Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Wafute kwenye vituo vilivyo na ushahidi wa kuwepo kasoro kubwakubwa tu sio nchi nzima. Hiv ccm kwanini mnataka kumwaga damu za watu wasio na hatiya?
 
Wakuu.
Hapa kilichofanyika ni kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na sii wa muungano.
Hii ni kwa majibu wa mmoja wa wanasheria niliyempigia simu na kumuuliza.
So uchaguzi wa Zanzibar (serikali) ya mapinduzi hauhathiri matokeo ya kura za muungano.
 
Hapo ndio matatizo. najua huu ni mpango mzima wa Kikwete na Shein kutaka kuendelea kubakia madarakani! watanzania hatulikubali hilo
 
wana jf ninaiyona rasimu ya katiba ya warioba ikirejea taratibu ccm walikwepa mambo mengi leo rais kikwete mambo yanakudodea kwa mara ya kwanza tangu tupate uhuru matokeo ya urais zanzibar yanafutwa kweli unatuacha na historia kubwa ila kwa rais ajae nafuu yake ni kurejea rasimu ya warioba la sivyo nae ataondoka kwa aibu
 
Mipango ya shetani inaelekea kufeli, na Magufuli awe muungwana tu, wanamlazimisha aongoze hii Nchi lkn naamini hata akifanikiwa kuapishwa atakuwa na wakati mgumu kuliko tunavyodhani, naona kabisa hii Nchi ikirudi nyuma zaidi ya hapa tulipo.
 
Maswali ya kujiuliza hivi itaundwa Tume nyingine maaana kama hata wajumbe wanakamatana mashati hataelewana kamwe.
 
kwa hiyo na zile kura za urais zilizo pigiwa raisi wa wa muungano na wananchi wa zanzibar inabidi zifutwe
 
Zilizofutwa ni Matokeo Ya Urais na Sio Ya Wabunge, madiwani wala Wawakilishi. Kwa hiyo Kura za Ubunge ziko pale pale
 
Kujitangza kisheria no kosa mwny/kiti amefanya vema

Mkuu hebu shirikisha akiri yako wkt unachangia usitumie tu hilo kalio. Kwahiyo kwaupeo wako uchaguzi ukirudiwa akajitangaza tena utafutwa tena?

Kamahujui kitu siyolazima uchangie, nivema ukanyamaza wanaojua wachangie nawewe utaambulia anglau ma2 ma3.
 
Nadhani hili halina ubishi kwani wasimamizi wa uchaguzi wa muungano ni kwa upande wa Zanzibar ni ZEC, hivyo kama kulikuwa na maroroso, basi yataathiri pande zote.

Ila sijui kama busara inamashiko kwamba kama mgombea wa chama X kamshinda mgombea wa chama Y kwa kura ziadi ya idadi ya wapiga kura wa Zanzibar, basi aweze kutangazwa mshindi bila kujali kura za Zenj. HILI LINAWEZA KUZUA MGOGORO WA KIKATIBA
 
Wakuu.
Hapa kilichofanyika ni kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na sii wa muungano.
Hii ni kwa majibu wa mmoja wa wanasheria niliyempigia simu na kumuuliza.
So uchaguzi wa Zanzibar (serikali) ya mapinduzi hauhathiri matokeo ya kura za muungano.
...... .....
.

hhahaha kilaza kwahiyo huyu raisi wa wa bara atakuwa wa Tanganyika peke yake
 
Uchaguzi urudiwe tena chini ya tume huru sio chini ya tumeccm, mahakamaccm na polisiccm.
 
Sheria ya kufuta uchaguzi na muda was kurudia katiba inasemaje?

Je waangalizi wa kimataifa kwakua wao ndio watoaji wa pesa zote zinazofanyia uchaguzi sheria zao zikoje?

Sheria ya Tume MTU akijitangaza haisemi kuwa uchaguzi urudiwe Bali kuna adhabu zake ambazo zimeainishwa.
 
JIFUNZE KWA UNDANI KIDOGO KIONGOZI, USIWE MVIVU WA KUFIKIRI NA HUKU MUNGU AMEKUPA AKIRI


tume-nec futeni matokeo ya urais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania.

Simple logic

kama tume ya kule zanzibar-zec inakiri kuwa uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi,
means hata matokeo ya ya urais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania inabidi yafutwe pia

kwa sababu

Mbona kuna mikoa mingi uchaguzi umehairishwa, kwanini USIRUDIWE ZANZIBAR ??? ..Hii ni internal matter ya wana Zanzibar sio swala la kila mtu. Leo hii Ubungo wakitaka kurudia uchaguzi utafutwa na waanze upya, HAUWEZI kusema TANZANIA nzima WARUDIE UCHAGUZI.

Kwani Bara mliona picha ya MAALIM SEIF kwenye karatasi ??? Hili tatizo ni LOCAL jimboni Zanzibar sio TANZANIA nzima.
 
Back
Top Bottom