PostGE2025 Tume ya Uchunguzi yenye lengo la kudogosha mauaji ya watanganyika

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Naam katika ubora wako, uchambuzi makini kabsa, hadhi ya JF ilielekea kupotea mlivyokaa kimya na kuacha mijadala ya kufikirisha ubongo iongozwe na mshamba!
 
Bandiko hili linaweza kuisaidia sana nchi isipotee zaidi ya ilipofika. Mfanano wa Wahutu kuhubiri mauaji na serikali kukaa kimya wakidhani wanawasaidia, na huu wa baadhi ya viongozi wa dini kuhubiri mauaji huku serikali ikikaa kimya wakidhani wanawasaidia unatisha sana.

Ajabu ukisoma historia unaona tunafanya makosa ambayo wengine walifanya zamani sana!
 
Wewe mpumbavu kama mtoa mada, kaanza kwa kuorodhesha watu wenye 'mamlaka' wanaopaswa kwenda ICC
Kikwete ana mamlaka gani,rais mstaafu atamuamuru nani?
 
Makosa ya viongozi wa dini kuchochea machafuko Rwanda
 

Attachments

  • Screenshot_2025-11-20-16-55-40-719.jpg
    132.6 KB · Views: 25

welcome to the post Christian world, watu wengi wanadharau na kukejeli Christianity lkn hawaelewi how Christian haki na usawa, wanachukulia kila kitu poa kwa kua vipo wanafikiri vimekuja tu, bila ya Christianity hakuna wa kutetea wasio na sauti, post Christian world ni communist na islam, na hili lililotokea tanzagiza ni kionjesho tu ya yale yanayokuja.

wanyonge watauliwa na kutupwa, haki zao kuporwa na hakuna wa kuwatetea, the whole international community na haki za kila raia ni Christian, bila ya Christianity mtakuwa na watawala ambao wanaweza kufanya mauaji na uonevu uliopitiliza bila kuulizwa na yoyote, communist china hajali serikali yako inakutreat vp maadamu inampa anachotaka.

angalia kinachoendelea sudani ulishasikia china akisema chochote?

in a post Christian world, wengi watalia na kusaga meno kuomba Christianity irudi hasa wachini na wasio na mtetezi, lkn ikishatoka hairudi, itakuwani dunia ya wenye nguvu, leo hii bado USA anaweza kutuma naval destroyer somewhere to protect the oppressed, lkn hizo siku zinaishia pia ...
 
Moja ya kitu ninacho kiona na cha wazi ni kuwa kama icc ita shindwa kuwa sdhughulikia hawa wadhalimu.

Basi wananchi walio umizwa au kufanyiwa vurugu wata anza kuchukua hatua ili kulipa kisasi.

The country is no longer in the balanced realm, I see a lot cracks which needs to be taken care of.
 
Polisi wa usalama barabarani hawawezi kushika bunduki kubwa vile (High Caliber Gun) bila kupewa kibali maalumu na mamlaka za juu. Kiutaratibu afisa mwenye dhamana ya ghala la silaha (Armoury) ndiyo anakamatwa. Hakuna mwingine.​
Mkuu je ikitokea Baada ya ripoti ya tume ya ndani...Serikali ikaamua ijitoe ICC kwa kupiga kura bungeni..kama .nkurunzinza alivofanya Burundi....unahisi kutakua na namna yeyote ile ya kuwawajibisha kwa
mauaji waliyofanya?au ndo itakua imetoka hiyo MALCOM LUMUMBA
 
Sasa jakaya anaingiaje hapo,au unaendeleza chuki alizokujaza askofu aliyesema 'mtu ukistaafu kaa mbali na serikali'!?
Wale Mashekhe na BAKWATA wanaotaka kuyachoma moto makanisa yote nchini ni yupi aliefanyiwa hivyo? Msikurupikie mambo bila kujua.
 
Napingana na hoja yako.
Haki, usawa, na ustawi hutokana na taasisi imara, na sio dini. Na pia kumbuka kuna ukristo kama tamaduni na si dini.
 
Napingana na hoja yako.
Haki, usawa, na ustawi hutokana na taasisi imara, na sio dini. Na pia kumbuka kuna ukristo kama tamaduni na si dini.

ndio maana nikaandika wengi hawaelewi how Christian haki, usawa na freedom, wengi mnafikiri hivi vitu vipo tu, siyo kweli kuna kazi kubwa sana na sacrifice zimefanyika watu wamepoteza maisha kwa karne nyingi kujenga hizo taasisi, kuna sababu kwa nini zote ziko na zilianzishwa na Christian western world na siyo communist au islam.

kuanzia mahakama za kimataifa, un, ngo's zzinazotetea wanyonge kama mfano wamasai wanaofurumushwa kwenye makazi yao huwezi kusikia communist china akitetea wamasai, ni Christians, Christians wanaweza kuwa wanaishi mbali kabisa labda australia huko lkn bado ukaona wanajituma na kujitoa kutetea humanity.

post Christian World itakuwa ngumu sana na evil...
 
Haya yanayotokea Tanganyika yametokea kote duniani. Tatizo ni kwamba tuliaminishwa kwamba sisi tuna kitu cha ziada kuliko majirani kama Rwanda, Kenya, Uganda, Kongo na Burundi. Sasa hiyo ngano (A Myth) imepasuka na ukweli umefahamika kwamba kumbe tuko sawa tu. Watanganyika na kuamini kwamba wao ni wa kipekee (Exceptionalism) ndiyo imetufikisha hapa. Watawala wanafanya chochote kile halafu wanajiliwaza kwa kusema hawa watu hawawezi kufanya lolote lile. Sasa wamefanya na wataendelea kufanya.

Kiuhalisia, serikali zote huwa zinazaliwa na kuanguka. CCM haina utofauti na serikali zilizowahi kuwepo hapa duniani kwa miaka zaidi ya 6000 tangu ustaarabu uanze. Mabadiliko huwa yanakuja tu (Change Is Constant), inategemea umejipangaje kuyakabili. Tanganyika haikujipanga kuyakabili mabadiliko na yamekuja kwa ghafla. Sisi tuko kama meli ya The Titanic ambayo iliaminiwa kwamba haiwezi kuzama, ila kiko wapi sasa. Serikali ya CCM na taasisi zake ndiyo viko ukingoni, sasa itategemea wataondoka kwa busara au lazima damu imwagike.

Kule Uingereza walinyonga mfalme wao, baadaye mtoto wake katawala akaanza ujinga uleule wa baba yake watu wakamfuata na ashukuru alikuwa na akili akakubali kuachia madaraka. Kule Urusi Ramanov walitawala kwa miaka zaidi ya 300 na hawakuamini kwamba kuna siku watatoka. Mwaka 1907 warusi waliandamana na kina Ramanov wakitumia shirika lao la kijasusi (THE OKHRANA) ambalo lilikuwa ni hatari waliaua, kuteka, kufunga na kutesa maelfu ya warusi. Wakajua yameisha.

Urusi imeingia kwenye WW1 raia wake wenye kisasi wakajiunga na Ujerumani kuhujumu nchi. Waliwasaidia wajerumani kuitwanga Urusi na kuitoa kwenye vita mwaka 1917, halafu wakaikamata familia iliyohusika na kuua maelfu ya ndugu zao miaka kumi nyuma. Walikamata familia nzima ya Ramanov na kuitandika risasi bila kumsazia hata mtoto. Vladmir Lenin ambaye alitoa hiyo amri alishuhudia kaka yake akinyongwa na serikali ya Ramanov, hivyo akalipiza kisasi.

KIUFUPI, kinachotokea barani Afrika hakina utofauti ni mapinduzi yaliyowahi kutokea Ulaya mnamo mwaka 1848 (1848 Revolutions) ambapo mataifa zaidi ya 50 yalighubikwa na vuguvugu za kutaka mabadiliko. Mapinduzi yalianzia Ufaransa mwaka 1848, ambapo walipindua kabisa mfalme wao na kuanzisha Jamhuri. Ila hasira zote hizi zilianza pale kabla ya maandamano, serikali ya Ufaransa kutumia nguvu kubwa kuanza kuua watu kikatili. Baada ya watu kuona Ufaransa imewezekana kikanuka Ulaya kote. Hivyo hawa Gen-Z wanapoona kwingine imewezekana basi fahamu fika lazima waige na hapa.

Kabla ya 1848, mataifa ya Ulaya yenye mifumo ya kifalme hayakutaka kubadilika, hivyo mwaka 1814 baada ya kumuangusha Napoleon yakapanga mkakati kule VIENNA (The Vienna Congress) wakishirikiana na Kanisa Katoliki kwamba wahakikishe wanaunda mtandao wa kupinga mabadiliko kutoka kwenye THEOCRATIC ABSOLUTE MONARCHIES to REPUBLICANISM. Kinara wa huo mchezo alikuwa ni Clemens Von Metternich ambaye aliunda mtandao wake wa kijasusi Ulaya nzima, kushughulikia wanaotaka mabadiliko. HAKUWEZA...

Ila mwaka 1848, Ujasusi wake na ule wa Kanisa vilifeli vibaya mno na watu walipindua kabisa falme na kuanzisha CONSTITUTIONAL MONARCHIES. Serikali iliyopona baada ya haya machafuko ni moja tu, PRUSSIA. Ukiuliza kwanini ilipona ni kwamba walifanya mabadiliko makubwa ya katiba na kuruhusu ULIBERALI ambapo watu waliruhusiwa kuishi maisha yao watayakayo. Mataifa yaliyokomaa kama AUSTRIA ambalo ndiyo lilikuwa na nguvu ulaya ilikula kwao. Baada ya hayo mabadiliko PRUSSIA ikajikuta inapata maendeleo kuliko taifa lolote Ulaya mwisho kuunganisha mataifa zaidi ya 30 na kutengeneza taifa la Ujerumani.

Hii CCM hii na TISS+PT+TPDF walioua maelfu ya Watanganyika hawataamini kitakachotokea hapa....
​
 
Hatari sana.
 
Forget about ICC, ile event haina quality ya kusajiliwa kwenye hiyo Mahakama kwa vile Serikali ilikuwa inatumia nguvu stahiki kutuliza riots ambazo zilianza kwa kuchoma miundombinu ya Serikali, vituo vya mafuta ya magari, mabasi ya umma na ya binafsi.

Nguvu pekee ambayo ilistahili kuyatuliza yale magenge ya wezi na waharibifu ilikuwa ni risasi za moto tu. Tear gas bombs na maji ya washawasha yasingesaidia kitu, yale hutumika kwenye issue ndogo kwenye fujo za sokoni au uwanja wa mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…