Zanzibar Electoral Commission (ZEC), hivi punde, imeyafuta matokeo yote ya Urais ya Visiwani Zanzibar katika kile kilichosemwa kuwa yalikuwa na kasoro nyingi. ZEC imeahidi kutangaza tarehe nyingine ya kufanyika upya kwa uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar.
Hata huku Tanzania Bara, katika Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna manung'uniko mengi juu ya matokeo yanayoendelea kutangazwa na National Electoral Commission (NEC). Vipi napo hatua kama ya Zanzibar ikachukuliwa kumaliza fukuto lililopo?
ZEC imeonesha njia. NEC mko wapi nanyi mfanye jambo? Tanzania inapaswa kuwa moja: ya amani, utulivu na mshikamano. Mambo ya uchaguzi, kuyarudia, si mambo mageni. Ni mambo yetu na kwa mustakabali wetu kama Taifa la Tanzania. NEC, chukueni hatua!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam