PostGE2025 Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29 yaongezewa Muda tena hadi Aprili 24, 2026

PostGE2025 Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29 yaongezewa Muda tena hadi Aprili 24, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Karata zote za utawala usio halali wa Samia zinazidi kuisha, akubali tu hakuna sarakasi ya Tume yake inayoweza kumuokoa kutoka kitanzi cha kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Ukatili Dhidi ya Binadamu ya ICC The Hague Uholanzi akajitete.

Atumie muda huu kuomba ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali yake haramu Hamza Johari na pia kuomba wakili mkuu wa serikali kuunda jopo atakaloongozana nalo kwenda ICC The Hague kujaribu kujinasua huku tukimtizama akiwa kizimbani mubashara akisomewa mashtaka na timu yake ikijaribu kumuokoa kutoka maovu makuu aliyowatendea waTanzania
Hawahangaikii kutokwenda ICC; wanalazimisha kufa na wapinzani wao wakui. Uchunguzi hauwahusu wao bali wapinzani ili kuwaadhibu kabla ya kwenda The Hague!
 
Ikifika April 24 hatutaki kusikia wameongeza muda ni mambo mawili tu yafanyike moja Chande ajiengue na jopo lake waseme wao kazi za lawama hawazitaki maana wanachoenda kukireport ni uongo au mbili waseme hicho hicho walichoambiwa waseme kisha wote wapoteze legacy zao kuanzia yeye muongozaji mpaka wanaomfuata maana kila kitu kipo wazi unaongezaongeza muda wa nini si useme km ilivyo ueleweke ikifika April 24 watasema wameongeza muda mpaka May 15 oya mboni mnatufanya mazuzu hivi?
 
Ukiandika ukweli na aliyekuagiza uuandike akaridhia huwezi kuchukua muda mrefu, ukiona unaongeza muda kila mara, ujue unachoandika unakitunga kiwe ndio ukweli. Larry Madowo wa CCN akichukua ndani ya wiki 2 kuweka ukweli wa matukio yote, hakupata shida maana ndio ulikuwa ukweli.
Wanatengeneza ripoti ya kudanganya halafu wanataka kutushawishi kwa kutudanganya kwamba hawajadanganya! Hayo ndo maajabi.
 
Inasikitisha sana, mtu atumie mabilioni ya kodi za Watanganyika kuandaa mauaji ya Watanganyika halafu atumie mabilioni mengine ya Watanganyika kuunda Tume ya kumsafisha na mauaji hayo, halafu wanatokea mazwazwa Watanganyika kumtetea Mzanzibari huyu.
 
safi sana.
Wapinzani hawana shukrani, ingefanya haraka wangetia kelele kuwa tume ni geresha tu wamepewa cha kuandika na Samia
 
Inasikitisha sana, mtu atumie mabilioni ya kodi za Watanganyika kuandaa mauaji ya Watanganyika halafu atumie mabilioni mengine ya Watanganyika kuunda Tume ya kumsafisha na mauaji hayo, halafu wanatokea mazwazwa Watanganyika kumtetea Mzanzibari huyu.
vipi yale mauaji ya Mkapa kule Zanzibar 2001?
 
Huenda aliyeunda Tume ameikataa ripoti iliyotolewa! Anataka ifanyiwe marekebisho tena ili iendane na matakwa yake!
 
Hii ni project nzuri ya kugawia watu fulani pesa.

Tunajua from the beginning kwamba hakuna namna ambayo taxpayers wa Tanzania watanufaika na matokeo ya kazi ya hiyo tume ya mchongo!

Hizo pesa walizotumia kwenye hiyo tume pamoja na zile zilizoibwa na mashirika ya umma zingeweza tosha kutumika kama subsidy ya mafuta ya petrol wakati huu ; ikiwa njia ya kuwapunguzia wanannchi machungu ya maisha!!!
 
View attachment 3568640

Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026.

Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.

Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo.

Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3, 2026.

Hivyo, kufuatia nyongeza ya muda, wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi tofauti na matarajio ya Tume. Hivyo, Tume iliendelea kupokea ushahidi, taarifa na maoni zaidi. Kwa sababu hiyo, Tume haikuweza kukamilisha kazi yake ndani ya muda wa nyongeza uliotolewa na hivyo kulazimika kuomba muda wa ziada ili kukamilisha kazi yake.

Tume inaendelea kuwashukuru wananchi na wadau wote waliotoa ushirikiano kwa Tume wakati wa kufanya uchunguzi, ikiwemo wale waliofika mbele ya Tume kutoa ushahidi, taarifa na maoni, waliopiga simu na kutuma ujumbe, waliotuma ushahidi, taarifa na maoni kwa maandishi na waliowasiliana na Tume kwa njia za mitandao ya kijamii.
​
Pia soma: Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 yaongezewa muda mpaka Aprili 3, 2026
Sheria ya Tume za Uchunguzi ya Tanzania, Sura ya 32 Toleo Lililorekebishwa 2002, inampa Rais mamlaka ya kuanzisha tume za kuchunguza masuala ya maslahi ya umma, ikiwa ni pamoja na mwenendo wa watumishi wa umma, idara za serikali, na masuala ya rushwa. Sheria hii inaruhusu uteuzi wa makamishna, inaweka taratibu za uchunguzi, inatoa mamlaka ya kuwaita mashahidi, na kwa ujumla hutumika kwa ajili ya kubaini ukweli (fact-finding) badala ya kutoa hukumu.

Vipengele muhimu vya Sheria hii:

1. Kuanzishwa kwa Tume:
Kifungu cha 3 kinampa Rais mamlaka ya kutoa amri ya kuanzisha tume ya uchunguzi kwa hiari yake mwenyewe, kwa ushauri wa Waziri, au kwa kuzingatia kiapo cha mtu yeyote.

2. Wigo wa Uchunguzi:
Unahusisha mwenendo wa watumishi wa umma, mamlaka za serikali za mitaa, ukwepaji kodi, dosari katika mapato ya serikali, na usimamizi wa mashirika ya umma.

3. Mamlaka ya Tume:
Tume ina mamlaka sawa na Mahakama Kuu ya kuwaita mashahidi, kuhitaji nyaraka mbalimbali, na kuwahoji mashahidi chini ya kiapo.

4. Utaratibu wa Kazi:
Mikutano ya tume inaweza kuwa ya wazi au ya siri kulingana na maelekezo ya Rais, na makamishna wanatakiwa kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa.

5. Ripoti na Hatua:
Tume huwasilisha ripoti kwa Rais, ambaye anaweza kuchukua hatua mbalimbali, ikiwemo kutoa fidia, kuagiza kufunguliwa mashitaka ya jinai, pamoja na kuamua kama ripoti hiyo ichapishwe au la.

Kesho tunaenda kupokea ripoti rasmi ya Tume ya Kuchunguza Matukio ya Kabla, Wakati na Baada ya Oktoba 29 chini ya uenyekiti mahiri wa Jaji (Mstaafu) Othman Chande na wajumbe wenzake.
 
Back
Top Bottom