Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Hiyo barua/Tangazo la ZEC kutokuwa na Tarehe wa Kumbukumbu No. Tafsiri yake ni nini?!... Je tume wameandika wenyewe au wameshurutishwa kuandika hvyo?!...
 
Ndugu zangu ningependa kufahamu kisheria je ni NEC au ZEC inayosimamia upigaji kura Zanzibar kwa rais wa muungano sababu Zec imeshatengua matokeo ya urais wa Zanzibar je vipi kuhusu kura za rais wa muungano iwapo Zec pia ndio wasimamizi?
huku hayafutwi mwendo mdundo na kesho raisi atatangazwa mapema kabisa sawa sawa
 
ilo Tangazo la mwenyekiti wa tume mbona lina mstari kwenye wa kukata/limekuwa'cancelled'? Limeandaliw lingine nini?
 
Wangeshinda wao usingefutwa, ila kwavile ni mpizani, basi taratibu hazikufwatwa. Nchi ya wahuni. Sasa matokeo ya urais wa Jamhuri huku bara yakuwaje? Basi nayo yafutwe
 
hawakutafuta ushauri wa kisheria,halafu zile kura za magufuli na lowasa zinazotoka zanzibar itakuwaje?
 
Kuna mtu alitaahadharisha kuwa kuna jamaa fulani anataka kujiongezea muda tukabisha...!
 

Na kama hela hawana waombe msaada na pia kama wanajua wametenda haki wafute matokeo turudie uchaguzi
 
Maswali ya kijinga. Uchaguzi wa JMT husimamiwa na NEC; wa Zanzibar na ZEC. ZEC ndio waliofuta uchaguzi waliousimamia.

Sijui kwa nini umenijibu kwa jazba. Nilitaka kupata ufafanuzi kuwa kama mchakato ulikuwa sio halali na matokeo yote yanafutwa.

Vipi kuhusu kura za Magufuli na Lowassa zilizopatikana kwenye mchakato usio halali nazo zimefutwa?

Kama huna unachojua bora ukae kimya tu!
 

Wamepanic wakakurupuka na sasa wameshajikanyaga kilichobaki tutaona vikumbo vyenye mshindo mzito saaana
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…