Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Mkuu matokeo ysliyofutwa ni ya serikali ya mapinduzi na sii ya muungano.
Tambua kwamba wazanzibar wamechagua rais wa Zanzibar na rais wa muungano.
Na kasoro zipo kwenye uchaguzi wa rais wa Zanzibar na sii rais wa muungano.

Hivi umezisoma lakini sababu za kuhairishwa uchaguzi!!???
Moja wapo ni kwamba idadi ya wapiga kura katika kituo fulani ilikuwa ni ndogo kuliko idadi ya kura zilizopigwa...sasa unadhani kura za rais wa Muungano zitakuwa sahihi??
 
Kama Dr John Pombe Magufuli atapishana na mshindi wa pili kwa idadi ya kura CHINI YA LAKI 5 ambayo ndiyo idadi ya wapiga kura wote wa Zanzibar basi matokeo ya urais wa Muungano yatapaswa kusubiri marudio ya kura Zanzibar, lakini kama MAgufuli amemshinda mshindi wa pili kwa ZAIDI ya kura LAKI 5 basi matokeo yoyote ya Zanzibar hayawezi kuathiri MATOKEO YA URAIS WA MUUNGANO, kwa namna hiyo NSHINDI WA KURA ZA MUUNGANO ATAAPISHWA KAMA KAWAIDA.


Cha pili., NEC sio ZEC, hizi ni tume mbili tofauti, matatizo yaliyowapata ZEC sio matatizo yaliyowapata NEC, hivyo kama upande wa NEC hakukuwa na matatizo yoyote basi uchaguzi wa MUUNGANO KWA UPANDE WA ZANZIBAR UTAENDELEA KUTAMBULIWA, ni ule tu wa SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ndio utakaorudiwa.
Mzee wa kutafasiri katiba ya nchi - asante kwa upeo wako ila kama hujui ni vizuri kubakia kimya usubiri watu wanaojua katiba zote mbili za nchi, Sheria ya NEC na ZEC watujulishe nini impact ya hii kitu.
 
Wazanzibari maskini lini wataachwa kutawaliwa hawana haki kwenye nchi yao hawana haki ya kumchagua kiongozi wamtakaye.
 
Naomba kuuliza je kura za urais za Lowassa na Magufuli nazo zimefutwa?

Ndiyo hapo watueleze ni kwa jinsi gani kura za serikali ya muungano hazikuadhiriwa na hayo matatizo. Matatizo mengi waliyoyataja ndiyo yanatokea Tanzania nzima. Kuna Majimbo Wapiga kura wa Urais inasemekana ni wengi kuliko wa Ubunge.

But all in all Tume inamrushia mpira nani!!? Watueleze ukweli. Uchaguzi ulifanyika kwa amani kuliko wakati wowote wa mfumo wa vyama vingi. Waliokuwa wanajumlisha matokeo na kuyatangaza ni watumishi wa tume. Sasa hao watu kwa nini wasichukuliwe hatua haraka sana .............. naona mashtaka yao is a mountain!!
 
Zanzibar ni nchi, lakini kikatiba ya Muungano, iko CHINI ya mwamvuli wa TANZANIA. ni sawa na Tanganyika (Bara) iko chini ya Mwamvuli wa MUUNGANO. ndio mana Bara hawapigii kura Raisi wa Zanzibar, ila SOTE tunapigia Raisi wa MUUNGANO.

Ahsante, sasa soma tena nilichokiandika halafu jaribu kutoa jibu/majawabu tena !

Na kama uwezo wako umeishia hapo katika kuufahamu Muungano pia nashukuru kwa ulichokiandika hapo juu.
 
Yeye ni nani kuamuru kura irudiwe upya?. Hiyo gharama nani ataibeba?.
 
Na la Raisi Wa jamhuri ya Muungano anayewakilisha pande zote za muungano wakati Wa upande mmoja wa Muungano matokeo yamefutwa
Atakua Raisi Wa Jamuhuri ya TANGANYIKA ??????
 
Hivi akisema "kutofahamiana kwa wajumbe wa tume" ana maana wajumbe wa tume hawakukubaliana na hivyo kupelekea kupigana? Hapa anakiri jitihada kubwa za kuchakachua zilifanyika ila baadhi ya wajumbe wa tume wakakomaa. Hili linadhihirishwa pia na ukweli kwamba wajumbe wa tume waliweka itikadi zao za kisiasa mbele kama alivyoeleza. Kwa kuwa Tume ya Uchaguzi si halali na huru, uchaguzi utakaosimamiwa na tume hiyo hauwezi kuwa halali, huru na wa haki.

Na haya aliyoeleza Mwenyekiti wa ZEC ni mapungufu ya NEC pia. Wakati ZEC ina wawakilishi wa CUF pia,NEC inaundwa na makada wa CCM pekee. Kwa hivyo, hali ni mbaya zaidi kwa upande wa Tanzania bara.

Kuweka record sawa, ZEC imefuta uchaguzi uliofanyika Jumapili na matokeo yake yote. Si matokeo ya urais tu kama mleta taarifa JamiiForums alivyoeleza.
Hii ina maana kuna wanaume walikomaa mpaka zikachapwa, cha kusikitisha aliekua ameshindwa alikua radhi lkn kitengo kikawa kinashinikiza.
 
Kama walibeba kura za Raisi na uko ndo hayo yaliyotokea tufanyaje sasa?
 
hivi anae paswa kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki ni nani?

kama tume ndo wanalia uchaguzi haukua huru na wa haki je vyama vishiriki vya siasa kwenye uchaguzi vitasemaje? teh teh teh teh!

Precisely....eti tume inalalamika
 
ZEC haina mamlaka kwa NEC na NEC hawana mamlaka kwa ZEC, hivyo uchaguzi uliyoahirishwa/ kufutwa ni wa Zanzibar tu , ila matokeo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapo salama

Vp kuhusu kura za urais bara wanazopiga wazinzabar?
 
Tatizo ni je Maalimu na timu yake watakubaliana na uamuzi huo?
 
Huyu Jecha mbona anataka kutuingiza matatizoni jamani?
 
...... .....
.

hhahaha kilaza kwahiyo huyu raisi wa wa bara atakuwa wa Tanganyika peke yake

Tafuta reference kama mwenzako alivyofanya, na sio unamuita kilaza, sasa kwa taarifa yako wewe ndio kilaza, kuahirisha uchaguzi wa Zanzibar siyo kuahirisha uchaguzi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, baki hapo na elimu .... elimu......elimu
 
Na la Raisi Wa jamhuri ya Muungano anayewakilisha pande zote za muungano wakati Wa upande mmoja wa Muungano matokeo yamefutwa
Atakua Raisi Wa Jamuhuri ya TANGANYIKA ??????
Mkuu yaliyofutwa ni ya Zanzibar na sii ya muungano.
Ya muungano yanasimamiwa na NEC mkuu so NEC ndio wangetangaza kufuta.
 
Back
Top Bottom