Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Makamba naye aliyejitangazia ushindi vipi???
 
Magufuli asiapishwe kwa kura za upande mmoja, uchaguzi wote urudiwe chini ya tume huru , sio tumeccm.
 
umefutwa, ni baada ya Maalim Seifu kujitangazia ushindi, bila kufuata utaratibu


hakujitangazia mshindi amesema vile ambavyo alivyozipata zile papers za matokeo ambazo pia observers wote wanazo


aliwaomba tume wamtangaze kwa haraka kuepusha maafa nchini

CCM wanaielekeza Tanzania kwenye ARMAGEDDON
 
MATOKEO YA NEC YANA KASORO NYINGI.!

Jana nilisema nitatoa screnario tano kudhibitisha kuwa matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume si ya kweli na yanafaa kupuuzwa na kila mtu mwenye akili timamu. Licha ya Tume ya uchaguzi kutokua huru lakini imeamua kushirikiana na CCM kupuuza maoni ya watanzania na kuhujumu matokeo ya uchaguzi.

Scenario zifuatazo zinathibitisha hivyo;

1. Jimbo la Tunduma karatasi iliyobandikwa ktk ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi ikiwa na muhuri wa Tume inaonesha Lowassa amepata kura 32,219. Lakini matokeo yaliyotangazwa na Tume yanaonesha Lowassa amepata kura 6,000 tu. This means NEC hawatangazi matokeo wanayopokea kutoka kwny majimbo bali wanatangaza matokeo yao kama wanavyoelekezwa na CCM.

2. Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge. Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.

Niliwahi kusema "CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu". Kiazi kama January ndo anapewa kazi ya kuiba kura za Lowassa unategemea nini? Haiwezekani watu 24,000 waende kituoni kumpigia kura Rais tu halafu wasipige za Mbunge. Utaratibu ulikua watu kupiga kura 3. Sasa iweje waliopiga kura za Urais Bumbuli wawe wengi kuliko waliopiga za Mbunge? Yani mtu alienda kituoni akapewa karatasi ya Rais tu, alipopiga akaondoka bila kupiga ya Mbunge?.

3. Majimbo mengi asilimia za kura zimeonekana kuzidi 100 jambo ambalo linadhihirisha wizi wa waziwazi. Jimbo la Monduli Arusha Lowassa anatajwa kupata kura 49,675 na Magufuli kura 11,335 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (18%).

Jimbo la Arusha Mjini Lowassa anatajwa kupata kura 150,107 na Mgombea wa Chauma amepata kura 551 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (69%). Yani Lowassa amelingana na Hashim Rungwe jimbo la Arusha mjini.

Jimbo la Ndanda ukijumlisha asilimia za wagombea zinakuja 108%. Jimbo la Arusha mjini zinakuja asilimia 182% na majimbo mengine hivyo hivyo. This means waliopewa kazi ya kuiba kura walikosa umakini. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

4. Baadhi ya majimbo idadi ya kura zilizopigwa imezidi idadi ya wapiga kura. Kwa mfano ukijumlisha matokeo ya Jimbo la Makunduchi Zanzibar kwa wagombea wote utapata kura 10,382. Lakini idadi ya kura halali ni 10,352. Yani kura zilikua nyingi kuliko idadi ya wapiga kura. Sasa sijui kama kuna watu walipiga kura mara mbili au vp. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

Hali hiyo pia imejitokeza katika jimbo la Kilindi, jimbo la Bumbuli na majimbo mengine. Hii inapaswa kuingia kwenye kitabu cha records za dunia (Guiness) maana ni maajabu kupata kura nyingi kuzidi idadi ya wapiga kura.

Mwaka 1927 aliyekua Rais wa Liberia Charless King aliingia kwny kitabu cha Guiness baada ya Tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza kuwa ameshinda kwa kura 234,000 wakati idadi ya wapiga kura nchini kwake ilikua 15,000 tu. NEC nao wamefuata nyayo za Charless King. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

5. Kwa mujibu wa NEC jimbo la Bumbuli na Bukoba mjini ndio majimbo yenye watu smart kuliko majimbo yote Tanzania maana ndio majimbo pekee ambalo hakuna hata kura moja iliyoharibika.

Kwa mfano Bumbuli Idadi ya wapiga kura ni watu 44,011 na idadi ya kura halali ni 44,011. Haya ni maajabu mengine ya dunia. Yani ktk watu 40,000 hakuna hata mmoja aliyekosea. These people are very smart.

Ni ajabu jimbo la Makunduchi Zbar lenye wapiga kura 10,000 walioharibu kura ni watu zaidi ya 100 lakini jimbo la Bumbuli lenye wapiga kura zaidi ya 40,000 hakuna hata mmoja aliyeharibu kura. Kama unaelewa Probability utajua huu ni uongo wa kiwango cha PhD. Watu 44,000 are more likely kuharibu kura nyingi kuliko watu 10,000. KaJanuary hakajui hii formular coz kanapenda namba tu lakini hakajui hesabu. Itz shame.

NINI CHANZO CHA YOTE HAYA?

Sababu inayopelekea fraud hii ya kijinga ktk kutangazwa matokeo inasababishwa na Tume kuacha kutangaza matokeo halisi na kuamua kutangaza matokeo wanayopewa na CCM.

Kuna kikosi kazi cha vijana wa CCM wanaofanya tallying na kuwatumia Tume ya Uchaguzi. Kwa hiyo matokeo yanayotoka majimboni hayaendi moja kwa moja Tume, yanapita kwanza kwa vijana wa CCM wanayachezea ndipo yanaenda Tume. Katika kufanya kazi hiyo wanakosa umakini na kukosea hata vitu vidogo kama niliorodhesha hapo.

Licha ya kubadilisha matokeo ya Urais, mbinu nyingine wanaofanya ni kupunguza kura za Lowassa kwa kuongeza kwenye idadi ya kura zilizoharibika. Katika majimbo mengi Lowassa aliyoongoza hata idadi ya kura zilizoharibika ni nyingi.

Hebu jiulize imekuaje jimbo la Arusha mjini watu zaidi ya 5000 waharibu kura? Watu 5000 ni sawa na wakazi wote wa jimbo la Wawi Zanzibar. So ni sawa na kusema jimbo lote la Wawi wameharibu kura. Impossible.!

Mbinu nyingine ni kupunguza kura za Lowassa na kuwaongezea wagombea wa vyama vidogo. Kwa mfano jimbo la Moshi mjini mgombea wa ADC alipata kuta 11 jimbo zima. Na fomu ya matokeo iliyobandikwa ofisi ya Mkurugenzi inaonesha hivyo. Lakini kwenye matokeo yaliyotangazwa na Tume inaonekana amepata kura 186. Ongezeko la kura 175. Ujinga huu wameufanya ktk majimbo mengi.

WAY FOWARD.

Sisi tumefanya tallying ya majimbo yote ya nchi nzima na tunayo matokeo halisi kama yalivyosainiwa na mawakala wa vyama vyote. Matokeo hayo yanaonesha maoni halisi ya watanzania.

Viongozi wa chama wanakutana leo na muda si mrefu watatoa tamko. Rais wa Tanzania anachaguliwa na Watanzana, ni vizuri kuheshimu maamuzi yao.!
 
wanasheria tupeni ufafanuzi juu ya hili tukio la kuftwa uchaguz zanzibar je haku athiri uchaguzi wa bara? je matokeo ya rais wa Jamhuri yataendelea kutangazwa?
 
Hiki ni kichekesho, aibu kwa Taifa na ubakaji wa Demokrasia,
ZEC inasema uchaguzi haukuwa huru na haki ,eti taratibu nyingi zilikiukwa wakati wao ndo walikuwa na jukumu la kuhakikisha taratibu hazikiukwi,ukitake into mind serikali ni ya Chama tawala yenye jukumu la kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki.

Halafu suala la Maalim Seif kijitangaza mshindi ,kwa nini asichukuliwe hatua za kisheria kuliko kufuta uchaguzi uliogharimu millions of money za walipa kodi.

Shame on you .
 
Usikurupuke seif alitangaza kura alizopata na zile ambazo shein amepata hakusema yy ndo mshindi.
 
Kwa hiyo kura zote za urais wa JMT kutoka Zanzibar zimefutwa?

I hope so. Kwa kuwa kura za Zanzibar zimepatikana sambamba na kura za Muungano, basi kura za Muungano zilizotoka Zanzibar ni batili na inatakiwa zifutwe.
 
kwani ZEC ni mahakama? je, ni nani aliyelalamika kwamba uchaguzi umegubikwa na dosari? inawezekana DOSARI ni UWEZO MDOGO WA ZEC KUSHINDWA KUCHAKACHUA MATOKEO. ngoja NEC wamalize kuchakachua huku bara halafu waende kuchakachua kule zanzibar. naona ZEC wanataka kutuletea machafuko yasiyokuwa ya lazima. haiwezekani matokeo ya urais yakataliwe wakati matokeo ya ubunge, uwakilishi, udiwani na usheha yakubaliwe.

Mkuu hata nec hawawezi kuchakachua ukiangalia jimbo la liwale, waliojiandikisha wote wamepiga kura na hakuna kura iliyoharibika ni magufuli ni magufuli
 
Bara nao ufutwe maana Zanzibar walipiga kura na Rais wa Muungano
Zote zifutwe
 
Yaaani kurudia Uchaguxi ni gharama kubwa... nini kilichofanya uchaguzi ufutwe?? Watu wamepiha Kura halafu uchaguzi unafutwa kwa sababu ipi???? Seriakali ya nchi maskini kama Tanzania inaweza kumudu gharama ya kurudia uchaguzi kuliko kutangaza matokeo ya kweli... This is really sad, the competence of ZEC as well as NEC is highly in doubt, The exercise of true democracy is very low in developing countries like Tanzania,
 
Hizo facts zako hazina mashiko magufuli anaongoza vizuri bila ya shaka na lowassa amekubali hilo
 
ZEC mamlaka yake ni huko huko mchambawima.

Na majimbo yote ya huko yashatangazwa
 
Back
Top Bottom