Zanzibar 2020 Tume ya Uchaguzi Zanzibar: Kura ya mapema (Oktoba 27) haitahusisha Askari wote

Zanzibar 2020 Tume ya Uchaguzi Zanzibar: Kura ya mapema (Oktoba 27) haitahusisha Askari wote

Acha kuingiza udini katika masula haya. Nini mlengo wako. Usitumie usilamu kuhalalisha upumbavu wako uliokujaa mwilini. Uislamu sio dini ya kufanya Mambo ya kijinga.

Wapumbavu ni nyie mnaowaza dhulma ili mpate madaraka na mali kupitia madaraka .
Mkijenga taifa la kujali vyeo badala ya utu ,haki na upendo msitegemee kuwa mtaweza kuwajenga vijana waamini katika kutafuta mali kwa halali ,matokeo yake ni kila mtu kuwaza dhulma ,wizi ,ujambazi na ushirikina na udanganyifu wa kila aina.

Mnafanya mambo ambayo hata shetani anawashangaa.
Hivi wewe unaona ni sahihi Kupiga kura siku mbeli kwenye Kale ka nchi ka Zanzibar?
Hivi kwa nini mnapenda sana madaraka ya dhulma?

Acheni hizo ! Mnawaumiza watu kwa sababu ya kujinufaisha ,mmekua kama wafanyabiashara ya utumwa! Walikua hawajali uhai na masiha ya watu bali wao tu kupata!
Waovu wakubwa !!
Damu zote zinazomwagika kwa sababu ya dhulma iwe juu yenu na watoto wenu na wajukuu zenu.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji Mkuu mstaafu Hamid Mahmoud amesema kura ya mapema haitawahusisha wapiganaji wote wa vyombo vya ulinzi ikiwemo majeshi na Polisi, kama inavyodaiwa na watu wanaojaribu kupotosha ukweli na madhumuni ya kura hiyo.

Alisema hayo wakati akizungumza na viongozi wa vyombo vya ulinzi Chake Chake Pemba. Alisema sio wanajeshi wote waliopo Zanzibar na Polisi, watapiga kura hiyo siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

“Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu kura ya mapema, sio askari wote watashiriki katika kura ya mapema ya tarehe 27 Oktoba... kura hiyo ni kwa watu maalumu ikiwemo watumishi wa tume na wasimamizi wa uchaguzi na askari ambao watahusika katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 tu”alisema.

Alisema vipo jumla ya vituo vya kupiga kura 1,412, ambapo watumishi wapatao 7,000 watashiriki katika kura ya mapema Oktoba 27 kwa upande wa Unguja na Pemba.

‘’Hizo ndiyo sababu za kuwepo kwa kura ya mapema. Kati ya vituo vya kupigia kura 1,412 vilivyopo Unguja na Pemba, ni vituo 407 vitatumika kwa ajili ya kupiga kura hiyo siku moja kabla ya kura ya watu wote ya Oktona 28,”alisema.

Alisema tayari tume ya uchaguzi imetoa tangazo kwa vyombo vya ulinzi, kuwasilisha majina ya watu wao ambao watapiga kura ya mapema siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa, kuondoa hofu na wasiwasi kuhusu kura ya mapema, ambapo utaratibu wake upo unafahamika na kusimamiwa na mawakala wote wa vyama vitakavyoshiriki katika uchaguzi.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Faina Idarous alivipongeza vyama vya siasa kwa kufanya kampeni za kistaarabu wakati kampeni zikiwa zimebaki siku 23 kuingia uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

Alisema vyama vya siasa kupitia wagombea wake wote, wamezingatia kanuni na sheria za uchaguzi kufanya kampeni zitakazozingatia amani na utulivu na kuepuka matusi.

Sijaelewa yani vituo 1412 kwa watu 7000.
 
Back
Top Bottom