The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi imekabidhi hati miliki za kimila kwa wakazi 360 wa Kijiji cha Mpinga, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, bila malipo yoyote. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za serikali kupunguza migogoro ya ardhi na mipaka vijijini.
Utoaji wa hati hizi ulifanyika baada ya Tume hiyo kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi kwa vijiji kumi, ambapo Mpinga kilichaguliwa kwa upangaji wa kina na upimaji wa ardhi kwa wananchi.
Wakazi waliopokea hati hizo wameeleza furaha yao, wakisema zitawasaidia kuepuka migogoro ya ardhi, ikiwa ni pamoja na unyang’anyi.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Tume hiyo, Suzana Mapunda, amesema mafanikio ya ugawaji wa hati hizo yametokana na matumizi ya mfumo wa kielektroniki, uliorahisisha ukusanyaji wa taarifa na kuandaa hati ndani ya siku tisa.
Amewataka wakazi wa Mpinga kuzitunza hati zao ili kuongeza usalama wa milki zao na kuchochea maendeleo.
Mbali na wananchi, taasisi za dini na serikali katika Kata ya Mpinga, ikiwemo shule tatu za msingi, zahanati moja, ofisi ya kijiji, na maeneo ya serikali, pia zimepewa hati miliki za kimila.