Haya ni maoni yangu binafsi ,sijatumwa na mtu au taasisi yoyote ile ,bali ni utashi wa nafsi yangu baada ya kufuatilia mwenendo wa mteule huyu wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema).
Kiongozi huyu kwa kauli zake alizozitoa wakati akitafuta wadhamini ni za shari sana na amekusudia kulibomoa taifa aidha kwa yeye kutojua ,au anajua kwa makusudi kabisa ,sitarudia kauli zake kwani ziko wazi mitandaoni na zinapoonekana kuwakera watanzania na kumshutumu ,hujaribu kuzi-neutralize akijifanya hakumaanisha kile ambacho ni kusudi lake kabisa toka moyoni bila shaka yoyote ile.
Lissu hayuko peke yake ,kuna kundi la baadhi ya maadui wa mafanikio ya taifa hili,ambao ndio wanamtumia kufanikisha mission zao kwa kigezo cha demokrasia kama ambavyo wameyabomoa mataifa mengi barani afrika ili yawe tegemezi daima na milele.mfano Libya ,Irak,Zimbabwe
Naiomba tume isipitishe jina lake kugombea nafasi ya urais kwa sababu ndio kihunzi ambacho maadui zetu wanaomba mchana na usiku wakivuke, wakifanikiwa watanzania muamini tunaenda kugawanyika na kusambaratika,huyu kiumbe kapangwa hata kama akishindwa kihalali akatae matokeo, na nchi ikisha ingia taharuki ndipo maadui watapata mwanya wa kufanya maovu yao dhidi ya mafanikio yetu.ifahamike taharuki hiyo itarudisha nyuma taifa kulekea kujitegema .
Lazima watanzania mfahamu kitendo cha kupunguza utegemezi ikiwemo gharama za uchaguzi ambazo zimekuwa zikigharamikiwa na mataifa ya nje kwa muda mrefu kwenye chaguzi karibu zote kimewakwaza sana ,hiyo ndio pia njia wanayoitumia kuhalalisha watawala wanaowataka kwa maslahi yao binafsi.
Nionavyo ni kheri ya nusu shari kuliko shari kamili,
Nusu shari ni tume kukata jina lake,na shari kamili ni kuruhusu jina la Lissu kugombea urais.
Hivi sasa mitandaoni kuna vijana wameajiliwa kuitisha au waweza sema kuiogopesha tume ya uchaguzi kwa threads za kila aina, mimi nasema wapuuzwe hiyo ni mission maalumu kutuingiza mkenge wakidai jina lake lisikatwe kwa kigezo cha kwamba hapatatosha
mimi nasema patatosha jina lake likatwe tu,kuruhusu jina lake kugombea ndio hapatatosha kabisa kwa dhamira aliyonayo yeye binafsi na maadui zetu,na hili litakua ni kosa la kiufundi ambalo tutajilaumu wenyewe.
Mwisho,umoja wetu ndio ushindi wetu dhidi ya maadui wa maendeleo ya taifa letu,kipindi hiki tushikamane haswa .