NEC sio ZEC..
Mwenyekiti wa ZEC amesema uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi, hivyo kwa mamlaka
aliyokuwa nayo amefuta matokeo yote ya uchaguzi Zanzibar. Uchaguzi kurudiwa tena.
Taarifa zaidi zinafuata
maalim seiph angejua angekaa kimya tu!sasa mdomo wake umemponza!shein alishakubali kushindwa
sasa ndo wataumia zaidi katika hii raundi ya pili.
Leo mpatanishi wa mataifa mengine yamemfika shingoni.
sijui ni nani atayemuokoa na hili dubwana linalo mnyemelea.
Wakuu.
Kwa niaba ya wapenda demokrasia namuomba mwanasheria msomi Tundu Lissu na Kibatala Peter wajitokeze kutoa ufafanuzi wa uhai wa kura za muungano baada ya ZEC kufuta uchaguzi visiwani
Technically ukifuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar ina maana umefuta na kura za raisi wa muungano. Kwa maana hiyo hata uchaguzi na matokeo bara ni batili.NEC sio ZEC..
Nadhani hili halina ubishi kwani wasimamizi wa uchaguzi wa muungano ni kwa upande wa Zanzibar ni ZEC, hivyo kama kulikuwa na maroroso, basi yataathiri pande zote.
Ila sijui kama busara inamashiko kwamba kama mgombea wa chama X kamshinda mgombea wa chama Y kwa kura ziadi ya idadi ya wapiga kura wa Zanzibar, basi aweze kutangazwa mshindi bila kujali kura za Zenj. HILI LINAWEZA KUZUA MGOGORO WA KIKATIBA
. . . . . . . Tulia usome taarifa za watu.
ZEC wanasimamia chaguzi 2 kati ya 5 wanazopiga Wazanzibari. Zile chaguzi 3 zinazosimamiwa na NEC zitaendelea kutangazwa matokeo yake.
Unguja CUF wameshinda majimbo 10 ZEC wameyapunguza na kubaki 8 bado kura za wizi hazijatosha ni upuuzi mtupu kurudia uchaguzi wameshindwa watoke
Kama wamesema Zanzibar uchaguzi haukuwa huru na haki,na.watu waliopiga kura kwa wawakilishi na rais wa zanzibar ndio haohao na katika vutuo hivyohivyo basi hata kura za mgombea urais wa jamuhuri na za.wabunge hazikuendeshwa kwa njia ya uhuru na haki.
Naomba kuuliza je kura za urais za Lowassa na Magufuli nazo zimefutwa?
kura za urais wa jamhuri ya muungano zinasimamiwa na NEC si ZEC
Tulianza na Mungu hakika.Nasubiri tamko la wanasheria wetu wasomi waliotukuka.
Ila wasicheleweshe,watoe tamko kabla ya majimbo kuisha kutangazwa.
Technically ukifuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar ina maana umefuta na kura za raisi wa muungano. Kwa maana hiyo hata uchaguzi na matokeo bara ni batili.
'Namuona' Kagame akicheka kimoyomoyo juu ya Demokrasia ya Tanzania...!