Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

sababu namba 3 zec wamesema idadi ya wapiga kura kuzidi wa kwenye daftari. nauliza hao waliozidi hawakupiga kura za wabunge na na rais wa muungano?
 
Kilichotokea zanzibar ni kwamba CCM walikua wamepeleka nguvu zao zote bara kuhakakikisha wanamchakachua lowassa haswa...wakasahau kuchakachua zanzibar. Sasa wameumbuka
 
eti kawe! huyu ni rais wa muungano wa nchi mbili tunamzungumzia. kama zanzibar kuna ubatili tunakuwa na rais wa tanganyika na si muungano.
 
...rais wa JMT hupatikana kwa kura za bara na zenj.....na kama kura za zenj zimefutwa basi rais wa JMT hawezi kupatikana kwa kura za bara pekee....Kama NEC wakilazimisha kumtangaza mshindi bara huku kura za zenj zimefutwa basi huyo rais atakuwa batili...na hili litaleta mgogoro mkubwa wa kikatiba.....maana wazanzibar hawatamkubali rais wa JMT ambaye amepatikana kwa kura batili toka zenj.....

...watawala hawajaona bado msingi wa kufutwa uchaguzi zenj...wakilazimisha kumtangaza rais wa JMT kama NEC wanavyosema basi wanatengeneza mgogoro mkubwa wa kikatiba na zenj....na hili litawagharimu kweli kweli kwa rais watakaemwapisha kwa nguvu.....

....rai yangu ni NEC kusitisha kutangaza mshindi wa urais wa JMT hadi pale zenj watakavyopiga kura....watawala wakilazimisha mambo itakula kwao vibaya hapo baadae...na huyo watakaemtangaza kwa nguvu hatakubaliwa zenj...na hivyo ataanza urais na mgogoro mkubwa wa kikatiba....


..watawala waisome katiba ya JMT waelewe....haya mambo ni zaidi ya wanavyofikiri...maana kama wamewalazimisha ZEC kufuta uchaguzi bila kujua madhara ...basi itakula kwao vibaya....NEC nguvu yao kikatiba inaishia kumtangaza rais tu....lakini jinsi rais alivyopatikana ni issue nyingine ya kikatiba itakayokuwa na msingi baada ya rais kutangazwa...
 
Haipo hivyo wewe! Zanzibar kuna kura za nec na za zec na zote zina waangalizi tofauti! Sema mpiga kura ni yuleyule!
 
Ingawa utata wa kisheria utakuwepo lkn sio kwa hoja hiyo hapo!
 
umefutwa, ni baada ya Maalim Seifu kujitangazia ushindi, bila kufuata utaratibu

Alichofanya ni kutoa hesabu aliyopata baada kujumuisha matokeo ya kura yaliyobandikwa katika kila kituo cha kupigia kura na nakala kutolewa kwa kila wakala ama ilivyoelekezwa na tume. Matokeo hayo siyo siri tena kwa kuwa yako hadharani.
 
hujui kitu wewe waangalizi ni wale wale wa zec,ungekaa kimya tu
 
Haipo hivyo wewe! Zanzibar kuna kura za nec na za zec na zote zina waangalizi tofauti! Sema mpiga kura ni yuleyule!
hujui kitu wewe waangalizi ni wale wale wa zec,ungekaa kimya tu
 
eti kawe! huyu ni rais wa muungano wa nchi mbili tunamzungumzia. kama zanzibar kuna ubatili tunakuwa na rais wa tanganyika na si muungano.

ballot box ni mbili tofauti. kama walikosea kujumlisha matokeo yao au kama kuna wizi kutoka kwa mawakala wao, haitadhuru usimamizi wa kura za tanzania bara kwasababu wasimamizi ni watu tofauti.
 
ballot box ni mbili tofauti. kama walikosea kujumlisha matokeo yao au kama kuna wizi kutoka kwa mawakala wao, haitadhuru usimamizi wa kura za tanzania bara kwasababu wasimamizi ni watu tofauti.

Tuwe wakweli.

