PostGE2025 Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29 yaongezewa Muda tena hadi Aprili 24, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sio tuu tume huru, sio tume halali. Ni upuuzi tuu wa huyo mama.
Ngoja nikukumbushe mfanano wake.

Wakati ule wa vuguvugu la "No Reform, No Election".

Marekebisho yalitakiwa kufanyika kupitia kwenye Bunge.
Bunge halikuvunjwa mwisho wa siku yake...., kulaghai watu kwamba pengine bado kutakuwepo na fursa ya kurekebisha.
Unakumbuka lile Bunge lilivunjwa rasmi lini?

Inawezekana kabisa usione mfanano wa mtindo wa huyu mtu Laghai kabisa katika kuvuruga akili za watu.

Hiyo Ripoti ya hiyo Tume, hata ikitolewa leo na kuilkabidhi kwa aliyeiunda; usitegemee kusikia chochote tena juu yake.

Kuna tume iliyoundwa kuchunguza kifo cha Mzee Ally Mohammed Kibao?. Sijui kama anakumbuka chochote kuhusu hilo jambo.
 
Hivyo, kufuatia nyongeza ya muda, wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi tofauti na matarajio ya Tume. Hivyo, Tume iliendelea kupokea ushahidi, taarifa na maoni zaidi. Kwa sababu hiyo, Tume haikuweza kukamilisha kazi yake ndani ya muda wa nyongeza uliotolewa na hivyo kulazimika kuomba muda wa ziada ili kukamilisha kazi yake.
"...kufuatia nyongeza ya muda wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi...."
 
Wanaona aibu kuitoa kwa sababu nakala lazima ifike kwa watu wenye akili zao, hapo ndipo watavuliwa nguo hadharani.

Ingekuwa anakabidhiwa The butcher pekee ingekuwa imeshatolewa ndani ya mwezi tu.
 
Kura milioni 32 kama wanavyodai walihesabu kwa siku 3 bila internet hilo genge linalotumia pesa za walipa kodi kila siku linaongezewa siku kutunga uongo nani ananufaika na ujinga huo?

Muuaji hawezi kujinusuru hapo.
 
Ukiandika ukweli na aliyekuagiza uuandike akaridhia huwezi kuchukua muda mrefu, ukiona unaongeza muda kila mara, ujue unachoandika unakitunga kiwe ndio ukweli. Larry Madowo wa CCN akichukua ndani ya wiki 2 kuweka ukweli wa matukio yote, hakupata shida maana ndio ulikuwa ukweli.
 
Na hapa ndipo inadhihirika ule usemi kwamba, kusema/kutunga uongo ni kazi ngumu mnoo inabidi uwe very smart na mwenye kumbukumbu haswa. Tofauti kabisa na kusema ukweli. Ukweli unatiririka tu hata uamshwe saa tisa za usiku.
 
View attachment 3568640

Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026.

Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.

Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo.

Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3, 2026.

Hivyo, kufuatia nyongeza ya muda, wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi tofauti na matarajio ya Tume. Hivyo, Tume iliendelea kupokea ushahidi, taarifa na maoni zaidi. Kwa sababu hiyo, Tume haikuweza kukamilisha kazi yake ndani ya muda wa nyongeza uliotolewa na hivyo kulazimika kuomba muda wa ziada ili kukamilisha kazi yake.

Tume inaendelea kuwashukuru wananchi na wadau wote waliotoa ushirikiano kwa Tume wakati wa kufanya uchunguzi, ikiwemo wale waliofika mbele ya Tume kutoa ushahidi, taarifa na maoni, waliopiga simu na kutuma ujumbe, waliotuma ushahidi, taarifa na maoni kwa maandishi na waliowasiliana na Tume kwa njia za mitandao ya kijamii.
​
Pia soma: Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 yaongezewa muda mpaka Aprili 3, 2026
Tume yenyewe ya mama samiah, hamna kitu hapo
 
Karata zote za utawala usio halali wa Samia zinazidi kuisha, akubali tu hakuna sarakasi ya Tume yake inayoweza kumuokoa kutoka kitanzi cha kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Ukatili Dhidi ya Binadamu ya ICC The Hague Uholanzi akajitete.

Atumie muda huu kuomba ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali yake haramu Hamza Johari na pia kuomba wakili mkuu wa serikali kuunda jopo atakaloongozana nalo kwenda ICC The Hague kujaribu kujinasua huku tukimtizama akiwa kizimbani mubashara akisomewa mashtaka na timu yake ikijaribu kumuokoa kutoka maovu makuu aliyowatendea waTanzania
Kwani huu mpango wa kupelekwa ICC bado upo? siyo kwamba ameshinda hii vita?
 
View attachment 3568640

Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026.

Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.

Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo.

Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3, 2026.

Hivyo, kufuatia nyongeza ya muda, wananchi waliendelea kujitokeza kwa wingi tofauti na matarajio ya Tume. Hivyo, Tume iliendelea kupokea ushahidi, taarifa na maoni zaidi. Kwa sababu hiyo, Tume haikuweza kukamilisha kazi yake ndani ya muda wa nyongeza uliotolewa na hivyo kulazimika kuomba muda wa ziada ili kukamilisha kazi yake.

Tume inaendelea kuwashukuru wananchi na wadau wote waliotoa ushirikiano kwa Tume wakati wa kufanya uchunguzi, ikiwemo wale waliofika mbele ya Tume kutoa ushahidi, taarifa na maoni, waliopiga simu na kutuma ujumbe, waliotuma ushahidi, taarifa na maoni kwa maandishi na waliowasiliana na Tume kwa njia za mitandao ya kijamii.
​
Pia soma: Tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025 yaongezewa muda mpaka Aprili 3, 2026
Wasogozeze mpaka mwaka 3500, WATANGANYIKA sio wajinga tena
 
Back
Top Bottom