Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yamrejesha Boniface Jacob jimbo la Ubungo

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yamrejesha Boniface Jacob jimbo la Ubungo

Ikumbukwe jimbo hilo linahusisha wasomi wa vyuo vikuu wengi kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ardhi, Maji na Chuo kikuu cha Sheria kilichopo Mawasiliano.
Kama ni hivyo mbona sasa Kitila Mkumbo ni mwenzao kwani alikuwa professa wa pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Si watamchagua msomi mwenzao badala ya huyo kilaza?
 
Atashinda kwa sababu CDM na ACT Wazalendo watagawana kura. Na kwa jinsi wanavyochukiana watatumia muda mrefu kushambuliana badala ya kumshambulia Kitila.

Amandla...
Waligawanya fito, ACT ya Ubungo walitokea Ubungo Chadema.
Advantage to Kitila Mkumbo.
 
Jimbo la Ubungo lina historia ya kuwa chini ya upinzani tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama bingo, kuanzia Massey wa CUF, JJ Mnyika wa CHADEMA na baadaye Saed Kubenea CHADEMA. Miaka yote ya uchaguzi CCM imekuwa ikifanya kila mbinu ili ilichukue lakini kila uchaguzi imekuwa ikizidiwa kimikakati na upinzani.

Ikumbukwe jimbo hilo linahusisha wasomi wa vyuo vikuu wengi kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ardhi, Maji na Chuo kikuu cha Sheria kilichopo Mawasiliano.

Wapiga kura wake wengi ni wenye uelewa ni vigumu kuwarubuni kwa kanga na kofia.

Tutegemee mchuano mkali.
=============

Matokeo ya Nyuma.

2015: Saed Kubenea CHADEMA kura 87,777, Dk. Didas MasaburiCCM kura 59,640.

2010: John Mnyika CHADEMA kura 66,742, Hawa Ngh’umbi CCM kura 50,544.

2005: Charles Keenja CCM.
2000: Hussein Mmasy CUF.
Tusiwasikie mnasema mmeibiwa kura.
 
Back
Top Bottom