Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

 
Hii hpa
 

Attachments

  • 1446040576334.jpg
    20 KB · Views: 50

kwakuwa umeamua kutotaka kuelewa sina namana ya kukulazimisha......
 
UKURUNZINZA upo kila mahali aisee, tunajifanya kuwashangaa majirani wakiwanyima wananchi wao haki ya kuwa na viongozi wanaowataka kumbe hata sisi tuna style yetu ya kufanya hivyo, Shame on us
 
Nilitaka kushangaa hizi Kura maelfu alizopata lowassa pemba.hawa wapemba hawa
 
Ni KOSA kisheria... Jaji Lubuva kuendelea KUTOA MATOKEO...wakati ZANZIBAR wamefuta matokeo yote.. NA MATOKEO YALIOLETWA NA ZEC HUKU PIA NI BATILI... HIVYO NEC haina UHALALI KISHERIA KUTANGAZA MATOKEO...!!!

Ukawa, NENDENI MAHAKAMANI kuishtaki NEC haraka sana...!!! Fanyeni haraka sana sanaaaa...!!!

NEC ni CCM 100%...Matokeo yamepikwa na kuchakachuliwa sana sanaaaaa...!!!!

UKAWA... kataeni MATOKEO YA NEC... haraka... haraka...!!! Ni batili...!!!😨😨😨
 
CCM haiwezi kutoka madarakani kwa makaratasi.

Lazima tunyooshane ndo tupate akili.
 
Kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, napenda niseme yafuatayo nikiwa ni mmoja wa Wazanzibari tuliodhulumiwa haki yetu kubwa ya kibinadamu; haki ya kuchagua kiongozi tunayemtaka na kuheshimiwa maamuzi yetu:

Naomba mambo yafuatayo yazingatiwe:
1. Mwenyekiti wa tume ametoa tangazo hilo nje ya kituo cha kutangazia matokeo ya uchaguzi.
2. Aliyoyasoma hakuyaandika yeye mwenyewe na ndiyo maana alikuwa anajikwaa matamshi mara kwa mara.
3. Inaonesha alitoa taarifa hiyo chini ya amri ya mtu fulani na si kwa maamuzi yake.
4. Ili uchaguzi ufutwe ni lazima (a) wajumbe wa tume wakubaliane kuufuta na (b) vyama vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi vishirikishwe na wengi waunge mkono shauri hilo.
5. Hakukuwa na swali hata 1 aliloulizwa juu ya maamuzi yake ili alitolee ufafanuzi maana ameacha maswali mengi kwa watu.
6. Tume iliweka fomu za malalamiko ambazo zilihitajika zijazwe na mawakala katika vituo vya kupigia na kuhesabia kura na hazijazwa malalamiko aliyoyasoma katika taarifa yake ya kufuta uchaguzi.
7. Iwapo kasoro zilitokea Pemba hakukuwa na sababu ya kufuta matokeo ya Zanzibar nzima, maana uchaguzi ungelazimu kurudiwa huko Pemba tu.
8. Iwapo kulikuwa na kasoro kwa nini tume ilitoa matokeo ya majimbo 31, ambayo ni zaidi a nusu ya majimbo yote?
9. Inasemekana baadhi ya makamanda waliopewa kazi maalumu na CCM walifanikiwa kuwapora vyeti vya kuthibitishwa na tume kwa wagombea wa CUF kuwa washindi wa nafasi za Uwakilishi na ubunge mara tu baada ya kukabidhiwa na hao ndio waliofanya kazi ya kufuta na kuandika mara 2 au zaidi zile fomu zilizosainiwa na mawakala katika vituo baada ya kukabidhiwa kwa tume. Na

10. Inakuwaje NEC wapokee matokeo yote kutoka Zanzibar na wayatangaze bila ya kimeme ikiwa uchaguzi wa Zanzibar haukuwa na uhalali?

Baada ya yote hayo, nashauri yafuatayo:
(a) Viongozi wa CUF musikubaliane na kauli ya ZEC kwa sababu haina ridhaa ya wajumbe wa Tume wala hakuna ushirikishwaji wa vya.a vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi.
(b) CUF shirikianeni na waangalizi wa uchaguzi katika kuthibitisha ukweli na uongo wa kauli ya mwenyekiti wa ZEC juu ya mbinu hiyo ya kuwanyima ushindi.
(c) CUF waombeni waangalizi wa uchaguzi waishindikize tume na serikali ya CCM iliyokwisha muda wake wakubaliane na matokeo yaliyo mbele yao.

Nawaomba Wazanzibari wenzangu, iwapo itatokea kurejea kupiga kura kwa mara nyengine tuiangushe CCM zaidi ya mara hii.

Ahsanteni na tuwe pole sote kwa umoja wetu.
 
Sikieni tunapo sema lowasa kashi si kwamba tunaleta siasa ila haki ya mtu na apewe.nahakikisha mtasikia mengi zaidi ya hayo znz si wajinga kufuta matokeo kuna watu mpaka sasa hatujui walipo huko znz.hivyo tuwe wapole kua MUNGU anavyo lekebisha Jambo hili
 
sio kweli KURA za BARA na VISIWANI hazichanganywi, NEC wanasimamia kura za Raisi wa Tanzania, bara na visiwani, huko Zanzibar wamejichanganya wenyewe na kura zao. Sisi huku bara mambo yataendelea kama kawaida.

Lakini mkuu huo uchaguzi umefanyikia wapi??? Si zanzibar??! Kama zec wamesema kura ni batili kwanini wewe unasema ni halali???
 

Kuna watu nchi ni watu wazima lakini akili hazimo kabisa!! na watu hawa utawakuta misikitini na makanisani na tena msitari wa mbele lakini damu iko mikononi mwao!! Ni hatari!!
 
Kwa hiyo matokeo ya Bara yatasubiri au inakuwaje ?Maana kuna kura za Bara kule Zanzibar
La ajabu alilosema Lubuva mchana huu ni kuwa kura za wabunge na rais wa jamuhuri kwa upande wa zanzibar wamezipokea kutoka majimbo yote na hazina kasoro yoyote hivyo zinahesabika ni halali.
Pia kasema kura zilizopigwa ni nyingi kuliko waliojiandikisha.
w
swali. Iweje za jamihuri ziwe sawa lakini za shein na maali ziwe zimezidi. Kivipi wakati walichagua pamoja. Au ndio ulofa huu tulioambiwa watanzania ni malofa.
 

Kura ya jamuhuri ya muungano inasimamiwa na ZEC, na mawakala ni wa Zec, iweje kura za muungano ziwe halali? labda sheria ipindishwe
 
Hakuna katiba ya kibaguzi kama ya Zanzibar. Mtu wa bara ukienda Zanzibar huchagui kiongozi yeyote wa Zanzibar, yaani ni ubaguzi mtupu. Ila wao wakija kwetu wanachagua mpaka viongozi wa mtaa.
Nataka kujua wabara waliopiga kura Zanzibar nao kura zao zifutwe ?
 

You have said it my Brother
 

Sababu za kufuta ichaguzi zimetajwa 9 na sio mbili km unavosema
 
 
Wana jamvi, moja ya sababu zilizopelekea ZEC kughairisha uchaguzi wa Zanzibar ni uchaguzi huo kutokuwa wa huru na haki.
Karibu waangalizi wote wa kimataifa wametoa ripoti zao na kusifu kuwa uchaguzi wa Tanzania umekuwa wa huru na haki.
Swali langu ni je waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wametoa ripoti zao kwa kuangalia hali halisi ya uchaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…