Vipi matokeo ya Rais wa Muungano kutoka Zanzibar ambayo ZEC imekuwa inaipa NEC iyatangaze, na ZEC imerudi kusema kuwa ni batili? Je, ni halali NEC kutangaza matokeo ambayo anayeyatoa ameshasema ni batili? Hebu tufafanulie maoni yako hapo...Hivyo uchaguzi wa Raisi wa muungano na wabunge wa muungano uliofanyika zanzibar kwangu mimi nauona ulifanyika vizuri chini ya usimamizi wa Jaji Lubuva.Zoezi la kutangaza matokeo liendelee.Ya ZEC wabaki nayo ZEC wenyewe
ni hao hao, ila matatizo yako kwenye karatasi zilizopigiwa kura za wakina Raisi wa ZNZ na Wawakilishi, Matokeo ya Bara yanasimama.
Ahsante, sasa soma tena nilichokiandika halafu jaribu kutoa jibu/majawabu tena !
Na kama uwezo wako umeishia hapo katika kuufahamu Muungano pia nashukuru kwa ulichokiandika hapo juu.
Sasa kwanini na bara wasifute matokeo au kwa sababu UKAWA wamezembea kutangaza matokeo yao!!!!
umefutwa, ni baada ya Maalim Seifu kujitangazia ushindi, bila kufuata utaratibu
Aisee! Ina maana uchaguzi wa Zazibar ulikuwa unaratibiwa na tume mbili tofauti, yaani ndani ya chumba cha kura kulikuwa na wajumbe wa NEC na wa ZEC na kila mmoja alikuwa anatupa jicho kwenye sanduku la kura linalomuhusu? Naona leo wengi mtalala na viatu, maana hamtaki matokeo ya ZEC lakini ya NEC mnayataka!Mkuu yaliyofutwa ni ya Zanzibar na sii ya muungano.
Ya muungano yanasimamiwa na NEC mkuu so NEC ndio wangetangaza kufuta.
Tanzania tuifanye nchi ya amani jamani!
Mbona mwkt hajafuta pia tanganyika ambako baadhi sehemu kuligubikwa na kasoro nyingi?
Huu ni ujumbe tosha kwa wale woote walio na fikra ya kwamba CCM itafanya mabadiliko. MAALIM Seif kama mgombea ana face media anaeleza position yake juu ya kinachoendelea. Lowasa nae pia. Yuko wapi Shein na Magufuli?
CCM ndiyo ile ile. Nchi itaendelea kuongozwa kwa remote tu kutoka Msasani na Masaki
Acha uwongo wako, matokeo yaliyotangazwa na Tume ni Mbeya Tunduma
Ccm 19446 37.28%
Ukawa 32219 61.76%
Na bumbuli sio kama unavyosema. pitia humu JF kuna uzi wa updates za matokeo linganisha hayo unayoyasema na yaliyomo
nilikuwa nasema ile mahakama ya icc inawaonea waafrika lakini leo nimeamini kwamba ile mahakama ni kwa ajili yetu na inatuhusu kabisa.