Kwa vile Uchaguzi Mkuu Zanzibar ulihusisha Uchaguzi Mkuu wa JMT kwa kufanyikia kituo kimoja, mawakala wakiwa ni wale wale kutoka vyama vya siasa na maofisa wa ZEC wakiwa ni wale wale kwa niaba ya NEC, mapungufu yoyote yenye uzito wa kufuta Uchaguzi huo kwa mujibu wa ZEC yanahusu pia Uchaguzi Mkuu JMT huko Zanzibar.
 

Asante umejileta vizuri sana, sasa swali linarudi kwako, kama umesema hujawahi kusikia uchaguzi unarudiwa nchi nzima hata kama kuna majimbo yenye utata sasa ni kwa nini Zanzibar wanarudia? kwa maelezo yako si ni kwamba wangerekebisha hayo majimbo yenye utata tu?

yani unashangaa la kurudia kupiga kura bara lakini hushangai la uchaguzi wote kufutwa zanzibar???

kweli sa ivi mmedakwa bafuni wakati bao la mkononi ndo linakaribia tu kutoka,au safari hii mlitumia sabuni ya REVOLA ISIYO NA POVU JINGI?
 

Sijui kama ulinielewa. Utata wa upigaji kura uko visiwani, basi warudie huko. Hapa bara uchaguzi haukuwa na matatizo, kwa nini turudie?

ZEC ndiyo iliyofurunda na sio NEC.

NEC ni tume huru. NEC itaikandamizaje UKAWA wakati bosi wa NEC ni shemejie Lowasa (source hapo chini), na NEC imesema bara uchaguzi ulikuwa huru.

Nyie msitubabaishe. Mikakati yenu yote imeumbuliwa hadharani. Tunajua wazi mnachojaribu kukifanya kwa sasa lakini hapa leo mmepwelea. Watu walijua njama zenu na walikuwa wanawafuatilia kwa makini katika kipindi kirefu sana. Tokea mlipokuwa mnaweka mikakati hadi mlivyojiseti kuuharibu huu uchaguzi.

Hebu tembelea hapa chini ujionee mwenyewe ni nani alietaka kufunga bao la mkono, CCM au UKAWA?

The Times of Tanzania | News about Tanzania and beyond
Huu ndio mpango wa Lowassa kuiba kura uliovuja | The Times of Tanzania
 

hayo mambo ya ushemeji na lowasa sijui bla bla mingi ni propaganda hizo tuweke pembeni turudi kwenye hoja.

Miongoni mwa sababu za ZEC walizotoa kufuta matokeo ni kwamba kuna vituo wapiga kura wameonekana wengi kuliko waliojiandikisha kwenye daftari, hii ina maana kwamba kuna uchakachuzi pia basi ulifanyika katika kumchagua rais wa jamhuri kwenye majimbo hayo, swali linakuja kwa NEC ni kwa nini kwa upande wao hizi kura hazijaonekana ni batili? na wakati ZEC wamesema ni batili? wanapojifunga ni kwamba zote yani kura za ZEC na NEC zilipigwa at time, na watu hao hao, vituo hivyo hivyo, so kama za ZEC kwenye vituo hivyo ziliharibika na za NEC pia zinapaswa ziharibike kwa sa babu ndo kura hizo hizo
 

Please, kama hujasoma zile sources nilizokuwekea usije hapa kunipotezea muda.

Sichezi na majizi mimi.

Kasome majarida yote kwanza halafu unitafute. Ninakupa muda wangu lakini wewe sio saizi yangu hata kidogo.

Tusicheezeane hapa.
 

Yani hii hatua ya ZEC imeshatia dosari uchaguzi mzima wa rais wa jamuhuri ya muungano. Lubuva amejaribu tu kuforce maana hataki uchaguzi mkuu muungano ukwame ila ni kwamba kuna mgogoro wa kikatiba hapa. Halafu hatujajiuliza hizo siku 90 za ziada shein atakaa madarakani kwa muujibu wa sheria ipi? Maana kipindi chake alichopewa na wazanzibari kinaisha wiki hii. Sasa ataongoza by presidential decree au?
 
Please, kama hujasoma zile sources nilizokuwekea usije hapa kunipotezea muda.

Sichezi na majizi mimi.

Kasome majarida yote kwanza halafu unitafute. Ninakupa muda wangu lakini wewe sio saizi yangu hata kidogo.

Tusicheezeane hapa.

source zako zitanisaidia nini sasa?
kwani hapa unacheza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…