hao wote wangefika si kwa wito bali kwa ulazima '' summons''
 
Kwa taarifa yako bila machafuko hatutapata mabadiliko yoyote. Na machafuko yanatakiwa yawe makubwa sana hadi tupate Tanzania ya kweli. Kama mlitegemea mtapora chaguzi siku zote na tukae kimya kama makhanisi basi mmeukalia.
Akili za kina Lissu na Heche ndio hizi, machafuko yakitokea wanaokufa sio jamaa zako wa karibu hivyo huna uchungu wowote.

Uliza kina mama na baba walioomba misa kwenye makanisa katoliki baada ya kupoteza watoto wao namna wanavyoishi na uchungu kwa sababu ya upuuzi wenu wanaharakati.

Huwezi kupata Tanzania ya kweli kwa kutegemea machafuko, utaishi kupata waombolezaji wengi huko mitaani.

Utaishia kujaza roho za chuki na uasi miongoni mwa vijana wachache wa mijini, wakati huo wizara ya vijana inapambana kusambaza mitaji kwa maelfu ya biashara za ujasiriamali wa vijana.
 
Mkigoma mabadiliko ya kweli kwa njia ya amani, basi tutatumia njia mbadala. Vifo haviepukiki maama vinafanywa na wanaoshurutisha kukaa madarakani bila ridhaa ya umma.
 
Mkigoma mabadiliko ya kweli kwa njia ya amani, basi tutatumia njia mbadala. Vifo haviepukiki maama vinafanywa na wanaoshurutisha kukaa madarakani bila ridhaa ya umma.
Mabadiliko sio suala la kuamka na kuyafanya, sio sawa na biashara ya nyanya masokoni mkuu Tindo ni mchakato wenye kuhitaji muda ni masuala ya kisheria.

Ridhaa ipi ya umma wakati sisi tuliipigia kura CCM na mamilioni wengine pia walifanya hivyo.

Nyinyi mnaokuja kwa shari mtashughulikiwa kwa shari hiyo hiyo, msiende tu huko ICC kuanza kujilizaliza.
 
Huyo Tibaijuka aliwahi kuupinga mkataba wa DP World lakini alipopewa shule na wanasheria mpaka kesho haongelei tena suala lile.

Hayo ni matakwa ya wanasheria tume kuwa namna ilivyo.
 
Mabadiko yameanza kudaiwa tokq 1992, sasa unaposema sio suala la kulala na kuamka unamaanisha nini? Sheria zimeshabadilika nyingi sana toka wakati huo, sasa unaposema ni suala la kisheria unamaanisha nini?
 
Mabadiko yameanza kudaiwa tokq 1992, sasa unaposema sio suala la kulala na kuamka unamaanisha nini? Sheria zimeshabadilika nyingi sana toka wakati huo, sasa unaposema ni suala la kisheria unamaanisha nini?
Jifunzeni tu kutii sheria, huu ujanja wa kuleta vurugu hauna faida kwenu wala kwa mtu yoyote aliye hai.
 
Hiyo ni tume ya wapigaji tu wameomba kuongezwa siku ili waendelee kupiga pesa, hamna kitu hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…