Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yamrejesha Boniface Jacob jimbo la Ubungo

Ina maana wametafakari kwa kina ama?.
 
Jimbo la Ubungo lina historia ya kuwa chini ya upinzani tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama bingo, kuanzia Massey wa CUF, JJ Mnyika wa CHADEMA na baadaye Saed Kubenea CHADEMA. Miaka yote ya uchaguzi CCM imekuwa ikifanya kila mbinu ili ilichukue lakini kila uchaguzi imekuwa ikizidiwa kimikakati na upinzani.

Ikumbukwe jimbo hilo linahusisha wasomi wa vyuo vikuu wengi kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ardhi, Maji na Chuo kikuu cha Sheria kilichopo Mawasiliano.

Wapiga kura wake wengi ni wenye uelewa ni vigumu kuwarubuni kwa kanga na kofia.

Tutegemee mchuano mkali.

=============

Matokeo ya Nyuma.

2015: Saed Kubenea CHADEMA kura 87,777, Dk. Didas MasaburiCCM kura 59,640.

2010: John Mnyika CHADEMA kura 66,742, Hawa Ngh’umbi CCM kura 50,544.

2005: Charles Keenja CCM.

2000: Hussein Mmasy CUF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…