Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

NEC sio ZEC..

Wewe usiwe kiazi.. Wapigakura ni walewale na vituo ni vilevile!! Kama haki na taratibu zilikiukwa kwa Wazanzibar wakati wa zoezi la kupiga kura huwezi ukasema kwa kura za Muungano zilikuwa sahihi na kura za Zanzibar zilikuwa na kasoro!!!

Labda walazimishe tu lakini kwa lugha laini na isiyo na mazonge CCM wamekurupuka kushinikiza NEC ifute uchaguzi Zanzibar
 
Mwenyekiti wa ZEC amesema uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi, hivyo kwa mamlaka
aliyokuwa nayo amefuta matokeo yote ya uchaguzi Zanzibar. Uchaguzi kurudiwa tena.
Taarifa zaidi zinafuata

Ukirudiwa ndio wataambulia patupu
 
Tulianza na Mungu hakika.Nasubiri tamko la wanasheria wetu wasomi waliotukuka.
Ila wasicheleweshe,watoe tamko kabla ya majimbo kuisha kutangazwa.
 
sasa ndo wataumia zaidi katika hii raundi ya pili.
Leo mpatanishi wa mataifa mengine yamemfika shingoni.
sijui ni nani atayemuokoa na hili dubwana linalo mnyemelea.

Wanataka kuyazuia mafuriko kwa kifua?😆
 
theluthi mbili inatakiwa ipatikane kutoka upande wa zanzibar kama nitakuwa nimekosea mnisahihishe kwa mujibu wa katiba ya jmt
 
Wakuu.

Kwa niaba ya wapenda demokrasia namuomba mwanasheria msomi Tundu Lissu na Kibatala Peter wajitokeze kutoa ufafanuzi wa uhai wa kura za muungano baada ya ZEC kufuta uchaguzi visiwani

Tundu Lisu mtoe tafadhali.Sio mwanasheria wa kuaminika.Huyo akiwa mwanasheria alisema Lowasa Fisadi halafu akiwa mwanasheria hivyo hivyo akageuka kusema Lowasa SIO fisadi!!!!! He is an unrealiable advocate!!! Usitafute ushauri kwa Tundu LISSU.Mimi hata akijibu hata kumsikiliza sitasikiliza na hata akiandika siwezi soma alichoandika ni Mwanasheria kinyonga Tundu Lissu.
 
Nadhani hili halina ubishi kwani wasimamizi wa uchaguzi wa muungano ni kwa upande wa Zanzibar ni ZEC, hivyo kama kulikuwa na maroroso, basi yataathiri pande zote.

Ila sijui kama busara inamashiko kwamba kama mgombea wa chama X kamshinda mgombea wa chama Y kwa kura ziadi ya idadi ya wapiga kura wa Zanzibar, basi aweze kutangazwa mshindi bila kujali kura za Zenj. HILI LINAWEZA KUZUA MGOGORO WA KIKATIBA

Kikatiba, rais wa Muungano atapatikana baada ya kupigwa kura Bara na Visiwani.

Hata kama Mgombea X atakuwa anaongoza kwa kura mil 2, kiasi ambacho hakifikiwi tena na kura zote za Visiwani, hawezi kutangazwa kuwa raisi kama kura za Visiwani zitakuwa hazijapigwa au uchaguzi umefutwa.

Nimesikia watu wengi wamesema watakayo lakini ukisoma statement ya ZEC inasema UCHAGUZI haukuwa wa haki na huru na sio KURA za uraisi wa Zanzibar.

Sasa tafsiri maana ya Uchaguzi.
 
Unguja CUF wameshinda majimbo 10 ZEC wameyapunguza na kubaki 8 bado kura za wizi hazijatosha ni upuuzi mtupu kurudia uchaguzi wameshindwa watoke

walidhani wakipunguza majimbo na kura zitapungua. wapuuzi wakubwa!
 
Kama wamesema Zanzibar uchaguzi haukuwa huru na haki,na.watu waliopiga kura kwa wawakilishi na rais wa zanzibar ndio haohao na katika vutuo hivyohivyo basi hata kura za mgombea urais wa jamuhuri na za.wabunge hazikuendeshwa kwa njia ya uhuru na haki.

Yaani Mkuu Hata Mi Nilikuwa Najiuliza Swali Hilo Hilo!!! Kisheria Na Kikanuni Imekaaje!!!!??? Kama Uchaguzi Ni Batili, Na Matokeo Yake Kufutwa!!! Je, Uhalali Wake UKOJE, Kwa Upande Wa Kura Za Rais Wa Muungano, Zile Zitokazo Visiwani Huko!!!!!!!!??
 
Naomba kuuliza je kura za urais za Lowassa na Magufuli nazo zimefutwa?

Kuna mjinga mmoja anaitwa January Makamba anasema uchaguzi wa raisi wa Muungano husimamiwa na tume ya huku bara. NEC haijaona kama kuna tatizo huko Zenj.
 
Napata mashaka kuwa Zanzibar walikuwa slow, nahisi kulikua pia na kitengo cha IT kule ambacho kimefanya kazi na kufanikiwa moja ya malengo yake! Kushinda au kuvuruga matokeo halisi maana mwenyekiti kasema hii ishu imekithiri Pemba.
Na jinsi nionavyo, ndivyo walivyotaka kufanya na hapa bara ila Kova alikuwa fasta, ni pia bado ni mpango wao wakatae matokeo ila ni tooo late.
Hii sasa si habari njema ya uchaguzi kufutwa.
 
kura za urais wa jamhuri ya muungano zinasimamiwa na NEC si ZEC

Tulianza na Mungu hakika.Nasubiri tamko la wanasheria wetu wasomi waliotukuka.
Ila wasicheleweshe,watoe tamko kabla ya majimbo kuisha kutangazwa.

ZEC ni kwa Rais wa Zanzibar na Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Baraza la WAwakilishi huko Zanzibar...according to the Act below:

attachment.php
 
Technically ukifuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar ina maana umefuta na kura za raisi wa muungano. Kwa maana hiyo hata uchaguzi na matokeo bara ni batili.

Hii nayo point!
Ebu wenye ufahamu watueleze!
 
lubuva muda huu anasema hayo ya huko zanzibar eti hayawezi athiri matokeo ya urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania??

Sasa kura za uraisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa zile kura za zanzibar zilizofutwa na zec itakuwaje bado ni kura halali??? Kura zitakuwaje halali wakati zec wamesema kulikuwa na dosari zinzoonyesha hata fomu za matokeo kufutwa futwa??

Kama si halali utampataje rais bila kura za zinzibar????


Nchi inakwenda vitani
 
Mi nimejiuliza saana..kwanini chama kinapata kura 0. Hili nimeliona sana kwenye matokeo ya Pemba. hiki ni kitu kisichowezekana kwa akili ya kawaida.yaani chama kichukiwe kiasi kikose hata kura ya wakala ?
 
Back
Top Bottom