PostGE2025 Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29 yaongezewa Muda tena hadi Aprili 24, 2026

PostGE2025 Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29 yaongezewa Muda tena hadi Aprili 24, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
IMG_3481.jpeg


Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026.

Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.

Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo.

Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3, 2026.

Hivyo, kufuatia nyongeza ya muda, wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi tofauti na matarajio ya Tume. Hivyo, Tume iliendelea kupokea ushahidi, taarifa na maoni zaidi. Kwa sababu hiyo, Tume haikuweza kukamilisha kazi yake ndani ya muda wa nyongeza uliotolewa na hivyo kulazimika kuomba muda wa ziada ili kukamilisha kazi yake.

Tume inaendelea kuwashukuru wananchi na wadau wote waliotoa ushirikiano kwa Tume wakati wa kufanya uchunguzi, ikiwemo wale waliofika mbele ya Tume kutoa ushahidi, taarifa na maoni, waliopiga simu na kutuma ujumbe, waliotuma ushahidi, taarifa na maoni kwa maandishi na waliowasiliana na Tume kwa njia za mitandao ya kijamii.
​
Pia soma: Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 yaongezewa muda mpaka Aprili 3, 2026
 
View attachment 3568640

Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikguzi, ikiwemo wale waliofika mbele ya Tume kutoa ushahidi, taarifa na maoni, waliopiga simu na kutuma ujumbe, waliotuma ushahidi, taarifa na maoni kwa maandishi na waliowasiliana na Tume kwa njia za mitandao ya kijamii.
​
Pia soma: Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 yaongezewa muda mpaka Aprili 3, 2026

Chumvi itakuwa imekolea sasa wanafanya kazi ya kubalance.
 
Gwaride la Ushindi.

Wanapiga raundi ya mwisho
Ile ya Gwaride la Ushindi
Wanasiga paundi ya tisho
Wawalinde wao Wahindi
Wanazuga mafundisho
Wawapinde wao madingi
Wanakinga yao malisho
Waziibe na shilingi

Jenga jeshi, huna kesi
Hili ni Gwaride la Ushindi
Jenga jeshi, huna kesi
Hili ni gwaride la ushindi

Oooo, ooo, la ushindi
Oooo, oooo, la ushindi

Wanachekea utamu, haijakauka damu
Hivi hawa binadamu? Haijapauka hamu?
Wamejitoa fahamu, wakilewa kwa karamu
Maamuma maamamu, wanauma bila zamu
Wapiga bila awamu, mambo yao ya haramu
Wakishikia hatamu, bila hata ya salamu
Watu hawa Jehanamu, haiwatoshi hukumu
Tutayabeba dawamu , baragumu majukumu

Jenga jeshi, huna kesi
Hili ni Gwaride la Ushindi
Jenga jeshi, huna kesi
Hili ni gwaride la ushindi

Oooo, ooo, la ushindi
Oooo, oooo, la ushindi
 
Mambo mengine ni kujihangaisha tu bila sababu.
Hiyo ripoti kwani inamsaidia nani hasa?

Waseme tu wamemaliza kazi na wamekabidhi ripoti kwa mwenye uhitaji wa ripoti hiyo, basi inatosha.

Kinachojulikana toka mwanzo hiyo Tume iliundwa kwa sababu maalum. Ripoti yao kwa sasa haina uhitaji wowote.

Samia yupo madarakani, na Genge lake wote wamejipanga tayari kuvuna walichopigania na kulazimu kuua waTanzania.

Sasa hiyo ripoti ni ya nini tena!

Samia hawajibiki kwa mTanzania yeyote; mbali ya Genge lililomhakikishia kuendelea kuwepo madarakani.

Hii ripoti haiwahusu Genge wala Samia.

Kwa kuwa Samia hawajibiki kwa waTanzania ambao uwepo wake madarakani hauwahusu; hiyo ripoti inafaida gani kwao.

Ni Samia na Genge lake ndio wanaowawajibisha waTanzania; kwa hiyo hiyo ripoti hata kama inadai kuwajibishwa wahusika wa maovu, ukweli ni kwamba hawawezi kujiwajibisha wenyewe.

Samia apokee ripoti, na awashukuru hao wajasiriamali kwa juhudi zao za uwekezaji katika kazi hiyo; na mambo yaendelee
 
Karata zote za utawala usio halali wa Samia zinazidi kuisha, akubali tu hakuna sarakasi ya Tume yake inayoweza kumuokoa kutoka kitanzi cha kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Ukatili Dhidi ya Binadamu ya ICC The Hague Uholanzi akajitete.

Atumie muda huu kuomba ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali yake haramu Hamza Johari na pia kuomba wakili mkuu wa serikali kuunda jopo atakaloongozana nalo kwenda ICC The Hague kujaribu kujinasua huku tukimtizama akiwa kizimbani mubashara akisomewa mashtaka na timu yake ikijaribu kumuokoa kutoka maovu makuu aliyowatendea waTanzania
 
Back
Top Bottom