Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Hiyo barua/Tangazo la ZEC kutokuwa na Tarehe wa Kumbukumbu No. Tafsiri yake ni nini?!... Je tume wameandika wenyewe au wameshurutishwa kuandika hvyo?!...
 
Ndugu zangu ningependa kufahamu kisheria je ni NEC au ZEC inayosimamia upigaji kura Zanzibar kwa rais wa muungano sababu Zec imeshatengua matokeo ya urais wa Zanzibar je vipi kuhusu kura za rais wa muungano iwapo Zec pia ndio wasimamizi?
huku hayafutwi mwendo mdundo na kesho raisi atatangazwa mapema kabisa sawa sawa
 
ilo Tangazo la mwenyekiti wa tume mbona lina mstari kwenye wa kukata/limekuwa'cancelled'? Limeandaliw lingine nini?
 
Wangeshinda wao usingefutwa, ila kwavile ni mpizani, basi taratibu hazikufwatwa. Nchi ya wahuni. Sasa matokeo ya urais wa Jamhuri huku bara yakuwaje? Basi nayo yafutwe
 
hawakutafuta ushauri wa kisheria,halafu zile kura za magufuli na lowasa zinazotoka zanzibar itakuwaje?
 
Kuna mtu alitaahadharisha kuwa kuna jamaa fulani anataka kujiongezea muda tukabisha...!
 
JIFUNZE KWA UNDANI KIDOGO KIONGOZI, USIWE MVIVU WA KUFIKIRI NA HUKU MUNGU AMEKUPA AKIRI


tume-nec futeni matokeo ya urais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania.

Simple logic

kama tume ya kule zanzibar-zec inakiri kuwa uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi,
means hata matokeo ya ya urais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania inabidi yafutwe pia

kwa sababu

1. Kati ya lowassa/magufuli mmoja wao angekuwa rasi wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambapo ndani ya kula ambazo wangepata zipo kura za kule zanzibar, hivyo kama zec imefuta matokeo kule means hata kura za urasi za jamuhuri ya muungano wa tanzania zifutwe pia.

2. Mpigaji kura wa zanzibar alipewa kura tano (watu wa kuwachagua), zikiwemo za rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, hivyo alipiga kura tano, hivyo ni ngumu kusema kuwa hizo kasoro zilimuathiri shein na maalimu seifu tuna siyo kura za raisi wa jamuhuri ya muuungano wa tanzania ( lowasa na magufuli)

tume ifute huu uchaguzi kwa kura za uraisi

kuendelea kulazimisha hiii ni kupoteza muda na pesa bure kabisa, na huenda machafuko yakazuka,

kasoro za wazi ziko nyingi sana
bumbuli-tanga idadi ya wapiga kura wote ni tofauti na kula zote zinazoonekana katika ubunge na urais.

Lakini pia kuna sehemu nyingi sana asilimia za matokeo hazimatch na
100% ya kura zote

poleni nec-mmeponzwa na marombe jr... Poleni, na mkicheza mnaliingiza taifa katika machafuko.

Na kama hela hawana waombe msaada na pia kama wanajua wametenda haki wafute matokeo turudie uchaguzi
 
Maswali ya kijinga. Uchaguzi wa JMT husimamiwa na NEC; wa Zanzibar na ZEC. ZEC ndio waliofuta uchaguzi waliousimamia.

Sijui kwa nini umenijibu kwa jazba. Nilitaka kupata ufafanuzi kuwa kama mchakato ulikuwa sio halali na matokeo yote yanafutwa.

Vipi kuhusu kura za Magufuli na Lowassa zilizopatikana kwenye mchakato usio halali nazo zimefutwa?

Kama huna unachojua bora ukae kimya tu!
 
Katika hali ya kushtua Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC) imetangaza kuyafuta Matokeo ya urais wa Zanzibar.

Yadaiwa Uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.

Imeahidi kutangaza tarehe rasmi ya kurudiwa uchaguzi.

====
Statement:

vU05dG9.jpg

EdIidYV.jpg

BLhdlD9.jpg


VIDEO:

Chanzo: ZBC TV


Wamepanic wakakurupuka na sasa wameshajikanyaga kilichobaki tutaona vikumbo vyenye mshindo mzito saaana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom