Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Wadau,
Angalieni hilo tamko kwa umma.

Mmeona hiyo barua hapo haina kumbukumbu wala tarehe?

Mwenyekiti aliikurupuka au alilazimishwa kutoa tamko hili?
 
Tatizo wengi wamejifunzia siasa JF. Nicheke mie khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
machafuko utaleta wewe. Hata kama kamzidi kura milioni moja bado rais wa nchi anschaguliwa na wa zanzibar pia.

Yani unataka turudie kupiga kura upya hapa bara? Wewe utakuwa umerogwa.

Kuna irregularities gani zilizotokea kwenye majimbo yote Tanzania bara? Kama hicho ndio unachotaka basi ni wewe na wengine mliokuwa na fikra kama hizo ndio mnaotaka kutuletea vurugu.

Chaguzi nyingi tu za nyuma zilikuwa na majimbo yaliokuwa na utata lakini hata siku moja sijasikia watu kudai kuwa uchaguzi wa nchi nzima urudiwe.

Jamani kubalini mmeshindwa (denial ni kitu kibaya sana). UKAWA-CDM waanze kujipanga kuanzia sasa kushinda 2020.
 
Anaingiza Muungano kwenye matatizo makubwa sana ya Kikatiba! Amekurupuka vibaya sana. Wale washauri wake wamekosea sana!
 
Mkuu Seif ni golikipa hodari.
Kapangua hata goli la mkono zanzibar. Refa katoa red card kwa mchezaji ....pambano linaendelea bado ni kali lakini . CCM wachezaji 9 CUF wachezaji 10! dakika ni za majeruhi.
 
Kujichanganya kote huku mi nadhani Mungu ameamua.
UKOMBOZI NI MUDA HUU.
Watalazimisha sana lakini hawataweza.
 
Kwanza ninpe heko nyingi Maalim kwa kuwabana hawa mafisiem. Kwa vile alijua mchezo wao, basi akawawahi. Hongera sana. Lakini kama nisingeona video clip, hilo tangazo kama lilivyoandikwa ni batili - halina tarehe. Inaonesha jinsi walioliandaa walivyokuwa chini ya shinikizo kubwa sana. Hata uandishi wenyewe si wa kimantiki. Huu ni ushahidi kuwa kauli zilizondaikwa ziliandikwa kwa shinikizo lisilo la kawaida.
 

Kwetu walikuja na kuishia kukaa ndani ya gari na kuchungulia dirishani huku wamefunga vioo (Full AC). Baada ya muda mwangalizi mmoja kashusha kioo akapiga picha kisha waka ondoka.

Nilijiridhisha kuwa, hawana lolote zaidi ya ku-justify ulaji wa posho zao na kufanya utalii.
 
umefutwa, ni baada ya Maalim Seifu kujitangazia ushindi, bila kufuata utaratibu

Katika sababu alizozitoa yeye mwenyekiti hio ya Seif sharif kujitangazia hamna. Na jengine kuwa Seif Sharif hakujitangazia bali alitoa takwimu inayoonyesha kuwa yeye ndie mshindi na akataka tume ya Zec imtangaze mshindi
 
Jecha ametumia utaratibu upi na vifungu vipi vya sheria kufuta uchaguzi?
 

Wewe unafikiri penalty shoot out hii kwamba kama ushakosa penalty mbili na mwenzako kapata nne, kwa hiyo ya mwisho huna haja ya kupiga.

Sheria iko wazi kuwa Rais wa Muungano atatokana na uchaguzi wa Bara na Visiwani. Hata kama asipate kura hata moja visiwani, lakini kura zipigwe ama process iwe valid.

Hiyo logic yako weka upande
 
Hata huku bara matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa nini wawe na haraka ya kutangaza ndani ya wiki moja?

Tanzania ni kubwa kieneo, walau majumuisho ya kura za Urais wa Jamhuri wa Tanzania ungechukua mwezi ili wadau (vyama, tume NEC na wadau wengine) wajiridhishe majumuisho ya vituo 63,000 vinalingana na yale ''matokeo rasmi'' ambayo Mwenyekiti wa NEC anayasoma kuwa ni 'rasmi''

India uchaguzi wa Waziri Mkuu unachukua mwezi mzima kutangaza baada ya kukamilika ili ''kujiridhisha'' Why does India's election take so long? - BBC News . Tanzania tuna tekenolojia duni, vituo zaidi ya 63,000 halafu tunataka kutoa mtokeo ndani ya wiki moja.

Why does India's election take so long?

As India heads towards the eighth phase of its marathon general election on Wednesday, many are asking whether the world's largest democracy deserves such a protracted voting exercise.
For those not up to speed, India's 16th general election for its 543 parliamentary seats is currently being held in nine phases from 7 April to 12 May - at 36 days, it is the longest in the country's history.
The five-phase 2009 vote took about a month - this time there are almost double the stages but the process will not take that much longer Why does India's election take so long? - BBC News
 


Sawa, lakini kura za bara zilishapigwa siku ya Jumapili.

Sasa niambie zilikuwa na hitlafu gani? Kama hazikuwa na hitlafu basi ni halali - tungojee za visiwani sijui watapiga lini tena.


Jamani, hata kama mmepitia shule za kata jaribuni msijidhalilishe hapa kwa mantiki potofu.
 
Ni sawasawa kabisa. Lazima pande zote zihusike. Hivi iwapo upande wa Zanzibar hawajampigia kura hata moja mgombea wa urais wa jamhuri inakuwaje?
 
Hivi hawa wazanzibari wanapopiga kura za raisi na wabunge wa jamhuri wanatumia vikatio vya NEC au ZEC ?
 
Katika sababu alizozitoa yeye mwenyekiti hio ya Seif sharif kujitangazia hamna. Na jengine kuwa Seif Sharif hakujitangazia bali alitoa takwimu inayoonyesha kuwa yeye ndie mshindi na akataka tume ya Zec imtangaze mshindi

Hivi we mwehu .. sababu ya saba hujaiona ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…