Tume Ya Uchaguzi Inatakiwa Kumfuta Kwenye Orodha ya Wagombea.

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Sheria zetu za uchaguzi zinatamka wazi kuwa tokea mtu ametangaza nia ya kugombea, akianza kugawa zawadi kwa wapiga kura, hiyo itahesabika ni rushwa.

Sa100 tangu alipojitangaza kuwa yeye ni mgombea pekee wa nafasi ya Urais kupitia chama haramu, amegawa mitungi ya gas nchi nzima, amegawa pikipiki nchi nzima, amegawa vitenge na baiskeli nchi nzima. Na hivyo vyote vimetajwa kuwa amevitoa yeye Sa100, na vimeandikwa jina lake.

Hivi tunahitaji ushahidi gani zaidi ya huu, kuwa Sa100 amegawa rushwa ili kuwashawishi wapiga kura?

Kama kweli tuna tume ya uchaguzi huru, na siyo tume yake Sa100, ichukue hatua mara moja, ndipo tuamini kuwa ni tume huru.

TAKUKURU, kama kweli ni taasisi huru inayoshughulika dhidi ya rushwa, ni lini ilikemea au kuchukua hatua dhidi ya rushwa hii iliyo wazi kabisa?

Chama changu cha kale, pale kilipokuwa chama cha kutetea haki, wakati ule ambao mtu hata akidhulumiwa haki yake, alikuwa akisema, "naenda ofisi ya chama wanisaidie", kama watakubali kweli Sa100 awe mgombea kupitia chama chao, huku wanajua wazi kabisa kuwa amekiuka taratibu, sheria, kanuni, na katiba zote, ya chama na ya nchi, kitakuwa kimejipaka uchafu ambao kamwe hautakuja kufutika. Na wananchi wapiga kura, kama tutaletewa mgombea ambaye ni dhahiri ametoa rushwa, ameshindwa kuheshimu katiba ya chama chake, sheria na katiba ya nchi, basi huyo mgombea tuwaachie watu wa chama chake haramu, sisi tusijitie unajisi huo. Iwe ni marufuku kabisa mtu mwema, mzalendo wa kweli, kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye mchakato uliojaa unajisi.
 
Kodi zetu zinachezewa saaana. Ifika mahala watanganyika tuone uchungu wa kodi zetu
 
Back
Top Bottom