Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hapo kwenye kuiregard Zenji km kajimbo ka uchaguzi ni matusi makubwa kwa wanavisiwani na ni kebehi kwa washirika wote wa Muungano.
Uchaguzi wote urudiwe si zenj wala Bara, na kiranja wa uchaguzi awe huru!
Hapa ndipo tuone itavyokuwa ni vipi; maana:-
1. Ikiwa ni kweli uchaguzi wa rais wa JMT unasimamiwa na NEC na si ZEC, tuelezwe kulikuwa na daftari tofauti la wapiga kura wa kura za urais wa JMT?
2. Je, kulikuwa na wasimamizi wawili tofauti katika kila kituo na jimbo mmoja kwa ajili ya kura za rais wa JMT na mwingine rais wa SMZ?
3. Je, kulikuwa na vituo tofauti kabisa kwa ajili kupigia kura za rais wa JMT na rais wa SMZ?,
4. Je, kura hizi zilipigwa siku tofauti kwa kura za rais wa JMT siku yake na rais wa SMZ siku yake?
Kama jibu ni HAPANA kwa angalau swali moja katika hayo; ni wazi kwamba "uchaguzi huu na matokeo yake yote" yafutwe (kama nilivyonukuu katika taarifa ya ZEC si mimi)
Katika hali ya kushtua Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC) imetangaza kuyafuta Matokeo ya urais wa Zanzibar.
Yadaiwa Uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.
Imeahidi kutangaza tarehe rasmi ya kurudiwa uchaguzi.
====
Statement:
![]()
![]()
![]()
VIDEO:
Chanzo: ZBC TV
Mfano: Tanzania bara Jimbo la ubungo, unapewa karatasi TATU (Raisi muungano, Mbunge na Diwani) . kwa ZANZIBAR unapewa 4 (Raisi wa Muungano, Raisi wa Zanzibar, Mwakilishi na Diwani) tatizo liko kwenye hizi tatu za mwisho sio ile ya TANZANIA yote!!! TANZANIA BARA Hawana karatasi ya nne ya URAISI ZANZIBAR kwahiyo HAWARUDII.
Yes mkuu ndivyo ilivyokua.Hapa ndipo tuone itavyokuwa ni vipi; maana:-
1. Ikiwa ni kweli uchaguzi wa rais wa JMT unasimamiwa na NEC na si ZEC, tuelezwe kulikuwa na daftari tofauti la wapiga kura wa kura za urais wa JMT?
2. Je, kulikuwa na wasimamizi wawili tofauti katika kila kituo na jimbo mmoja kwa ajili ya kura za rais wa JMT na mwingine rais wa SMZ?
3. Je, kulikuwa na vituo tofauti kabisa kwa ajili kupigia kura za rais wa JMT na rais wa SMZ?,
4. Je, kura hizi zilipigwa siku tofauti kwa kura za rais wa JMT siku yake na rais wa SMZ siku yake?
Kama jibu ni HAPANA kwa angalau swali moja katika hayo; ni wazi kwamba "uchaguzi huu na matokeo yake yote" yafutwe (kama nilivyonukuu katika taarifa ya ZEC si mimi)
Hizi ni tetesi au ukweli? Vituo vya TV na radio vyote mbona kimya kuhusu habari hii?
Zimefutwa Kura Za Urais tu na Sio mengine